Masijala wanakwamisha shughuli za Watu na Serikali

Masijala wanakwamisha shughuli za Watu na Serikali

fungi06

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2020
Posts
738
Reaction score
1,017
Wakuu ivi huyu masjal ni nani?

Maana sikuizi ofisi za serikali nyingi ukienda kufwatilia maswala ya msingi..unaskia "barua yako haijajibiwa na masijala njoo mwezi ujao au mwakani njoo" Kirahisi rahisi ivyo?

Ikumbukwe kua binadamu anaishi vizuri kwa kumtegemea binadamu mwenzake..

Pale unapokwamisha shughuli za wenzako kwa maksudi, eti masjala ajajibu. Au itume kwa masjala.

Haya mambo ya masjala yanaboa kichizi.

Alafu ndo juzi naskia adi kwenye vyombo vya habari, eti mkuu wa nchi analalamika na yeye awa MASJALA wanakwamisha mpka miradi ya taifa 🤣🤣

Ivi kweli mjibu makaratasi ya barua anaweza kuichezesha adi serikali!

Mimi naona kama AI itatuuwa kwa kufanya maamuzi sahihi kwa mda mchache basi wacha ituuwe ila sio kuuliwa na mcheleweshaji majibu ambae majibu yake kwa namna kubwa huenda sio sahihi..

Kweli napongeza mno mkuu wa nchi kusupport ukuwaji wa technology tupunguze idadi ya mizoga jamani, mtu unakuta unastaili kulisha familia, baba mgonjwa, mama hana kazi ananitegemea,

Alafu nafanya malipo yote stahiki naishia kuambia huduma hii utaipata ukijibiwa barua yako kwa masjala🤔🤔

Kweli inakatisha tamaa na sura zinazidi kufubaha..mtaani ni bora ukumbane na changamoto ya njaa kuliko ukumbane na ubabaishaji unaofanywa na baadhi ya waajiriwa wa serikalini.

Mnatuongezea kwakiasi flani mzigo wa umaskini.. Au ndo mpaka rushwa itolewe ndo upate majibu ya barua yako?

Muwe mnaweka description zinazo eleweka sio nenda rudi, nenda rudi, nenda rudi!! Hell.

Mfumo utengenezwe unaoweza kujisimamia izo Bilion 210 na kitu zikatendewe haki kwenye hii sekta ya communication. Tunachoka izi akili za mambuzi wanaolipwa mwisho wa mwezi kutuongezea ugumu wa maisha

Sasa basi jamani masjala kama uwezi kujibu barua ndani ya mda sasa ni mda wakukaa pembeni na kutuacha tuendeleze taifa sasa
 
Masjala (Registry) ni idara ndani ya ofisi inayohusika na Records Management.

Hupokea na kutoa barua zote za Taasisi husikia.

Kimsingi Masjala Kama Masjala huwa haiwezi kujibu barua, Bali barua barua zinazoingia na kutoka lazima zipitie Masjala Kwa ajili ya kuweka kumbukumbu.

Shida Ipo Kwa hao wamama wa Masjala, huwa hawasemi ukweli, wasumbufu Sana, wasiojali na kuthamini muda wa mteja.

Ukienda taasisi yoyote ya umma, make sure unahudumia hata na mwanaume mwenzio anaweza kukupa majibu ya kueleweka kuliko wamama na wadada.
 
Yaani ukiondoa polisi wengine wanaojiona miungu watu ni Masjalala za nji hii,wanaona bila wao hakuna kitu utafanya duniani,wakishakaa na mabulungutu ya faili wanaona wao ndio kitengo chenyewe,wengi ni wazee na wanga wakubwa ndio maana hawafukuziki,Imagine teknolojia imekuja ila Vibabu vipo tu,kuna namna.
 
Back
Top Bottom