Mashtaka ya Ugaidi: Shujaa wa 'Hotel Rwanda', Paul Rusesabagina akutwa na hatia. Ahukumiwa kifungo cha miaka 25


Hizi ndiyo zile mahakama zinazofuata maelekezo kutoka juu. Beberu huziita kangaroo courts.

Huko unapelekwa kuwapa uhalali wa kukushona mvua zilizokwisha amuliwa hata kabla ya kesi kuanza.

Hizo ndiyo zile mahakama za mwendazake na pia za huyu anayeendeleza zile kazi.

Hiiiiii bagosha!
 

Kwani kwa paka ahitaji hukumu ya kifo kutokea mahakamani kwa mtu kufia mikononi mwa dola?

Wako wapi kina Mawazo, Ben, wale wa kwenye viroba nk?

Ma dikteta huwa hawahitaji mahakama.

Wazimu wao ukiwapanda mbona mwamalizana kikuku tu?
 
ila jamaa nae kiazi sana kwanini ajiingize kwenye siasa da ila watu wa usalama nyoka sana nasikia rafiki yake wa kalibu ndio alimuuza walijua wanaenda burundi akashangaa ndege imetua rwanda
Vipi mbowe aache siasa?
 
Naomba kufahamu kuhusu huyu aliyehukumiwa na uhusika wake katika filamu ya Hotel Rwanda,,
Paul Rusesabagina ni mhutu ambae wakati wa mauaji ya kimbari Rwanda, alishiriki katika kuwaokoa wa tutsi zaidi ya 1000 akiwemo mkewe na wanae, wasiuwawe. Aliwaficha kwenye hotel aliyokuwa akifanya kazi, na kwa ushirikiano wa vikosi vya UN na kidogo AU aliweza kuwatoro kinyume na matakwa ya wahutu wenzie.
Hotel Rwanda ilikuwa ni filamu ya simulizi ya ujasiri huu aliyoufanya. Alipendwa na kuheshimika nchini na mpaka nje ya Rwanda, hataUlaya. Hatimae alikuja akawa rafiki pia wa Kagame. Uadui na Kagame ulianza alipokosoa mambo katika uendeshaji wa nchi.
Paul Rusesabagina ambae alikuwa raia wa Rwanda/Belgium alikimbia nchi na kujiunga na upinzani. Amehukumiwa miaka 25 jela kwa makosa ya kubambikiwa.
 
Safi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…