WilsonKaisary
JF-Expert Member
- Apr 4, 2017
- 392
- 949
MASIJALA YA KITUME YA VATIKANI - Vatican Apostle Archive.
Imekuwepo zaidi ya karne 3 sasa, ni KIINI cha SIRI za Kanisa KATOLIKI Duniani. Mwanzoni iliitwa MASIJALA YA SIRI ikabadilishwa jina 2019. Hakuna anaeruhusiwa kuingia isipokua kibal maalumu kutoka kwa PAPA.
Mwanzoni ilikuwa ikiitwa "Vatican Secret Archive" yaani Masijala ya Siri ya Vatikani lakini baadae wakaona kuwa neno "siri" haliakisi ukweli wa masijala hiyo. Sio masijala ya SIRI bali ni ya faradha kwa maana ya kwamba inahifadhi nyaraka binafisi za kiti cha Baba Mtakatifu.
Zikiwemo barua, mikataba na nyaraka nyingine baina ya Baba mtakatifu na viongozi wa mataifa mengine duniani. Kutokana na mkanganyiko wa neno siri "Secret" na faragha "Private". Mwaka 2019, Papa Francis alibadilisha jina kutoka "siri" na kuuita Masijala la Kitume ya Vatikani.
Masijala hii ilianzishwa mwaka 1612, kufuatia agizo la Papa Paul 5, lililosisitiza kanisa kuhifadhi rekodi zake. Miaka ya 1790's wakati Napoleon anaiteka Italy aliagiza vitu vilivyo kwenye masijala hiyo vipelekwe ufaransa kwa awamu kulingana na wasaidizi wake watakavyoona.
Na alipokua mtalawa rasmi mwaka 1804, aliagiza masijala hiyo yote ihamishiwe Paris, Ufaransa. Na mpaka kufikia mwaka 1813 nyaraka zote zaidi ya 3000 zilikua tayari zimeshahamishiwa ufaransa. Mwaka 1814 baada ya utawala wa Nepoleon kuanguka serikali mpya ya ufaransa iliamua.
Kuirudisha masijala hiyo vatikani, japo ilitoa pesa kidogo kwaajili ya zoezi hilo. Hivyo vatikani wakauza baadhi ya mali vyao ili kuweza kuirudisha nyumbani masijala yao. Ila inaaminika kwamba kutokana na pesa hafifu kwa wakati huo, zaidi ya robo tatu ya nyaraka hazikurudi.
Tangu kuanzishwa kwake mpaka enzi za Nepoleon na baadae kurudi tena Vatikani, masijala hiyo imedumisha usiri wa hali ya juu, hakuna aliyekuwa na uwezo wa kujua kilichomo ndani ya masijala hiyo isipokuwa watu wenye kibali cha juu cha ulinzi na usalama. Mwaka 1879.
Papa Leo 13 aliamua kulegeza kidogo masharti kwa kuwaruhusu wana historia kuingia na kusoma nyaraka zilizokuwa kwenye masijala hiyo. Japo kumekuwa na mipaka ya nani aingie na nani asiingie ili kudhibiti waumini wa kiprotestanti kupotosha maana ya mambo yaliyomo ndani.
Hii ni kutokana na machapisho ya mwana historia Theodore Sickel ambayo yalichapisha mwaka 1881 akilishutumu kanisa kwa kufoji baadhi ya mikataba. Utaratibu wa kupitisha mchujo mkali kwa watu wanaopata nafasi ya kuingia kwenye masijala hiyo umeendelea kwa kipindi chote hicho.
Masijala hiyo iko kwenye chumba cha chini ya ardhi karibu na Maktaba kuu ya vatikani. Wanaoruhusiwa kuingia wanapewa kadi maalumu, lakini pia ni lazima watume maombi ya barua kwa Papa kabla ya kupata kibali hicho. Barua ni lazima itoke kwenye taasisi au chuo kinachoaminika.
Licha ya kuwa na maelfu ya maombi kutoka duniani kote ila Masijala inapokea watu 60 tu kila siku. Pia wanaoruhusiwa kuingia hawaruhusiwi kusoma kila kitu.
VATICAN APOSTLE ARCHIVE au MASIJALA YA KITUME YA VATIKANI inaaminika kuwa ndiyo masijala ya siri kuliko zote duniani, ina nyaraka za Mapapa wote tangu karne ya 8.
'MWISHO.
Ifahamike wazi baada ya Roman Empire kuanguka, likaanzishwa dhehebu la Roman Catholic kwa lengo la kurestore Roman empire.
Kiongozi papa anabeba majukumu mawili Kama kiongozi wa dini na Kama kiongozi wa nchi ya Vatican, Papa huwa anahudhuria vikao vya maraisi wa Dunia vya umoja wa mataifa Yani UN akibeba dhamana Kama raisi wa Vatican. Vatican ina pass port, fedha, jeshi na serikali, mpaka taasisi za ki-intellejensia za usalama.