Mashitaka ya Jaydee dhidi ya Gardner yaliishia wapi?

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
94,296
Reaction score
122,540
Hivi hili suala liliishia wapi?

Huyo bibie alienda mahakamani kumfungulia mashitaka huyo Kapteni au Kapteni aliomba radhi?

Kilichonifanya nikumbuke hili sakata ni hilo suala la Rais Magufuli [nendenni jukwaa la siasa na mtajua nazungumzia nini].

Huyo bibie naye hakutajwa jina bali alijihisi tu kuwa anayezungumziwa ni yeye.

Na kwa sababu hiyo baadhi yetu tuliona kwamba hata akienda mahakamani kufungua kesi, hiyo kesi, kama sheria ingefuatwa, basi hakuwa na nafasi ya kushinda kwa sababu madai yake yalikuwa frivolous.

Sasa ndo nawaza hapa hivi sokomoko zima liliishia wapi? Au ndo mapepo ya upepo tu...kwamba yalishapita na watu,ikiwemo wahusika, walishasahau....
 
Kichwa cha habari kinahamasisha,KUKOJOLESHWA.
 
Hahahhahhahhahha eti Rais Magufuli, hii sheria ina meno kwa Rais Magufuli pekee.
 
Ilikuwa kick tu yenye lengo la kupandisha hadhi ya ndi ndi ndi.
 
kukojoleshwa si tusi, lazima mwanasheria alimshauri, maisha yanasonga kila mmoja anakojoleshwa na mwingine.
 
Mpaka akitoa nyimbo mpya, ndio kesi inaendelea. Ni media tu zilikua zinafanya kazi yake
 
Hivi hili suala liliishia wapi?

Huyo bibie alienda mahakamani kumfungulia mashitaka huyo Kapteni au Kapteni aliomba radhi?

Kilichonifanya nikumbuke hili sakata ni hilo suala la Rais Magufuli [nendenni jukwaa la siasa na mtajua nazungumzia nini].

Huyo bibie naye hakutajwa jina bali alijihisi tu kuwa anayezungumziwa ni yeye.

Na kwa sababu hiyo baadhi yetu tuliona kwamba hata akienda mahakamani kufungua kesi, hiyo kesi, kama sheria ingefuatwa, basi hakuwa na nafasi ya kushinda kwa sababu madai yake yalikuwa frivolous.

Sasa ndo nawaza hapa hivi sokomoko zima liliishia wapi? Au ndo mapepo ya upepo tu...kwamba yalishapita na watu,ikiwemo wahusika, walishasahau....
Kumkojoza mtu sio jinai mkuu
 
Back
Top Bottom