Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 76,107
- 160,001
Brenda na Lydia walikuwa ni wahudumu wa ndege ya Precision iliyopata ajali ziwani kule Bukoba.
Mabinti hawa warembo ni kama mchango haupo au ni kidogo sana, lakini ni hawa ndio walio watuliza akili abiria waliokuwa katika taharuki kubwa, ni hawa ndio waliogawa life jackets, na pia ni hawa ndio kwa kushirikiana na Majaliwa waliweza kufungua mlango.
Licha ya kwamba hawa walikuwa kazini lakini hakika waliifanya kazi yao kwa weledi mkubwa sana, hivyo basi wanastahili kuheshimiwa na kutambulika rasmi kama mashujaa wa taifa.