Mashujaa waivua nguo Simba Taifa, timu 32 zafuzu simba haimo

leo sio tena mna kikosi kipana, imekuwa kocha hafai
 
[emoji1] [emoji1] [emoji1]

Si kwa povu hili
Siyo Povu, najaribu kuwafunda hawa vijana wetu.
Kwamba katika maisha ili ufanikiwa ni lazima utafute fulsa,wao wameisha ipata ya kusajiriwa Simba.
Cha pili lazima ufanye kazi kwa bidii na maarifa ili unufaike na ile fulsa uliyoipata.
Nia Ajabu wale vijana wa timu ya Bush men, iwafunike timu ya Born town tena mjini ya Kariakoo hadi,
Jogoo la Shamba Liwike Mjini ghafla namna hii.
 
Ndiyo hapo unapokubaliana na hoja yangu kwamba si sahihi kuwasajili kwa pamoja wachezaji wenye uwezo sawa kwenye nafasi moja. Messi anatosha kuwa striker wa kwanza wa Barcelona, hatafutwi nyota mwengine mwenye uwezo kama wake kusajiliwa. Ndio maana, mathalan, Higuain akaondoka F C Milan ili kumpisha Christiano. Vingunevyo Higuain angebaki kuwa kama unavyomlaumu Salamba dhidi ya Kagere. Usitarajie, mathalan, kwamba Haji Mwinyi atakuza kiwango chake akiwa chini ya kivuli cha Gardiel Michael pale Yanga. Hilo ndio kosa la usajili wa Simba msimu huu. Usimtegemee Niyonzima kujaza viatu vya Chama, au Rashid Mohamed vya Okwi, au kama ulivyoona jana kwa Dida dhidi ya Manula. Simba imekusanya mchezaji zaidi ya mmoja mwenye uwezo mkubwa kwenye kila nafasi kwa kuamini kwamba yeyote atakayeingizwa ataendelea kuwa mzuri. Si hivyo. Usije ukashangaa kukuta huyu mzuri asiyecheza ndani ya Simba akaishia kuwa dhaifu kuliko yule dhaifu anayepata nafasi ya kucheza kwenye timu nyengine. Ndicho kilichoonekana jana dhidi ya Mashujaa. Ndio maana golikipa wa Mashujaa halaumiwi licha ya uanagenzi wake kama anavyolaumiwa Dida mzoefu (aliyekosa nafasi ya kucheza mara kwa mara).
 
Dah! kikosi kipana wana uwezo wa kucheza mechi mbili kwa wakati mmoja , baada ya mechi ya jana msemaji wenu amesemaje kuhusu upana wa kikosi chenu
 
Unataka kikosi cha KWANZA KICHEZE BONANZA ukiumiza wachezaji tarehe 11.1.2019 unakutana na ESPERANCE,AL AHLY NA TP MAZEMBE unachezesha kikosi cha pili si eti?.hivi huwa mnafikiri kwa kutumia vitu gani?..
 
Unataka kikosi cha KWANZA KICHEZE BONANZA ukiumiza wachezaji tarehe 11.1.2019 unakutana na ESPERANCE,AL AHLY NA TP MAZEMBE unachezesha kikosi cha pili si eti?.hivi huwa mnafikiri kwa kutumia vitu gani?..
Lakn mkuu, mbona hao wa kikos A wanaeza umia tu hata mazoezn!!? Mf. Mkude na Dante waliumia mazoezn wakawakosa Lesotho (mnirekebishe kama nmevuruga kumbkumb)
 
Matokeo ya kawaida mchezoni hata Barcelona inafungwaga na Getafe
 
Hata kikosi cha kwanza cha Simba kwa sasa sio kizuri na hii inatikana na kocha tuliyenae.

Ukitaka kujua kocha mzuri ni kwenye upangaji time na subs. Jamaa uwezo wake ni mdogo sana na believe me ubingwa mwaka huu tutausikilizia redioni
 
Lakn mkuu, mbona hao wa kikos A wanaeza umia tu hata mazoezn!!? Mf. Mkude na Dante waliumia mazoezn wakawakosa Lesotho (mnirekebishe kama nmevuruga kumbkumb)
Mkuu kwa hatua Simba ilipo sasa hivi sio wa kuwaza mechi hizo(hadi hapa tulipo tuna Billion 1.2,) tukikomaa tu na makundi vizuri tukawa wa pili kwenye kundi tunapata Billion 2.1,hata tukiishia hapo.Hadi hapo huoni ni mashindano yapo tunapaswa kuweka nguvu zaidi?.Mtibwa ndiye bingwa mtetezi wa mashindano hayo na hadi naandika hapa HAJALIPWA hata sent 5,kwanini tusikomae na EPL & Kilabu Bingwa?.

Note;Simba haijazidiwa uwezo na Mashujaa kutolewa,imejitoa kimkakati tu,
Rejea;
*Maneno ya Manara kabla ya mechi
*Goli la Dida alilofungwa(angalia reaction yake)
 
Hata kikosi cha kwanza cha Simba kwa sasa sio kizuri na hii inatikana na kocha tuliyenae.

Ukitaka kujua kocha mzuri ni kwenye upangaji time na subs. Jamaa uwezo wake ni mdogo sana na believe me ubingwa mwaka huu tutausikilizia redioni
Kitakacho wanyima Simba ubingwa ni ratiba mbovu na mlindikano wa mechi watalazimika kucheza back to back na sio kikosi Chao Simba wanna kikosi kizuri kuliko Yanga na Azam
 
Mpira unaujua
 
Acha kujipa moyo we dada ina maana hujui umuhimu wa fa leo? Mbona mapinduzi mnapeleka timu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…