Mejasoko
JF-Expert Member
- Oct 20, 2019
- 298
- 600
Wakati meli ya Titanic inazama ilikua imembeba Billionare John Jacob Astor IV, Pesa aliyokua nayo alikua ana uwezo wa kujenga Meli zaidi ya 30 kama hiyo ya Titanic, Titanic ilijengwa kwa mwaka 1912 kwa $7.5 million ambayo kwa sasa ni sawa na $ 400 million ambayo ni sawa na Tsh 1,055,290,076,000.00, Trilion moja billion hamsini na tano million miambili tisini na elfu sabini na sita, sasa yeye alikua na utajiri zaidi mara 30 ya huo.
Meli hiyo ya Titanic iliyokua inatoka Southampton Uingereza kwenda New york city (USA) wakati inazama walitumia sheria ya "Women and children first " wanawake na watoto kwanza ndo waokolewe kwa kupewa lifeboats na Captain Edward John Smith ndo atakua mtu wa mwisho kushuka kwenye meli, Lakini tajiri John Jacob Astor IV alipewa nafasi ya upendeleo yeye ashuke pamoja na wale wanaookolewa wakwanza, lakini tajiri John Jacob Astor alikataa kushuka na nafasi yake kwenye lifeboat akasema wapande watoto wawili walioonekana kuwa na hofu sana.
Billionare mwingine Isdor Straus tajiri mkubwa wa marekani aliekua mmiliki wa Macy's Store nae alipewa nafasi ya upendeleo ya kuokolewa lakini nae pia alikataa kushuka akasema "Siwezi kupanda lifeboat kabla ya wanaume wenzangu hawajaanza kupanda", Mke wake Ida Straus alipoona mume wake kakataa kupanda lifeboat nae akakataa kupanda akaamua kubaki kwenye meli huku ikiwa inazama taratibu na nafasi yake kwenye lifeboat akasema apande msaidizi wake anaeitwa Ellen Bird.
Ida Straus akakubali muda wake wa mwisho duniani aumalize akiwa na mume wake Isdor Straus.
Matajiri hao walichagua kuachana na mali zao na uhai wao na siyo kuvunja sheria iliyowekwa ya "Women and children first " licha ya kuwa walipata nafasi ya kuwa miongoni mwa watu 705 waliopona kwenye ajali hiyo ila wao waliamua kuwa mongoni mwa watu 1500 waliofariki kwa kuthamini watu wengine kuliko nafsi zao.