Mwandishi Mbona hujazitaja familia mbili? Bomani na Mbowe (baba wa Freeman) mengine nayakubali hasa laana iliyopo CCM ambayo kimsingi laana hiyo imeasisiwa na Nyerere mwenyewe.
Hacena,
Nawataja watu kwa muktadha ya kile ninachoeleza.
Paul Bomani nimemtaja katika kitabu changu.
Msome hapa chini na hii ilikuwa mwaka 1953:
Uongozi wa TAA Makao Makuu ulianza kampeni ya nchi nzima
kuueleza umma matokeo ya safari ya
Kirilo kwenye Umoja wa
Mataifa kuhusu mgogoro wa ardhi ya Wameru na vilevile kuchangisha
fedha za kupelekamsafara mwingine katika Umoja wa Mataifa kuueleza
umoja huo kuwa Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini na Watanganyika
walikuwa sasa na haki ya kudai uhuru wao.
Kamati ya TAA ya watu watatu iliyowajumuisha
Kandoro, Kirilo na
Abbas Sykes iliundwa kwa ajili hiyo.
Ally Sykes akiwa mweka hazina msaidizi wa TAA aliombwa
Kirilo
ampelekee hawala ya posta Usa River kama nauli ya kumwezesha
kusafiri hadi Dodoma kujiunga na ile kamati ya watu watatu.
Kulikuwa hakuna huduma ya fedha katika posta ya Usa River na
fedha zile zilikaa hapo kwa muda bila ya kuchukuliwa hadi hapo
zilipopelekwa posta ya Arusha mjini ambako
Kirilo alizichukua.
Kuanzia tarehe 26 Septemba, 1953 kwa takriban mwezi mmoja ile
kamatiilitembelea na kuhutubia mikutano ya hadhara, ikikusanya
fedha Dodoma, Mwanza, Bukoba, Ukerewe, Tarime, Musoma na
Shinyanga.
Rais wa chama cha TAA, Kanda ya Ziwa,
Paul Bomani aliipokea ile
kamati ya watu watatu na kuhutubia mikutano pamoja nao katika
jimbo lote.
Bomani aliwaambia wanachama wa TAA na wananchi wote mjini
Mwanza kuhusu umuhimu wa kuchanga fedha kwa kwa kusudio hilo.
(Kutoka: ''Maisha na Nyakati za
Abdulwahid Sykes...'')