Mbona bado kuna taasisi za Umma nyingi tu ambazo zimeachwa bila ya kuunganishwa pamoja na kuunda taasisi moja??
Zipo taasisi au mashirika mengi sana ya Serikali ambayo yanapaswa kuunganishwa pamoja kwa sababu yanafanya kazi zinazofanana au kuingiliana ktk majukumu.
Hawa watu waliofanya kazi hii ya kuunganisha hizi taasisi hawajafanya Uchunguzi na Utafiti wa kina kuhusu suala hili.
Kwa maoni yangu ni kwamba, walipaswa kuualika umma wa Watanzania ili watoe maoni yao (Public Opinion) katika mchakato huu wa kuunganisha mashirika na taasisi za umma kabla ya kufikia hitimisho hili walilofanya. Sijui ni kwa nini Serikali huwa haitaki kuwashirikisha wananchi kwenye masuala nyeti kama haya ya ujenzi wa Taifa lao?? Sijui Serikali inaogopa kitu gani kuwashirikisha wananchi kwenye masuala kama haya??
Endapo kama Wananchi wangeshirikishwa kwenye suala hili, naamini kwa dhati kabisa kwamba wangeweza kuja na maamuzi au hitimisho ambalo ni bora zaidi kabisa kwa mustakabali mwema wa nchi yetu.
Hivi tunakwama wapi Watanzania ?????????????