FT: Mashujaa FC 0-3 Simba SC l Ligi Kuu ya NBC l Lake Tanganyika l 14.05.2026. Yanga na Simba tofauti sasa ni pointi 2

FT: Mashujaa FC 0-3 Simba SC l Ligi Kuu ya NBC l Lake Tanganyika l 14.05.2026. Yanga na Simba tofauti sasa ni pointi 2

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Licha ya kuwa timu ngumu inapocheza kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika, Mashujaa FC imekubali kupoteza kwa magoli 3-0 dhidi ya Simba ambayo imeendelea kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kuutafuta ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Simba imebaki katika nafasi ya pili ikwa na pointi 52 katika michezo 23 nyuma ya Yanga yenye alama 54, timu zote zikilingana idadi ya mechi za kucheza.

Magoli ya mchezo huo yamewekwa wavuni na Clotous Chama (mawili) na Suleiman Mwalimu, yanaifanya Mashujaa FC kubaki na alama zake 26 katika michezo 23.

==========================​

Mashujaa FC wataikaribisha Simba SC leo Mei 14, 2026 katika Uwanja wa Lake Tanganyika, Kigoma, kuanzia saa 10:00 jioni, katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC wenye umuhimu mkubwa kwa mbio za ubingwa.

Kwa Simba SC, huu ni mchezo muhimu wa kurejesha kasi katika harakati za kutwaa taji la ligi, huku Mashujaa FC wakisaka matokeo mazuri mbele ya mashabiki wao wa nyumbani.

1778763784603.png

UPDATES 👇

Wachezaji wa Kikosi cha Mashujaa FC, wameahidiwa kiasi cha Tsh. Milioni 100 kama watashinda mechi ya leo dhidi ya Simba SC, na Wachezaji watapata Tsh. Milioni 50 kama watatoka sare.

1778758637733.png
Kuelekea mchuano wa leo wa Ligi Kuu ya NBC, takwimu za Soka Metrics zinaonesha tofauti kubwa ya mwenendo wa matokeo kati ya Tanzania Prisons na Fountain Gate FC katika michezo yao mitano ya hivi karibuni:

🔹 Tanzania Prisons (L-L-L-D-L):

Wenyeji wanaingia uwanjani wakiwa na wakati mgumu baada ya kushindwa kupata ushindi katika michezo yao mitano iliyopita:

Vipigo vinne: Wamepoteza michezo dhidi ya Simba (4-0), Singida Black Stars (1-2), Azam FC (0-3), na Yanga (3-0).

Sare moja: Matokeo yao bora katika mfululizo huu ni sare ya 1-1 dhidi ya KMC FC.

Changamoto: Safu yao ya ulinzi imeruhusu jumla ya mabao 13 katika michezo hiyo, huku wakifunga mabao 2 pekee.

🔹 Fountain Gate FC (W-W-L-W-L):

Wageni wanaingia uwanjani wakiwa na hali nzuri zaidi ya kisaikolojia baada ya kuvuna ushindi mara tatu katika michezo mitano iliyopita:

Ushindi mitatu: Wameibuka na ushindi dhidi ya KMC FC (2-3), Coastal Union (3-2), na Kagera Sugar (2-1).

Vipigo viwili: Wamepoteza michezo dhidi ya Mashujaa (1-2) na Simba (0-3).

Nguvu ya Mashambulizi: Wamefanikiwa kufunga jumla ya mabao 9, hali inayowaweka katika nafasi nzuri ya kutafuta mabao ugenini.

1778764184850.png

Hali ya Uwanja

Muonekano wa mazingira ya uwanja wa Lake Tanganyika baada ya mvua iliyonyesha kwa takribani dakika 20 maeneo ya Kigoma Ujiji, Kigoma.



VIKOSI VYA TIMU ZOTE;

Kikosi cha timu mwenyeji, Mashujaa F.C

1778762543786.png

Kikosi cha Simba S.C

1778762356671.png

Mechi imeanza

6' Goooal - Chama (Kona ya moja kwa moja inazama kimyani)
 
💘♥️💓💞🔥🔥🔥🔥❣️❣️❣️❤️❤️💖💝SSC
 
Yap Yap ni Leo, Mei 14 2026 Simba ndani ya Msitu mzito wa Sokwe Aina ya Mashujaa FC,

Mashujaa wamejiapiza kuikaanga Simba siku ya leo huku Simba wakiweka wazi kuwa kilichowapeleka Kigoma ni alama 3 tu na si vingine, kwani utalii wa kuona Sokwe si jambo lao.

Simba leo watakuwa na Presha kubwa zaidi ya kutafuta matokeo kwani tayari baada ya mpinzani wake Mkubwa Yanga kupoteza mchezo siku ya jana wanaona kama kuna mfupa unarandaranda hivi porini na wao ni fisi waufatilie huenda watapata chochote kitu

Simba ikiwa ya pili kwenye msimamo na alama 49 huku mashujaa wakiwa wa 9 kwenye msimamo na alama 26

Upi utabiri wako? Nani leo kucheka zaidi au wote watatoka wakiwa wababe?

Screenshot 2026-05-14 at 14-33-15 Instagram.png



Mechi ni majira ya saa 16: 15 jioni
 
Ndugu zangu hawa Fawanews wameingia kwenye 18 za Azam au?
Chimbo mbadala?
 
Watanzania wote wanaoshabikia simba ni mazuzu na hayajielewi,yanapayuka payuka tu.
 
Back
Top Bottom