Mashujaa wa uhuru waliosahauliwa: Makala ya Al Haj Abdallah Tambaza

Mashujaa wa uhuru waliosahauliwa: Makala ya Al Haj Abdallah Tambaza

Mwandishi Mbona hujazitaja familia mbili? Bomani na Mbowe (baba wa Freeman) mengine nayakubali hasa laana iliyopo CCM ambayo kimsingi laana hiyo imeasisiwa na Nyerere mwenyewe.

Hacena,
Nawataja watu kwa muktadha ya kile ninachoeleza.
Paul Bomani nimemtaja katika kitabu changu.

Msome hapa chini na hii ilikuwa mwaka 1953:

Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima
kuueleza umma matokeo ya safari ya Kirilo kwenye Umoja wa
Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha
fedha za kupelekamsafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza
umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika
walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.

Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha

Kandoro,
Kirilo na Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo.

Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa Kirilo
ampelekee hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha
kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.

Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na
fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo
zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako Kirilo alizichukua.

Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile
kamatiilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya
fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na
Shinyanga.

Rais wa chama cha TAA, Kanda ya Ziwa, Paul Bomani aliipokea ile
kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika
jimbo lote.

Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini
Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.

(Kutoka: ''Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes...'')
 
Mwandishi Mbona hujazitaja familia mbili? Bomani na Mbowe (baba wa Freeman) mengine nayakubali hasa laana iliyopo CCM ambayo kimsingi laana hiyo imeasisiwa na Nyerere mwenyewe.

Mwanahistoria wetu mbona michango ya watu kama John Mwakangale, job Lusinde, George Kahama ,Peter Said Siyovelwa, Nangwanda sijaona, Jeremiah Kasambala hujaiainisha au wao hawastahili kukumbukwa ila hawa wa pwani tu? Au kwa vile majina yao hayashabihiani na utashi wako? Juu ya hayo, ukumbuke kuwa wakati wa kupigania uhuru UTP [ United Tanaganyika Party] ndio kilikuwa chama cha siasa cha wazungu na kiongozi wao alikuwa akiitwa Balydon na hao uliowataja wewe walikuwa ni wanachama na most likely sympathetic to the colonial cause!! Kiongozi wa UTP alikuwa mzungu na sio mwarabu wala mhindi!!
 
Mzee Mohamed Said Vitabu Vyako Vinapatikana Stores Gani, Na Vipi Kuhusu Bei Zake
 
Mzee Mohamed Said Vitabu Vyako Vinapatikana Stores Gani, Na Vipi Kuhusu Bei Zake

Nemo Judex,
Kitabu cha Abdul Sykes kinapatikana A Novel Idea Bookshop Slip Way
Masaki, Soma Bookshop Mikocheni, Ibn Hazm Media Centre Msikiti wa
Manyema na Mtoro na pia Tanzania Publishing House (TPH) Samora Avenue.
 
Mwanahistoria wetu mbona michango ya watu kama John Mwakangale, job Lusinde, George Kahama ,Peter Said Siyovelwa, Nangwanda sijaona, Jeremiah Kasambala hujaiainisha au wao hawastahili kukumbukwa ila hawa wa pwani tu? Au kwa vile majina yao hayashabihiani na utashi wako? Juu ya hayo, ukumbuke kuwa wakati wa kupigania uhuru UTP [ United Tanaganyika Party] ndio kilikuwa chama cha siasa cha wazungu na kiongozi wao alikuwa akiitwa Balydon na hao uliowataja wewe walikuwa ni wanachama na most likely sympathetic to the colonial cause!! Kiongozi wa UTP alikuwa mzungu na sio mwarabu wala mhindi!!

Bulesi,
Nitaanza na niliowataja katika kitabu ambao wewe unasema sikuwataja.

Job Lusinde
nimemtaja pamoja na harakati za Omari Suleiman na Haruna
Taratibu Dodoma wakati wanataka kufungua tawi la TANU mwaka wa 1955.

Nangwanda Sijaona nimemtaja pamoja na Suleiman Masudi Mnonji Lindi tka
wa 1961.

Waliobaki Peter Said Siyovelwa, Jeremiah Kasambala sikuwataja.
Sikuwataja si kwa sababu ulizotoa wewe.

Sikuwataja kwa kuwa hawakuingia katika yale niliyokuwa nayaandika.
Mukhtadha wowote wa kitabu una mipaka yake.

Lakini ikiwa kuna mambo muhimu ya kukumbukwa ambayo hayajaandikwa
ambayo watu hao wamefanya itakuwa vyema kama wewe utatuandikia
tuyasome.

Umekosea jina la kiongozi wa UTP.

Jina lake ni Ivor Bayldon siyo Balydon na makamu wake alikuwa Sheikh
Hussein Juma.

Bulesi,
Nami nina swali ningepeda kukuuliza.

Kuna mahali popote katika historia hii ya uhuru wa Tanganyika Omari
Suleiman
katajwa au Haruna Taratibu au Suleiman Masudi Mnonji?

Nakusihi soma kitabu changu kwanza ndiyo urejee hapa majlis kwa
mjadala
 
Kwa kulipa fadhila na kuonyesha shukrani zake, kwa kipindi fulani, Nyerere alikuwa anamlea pale kwake Msasani, mjukuu wa Mzee Mshume aitwaye Mwinyi Kiyate, baada ya babake na babu kufariki.

..hii habari ni mpya kwangu.
 
Back
Top Bottom