Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Wanajamvi,

Kuna watu wanastahili nishani. Kukosa uoga kwao hakuelezeki. Wakati Mwendazake anafungwa watu, kuharibu biashara zao, kuwapakazia makosa yasiyokuwa na dhamana, na wengine kuuawa, hawa jamaa hawakunyaza kimya. Kilikuwa kipindi kigumu cha kuogopesha sana. Watu hawakuwa huru kuongelea serikali na siasa mbele ya watu wasiowafahamu. Hawa jamaa hawakuyumba. Hebu tuwataje:

1) Tundu Lissu - Kwa kifupi tu - Huyu alindamana kupinga udikteta. Alikuwa na jeuri ya kumwita Mwendazake dikteta uchwara. Alifunguliwa kesi zisizokuwa na mashiko. Alipigwa risasi 16 na Mungu akamponya. Baadae akaja kumpinga Mwendazake katika uchaguzi! Katika mazingira na hofu iliyojengwa na Mwendazake, huu ulikuwa ni ujasiri wa kupewa nishani.

2) Lawrence Mafuru - Huyu alikuwa ni Managing Director wa NBC Bank na baadae Msajili wa Hazina. Alikuwa na hali nzuri tu ya maisha na angeweza kunyamaza tu akaendelea na maisha bila bughudha. Wakati Mwendazake anatimua timua watu waliokuwa wanapingana naye. Mafuru alidiriki kupingana na Mwendazake mchana kweupe kwenye TV wakati akijua wazi kuwa atapoteza kazi yake. Mwendazake aliwashutumu watu wa benki kuwa wanweka fedha za serikali katika fixed deposit the kulamba faida kwa manufaa yao. Mafuru akiwa Clouds 360, alimpinga Mwendazake kwa kusema kuwa huo ni uongo kwa vile jambo hilo kwa taratibu za benki haliwezekani. Haikuchukuwa juma moja, Mafuru akafukuzwa kazi na Mwendazake.

3) Wakili Kibatala na jopo lake - Hawa jamaa wamesimama na wapinzani kwa kipindi ambacho Mwendazake alifanya Watanzania kuogopa Upinzani kama ukoma. Hawa jamaa hawakuterereka hata kidogo. Siyo wengi wenye msimamo huu ktk Tanzania. Wengi wanaangalia matumbo yao tu. Hawa jamaa wanastahili nishani kwa kutoogopa udikteta ule.

4) Mashangazi Maria Sarungi na Wakili Fatuma Karume - Hawa wamempinga Mwendazake hata pale ambapo watu waliogopa hata kukohoa katika vyumba vyao vya kulala. Wanastahili kupewa nishani ya ushajaa.

5) Taja wako kama wapo
Aisee hawa jamaa ni wazalendo kweli kweli. Magufuli alikuwa anatisha kama Dubu.

Mtu aliyesimama wazi wazi kumpinga kama TL tena akiwa mahakamani sio mtu wa kawaida
 
Kulikuwa na yule mama aliyekuwa mkurugenzi katika wilaya fulani. Aliulizwa kuhusu pesa za barabara akamjibu Mwendazake kuwa hawezi kuweka mafungu yote ya fedha ktk halmashauri katika kichwa chake. Siku kadhaa tu akatumbuliwa. Laana za watu zilimmaliza mwendezake.
Yule injinia wa magorofa. alimjibu jiwe kisomi mpaka alikaa mzee Jiwe
 
Peter Msigwa alikataa pesa za familia kutoka kwa mwendazake kulipia faini yake kutoka gerezani.
Wanajamvi,

Kuna watu wanastahili nishani. Kukosa uoga kwao hakuelezeki. Wakati Mwendazake anafungwa watu, kuharibu biashara zao, kuwapakazia makosa yasiyokuwa na dhamana, na wengine kuuawa, hawa jamaa hawakunyaza kimya. Kilikuwa kipindi kigumu cha kuogopesha sana. Watu hawakuwa huru kuongelea serikali na siasa mbele ya watu wasiowafahamu. Hawa jamaa hawakuyumba. Hebu tuwataje:

1) Tundu Lissu - Kwa kifupi tu - Huyu alindamana kupinga udikteta. Alikuwa na jeuri ya kumwita Mwendazake dikteta uchwara. Alifunguliwa kesi zisizokuwa na mashiko. Alipigwa risasi 16 na Mungu akamponya. Baadae akaja kumpinga Mwendazake katika uchaguzi! Katika mazingira na hofu iliyojengwa na Mwendazake, huu ulikuwa ni ujasiri wa kupewa nishani.

2) Lawrence Mafuru - Huyu alikuwa ni Managing Director wa NBC Bank na baadae Msajili wa Hazina. Alikuwa na hali nzuri tu ya maisha na angeweza kunyamaza tu akaendelea na maisha bila bughudha. Wakati Mwendazake anatimua timua watu waliokuwa wanapingana naye, Mafuru alidiriki kupingana na Mwendazake mchana kweupe kwenye TV wakati akijua wazi kuwa atapoteza kazi yake. Mwendazake aliwashutumu watu wa benki kuwa wanweka fedha za serikali katika fixed deposit the kulamba faida kwa manufaa yao. Mafuru akiwa Clouds 360, alimpinga Mwendazake kwa kusema kuwa huo ni uongo kwa vile jambo hilo kwa taratibu za benki haliwezekani. Haikuchukuwa juma moja, Mafuru akafukuzwa kazi na Mwendazake.

3) Wakili Kibatala na jopo lake - Hawa jamaa wamesimama na wapinzani kwa kipindi ambacho Mwendazake alifanya Watanzania kuogopa Upinzani kama ukoma. Hawa jamaa hawakuterereka hata kidogo. Siyo wengi wenye msimamo huu ktk Tanzania. Wengi wanaangalia matumbo yao tu. Hawa jamaa wanastahili nishani kwa kutoogopa udikteta ule.

4) Mashangazi Maria Sarungi na Wakili Fatuma Karume - Hawa wamempinga Mwendazake hata pale ambapo watu waliogopa hata kukohoa katika vyumba vyao vya kulala. Wanastahili kupewa nishani ya ushajaa.

5) Taja wako kama wapo
 
Jenerari Ulimwengu.
Maneno ya Jenerali Ulimwengu mwaka 2016 yametimia kwa Tanzania kumpata kiongozi Samia the Law Giver mwaka huu 2021 ingawa rear guards yaani MATAGA hawapendi na wanafanya juhudi kubwa kupinga mabadiliko anayofanya Mh. Rais Samia Suluhu Hassan the Law Giver
Mapema kabisa Jenerali Ulimwengu :

14 Juni 2016

Jenerali Ulimwengu : Kunakuwa na wakuu wa nchi wanaitwa Law givers

Jenerali Ulimwengu: Kinachoendelea serikalini, Tumerudi nyuma miaka 50 kwenye demokrasia

Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa lakini ukiangalia picha kubwa ni kwamba tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia. Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ulimwengu kasema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete. Ulimwengu ameendelea kwa kusema Mheshimiwa Kikwete anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali na pili kuzima matumaini ya wananchi na kuwaacha wanarandaranda ambayo inaweza kuleta machafuko baadae kama haitawezekana kutengeneza katiba ambayo itajenga mustakabali wa wananchi wa Tanzania.
 
Back
Top Bottom