- Source #1
- View Source #1
Wakuu, nimekutana na haka ka video huko TikTok mtu anauliza kuwa anapigwa shoti na mashuka yake je chanzo ni nini?
- Tunachokijua
- Hali ya nguo ama mashuka kupiga shoti inatokana na cheche zinazozalishwa na umeme tuli (static electricity). Hii hutokea pale ambapo vitu viwili vinagusana katika mazingira yenye hewa isiyo na unyevu hasa wakati wa baridi.
Tovuti mbalimbali zimeeleza baadhi ya mambo yanayoweza kuchangia hali hii kuokea ambayo ni; aina ya kitambaa pamoja na hewa kavu wakati wa baridi.
Je, umeme huo una madhara?
Inaelezwa kuwa umeme unaozalishwa hapa ni mdogo na hivyo hauwezi kuwa na madhara makubwa ya kumdhuru mtu, ingawa inashauriwa kuweka mbali vifaa vya kielektroniki kama vile simu ya mkononi kwani umeme huo unaweza kuingia ufanyaji kazi wa vifaa hivyo.
Njia za kuondoa umeme huo.
Zipo njia mbalimbali zinazotajwa zinazoweza kutumika kuondoa hali hiyo, zipo za haraka, njia za asili na zile za kudumu kulingana na wakati huska.
Njia za haraka
- Nyunyizia maji kidogo kwa kutumia chupa (Spray bottle) kwenye nguo, shuka ama blanketi. Unyevu wa maji unaua ule umeme haraka sana.
- Pitisha ‘hanger’ ya chuma ya kuning’iniza nguo iliyotengenezwa kwa chuma tupu kwa kuigusisha ama kuipitisha kwenye kitaa husika.
- Karatasi za kukaushia (Dry sheets), hii ni iwapo unatumia mashine za kukaushia nguo changanya nguo pamoja na karatasi hizi.
- Tumia ‘humidifier kifaa maalum kinichaoongeza unyevu kwenye hewa ya chumba. Unyevu husaidia kuondoa umeme kwenye blanketi.
- Tumia magadi ya soda wakati unafua kitambaa husika.
- Anika nguo zako juani badala ya mashine za kukaushia nguo, ingawa pia usizianike kwa muda mrefu.
- Tumia siki (vinegar) wakati wa kufua
- Tumia mablanketi ya asili yaliyotengenezwa kwa pamba ama sufu hashiki umeme ukilinganisha na yale ya polister ama nailoni (nylon).
- Usikaushe kitambaa kupita kiasi
- Ongeza unyevu chumbani. Kama unaishi eneo lenye hewa kavu sana au unatumia kiyoyozi (AC) sana, kutumia kifaa cha kuongeza unyevu hewani (Humidifier) chumbani kwako kutamaliza kabisa tatizo hili.