Mashujaa wa kweli Tanzania hawakumuogopa Hayati Dkt. Magufuli

Aisee hawa jamaa ni wazalendo kweli kweli. Magufuli alikuwa anatisha kama Dubu.

Mtu aliyesimama wazi wazi kumpinga kama TL tena akiwa mahakamani sio mtu wa kawaida
 
Kulikuwa na yule mama aliyekuwa mkurugenzi katika wilaya fulani. Aliulizwa kuhusu pesa za barabara akamjibu Mwendazake kuwa hawezi kuweka mafungu yote ya fedha ktk halmashauri katika kichwa chake. Siku kadhaa tu akatumbuliwa. Laana za watu zilimmaliza mwendezake.
Yule injinia wa magorofa. alimjibu jiwe kisomi mpaka alikaa mzee Jiwe
 
Peter Msigwa alikataa pesa za familia kutoka kwa mwendazake kulipia faini yake kutoka gerezani.
 
Jenerari Ulimwengu.
Mapema kabisa Jenerali Ulimwengu :

14 Juni 2016

Jenerali Ulimwengu : Kunakuwa na wakuu wa nchi wanaitwa Law givers


Jenerali Ulimwengu: Kinachoendelea serikalini, Tumerudi nyuma miaka 50 kwenye demokrasia

Jenerali Ulimwengu akiwa kwenye kongamano la kigoda cha mwalimu Nyerere chuo kikuu cha Dar es Salaam, amesema pamoja na hatua nzuri anazochukua Rais wa sasa, Mheshimiwa John Magufuli ambazo zimepongezwa lakini ukiangalia picha kubwa ni kwamba tumerudi nyuma kama miaka 50 kwenye demokrasia. Ulimwengu amesema ni kutokana na kufinya uhuru wa kujieleza na hususan kwa kufinya uhuru wa wawakilishi wa wananchi ndani ya bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania. Ulimwengu kasema katika hili hamna kifimbo cha uchawi cha kujinasua isipokuwa mchakato wa katiba ambao ulichukua fedha nyingi kisha ukaachwa njiani na Mheshimiwa Kikwete. Ulimwengu ameendelea kwa kusema Mheshimiwa Kikwete anatakiwa kupelekwa mahakamani kujibu mashtaka kwa kusababisha hasara kubwa kwa serikali na pili kuzima matumaini ya wananchi na kuwaacha wanarandaranda ambayo inaweza kuleta machafuko baadae kama haitawezekana kutengeneza katiba ambayo itajenga mustakabali wa wananchi wa Tanzania.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…