Masikini UKAWA


A serious Disgrace kwa chama kikongwe kama hiki kuwa na aina hii ya Mwenezi!!Please uwe una-engage ubongo wako wakati wa kutoa tamko lolote publicly unatia aibu aisee
 
hvi Nape huwa anatumia nini kufikiri yan mwil mkubwa ana choongea pointless asipo taja Chadema hasikii raha sasa we Nape mwanasiasa gani kila siku Chadema isingekuwepo je? halafu mulivo zoea kuwadaganya wananch enzi za zidumu fikra za mwenyekiti badilika na siasa zako
 
maCCM yanajitekenya halafu yanacheka yenyewe...Nape, kama UKAWA wanapotea, ningetaraji iwe furaha kwako, lakini ptuuuu.

UKAWA wamewashika pabaya, hamtoki kirahisi pamoja na wingi wenu. Pale bungeni penyewe sasa hivi hamjadili katiba ila UKAWA.

Kama Nape, Mwigulu na Le Mutuz ndio think tank za CCM basi hili lichama bora life
 

swali kwamba hivi mwananchi ni nani hasa! hata Mimi nimeliuliza mara nyingi lakini bado kuna tatizo!
 

mkuu sijui kama unajielewa, wiki iliyopita uliwashauri kwa kuanzisha mada kuwa wasirudi tena bungeni, leo unaleta umaskini wa UKAWA kesho utasema utajiri wa UKAWA, sijui unatufurahisha wananchi wako au una lengo gani hasa...kiongozi wangu, kinachotafutwa na sisi walalahoi ni katiba bora sio katiba mpya tu. Uccm na uchadema wenu pelekeni kwenye jukwaa la Jokes, uku njoo na mada za kiutu uzima kiongozi wangu, Nakutakia ujenzi mzuri wa taifa hili.
 
Nape ni adui yangu wa kisiasa ujue hivyo tu!


Sent from my iPad using JamiiForums app

Ukitizama tofauti za kimitizamo na kimawazo kama uadui, Mara nyingi utaishi kwa frustration na nirahisi kupata nguvu inayokusukuma kutoka ndani,kufanya siasa za tindikali.
 
Mbona nyie ni wagumu kuelewa? ina maana kwa elimu ndogo nyie Nape Nnauye na @W.J.Malecela hamjui kuwa kuna sheria inayosema ili kifungu chohote kipitishwe ni lazima kuwepo theruthi mbili kwa pande zote (tanganyika na Zanzibar) ?

Hamjui kuwa CCM pekee kwa upande wa Zanzibar hawawezi kufikisha hiyo theruthi mbili?. Jenga hoja kwamba kwa maslahi ya kupatikana katiba UKAWA wanaombwa kurudi siyo kutoa hoja dhaifu kama hizi.nyie mtakua lini lakini?
 
Last edited by a moderator:

...Mkuu miongoni mwa masomo aliyopata F form IV ni English na Civics. Kiswahili alipata D kwa hiyo msaidie kijana mwenzio kutafsiri lugha yako ili iwe katika lugha "aliyofaulu"
 
Bahati mbaya sana huwa huwezi kutetea hoja zako majukwaani. Ukianzisha topic huwezi kuhimili hoja zinazoshushwa dhidi ya viroja vyako. Nape you sound toooo and extremely low kila linapofika suala la kujenga hoja...maana hata kuandika unapata taabu...hata kuandika unajifunza bado?

Ok. Suala la kwanza unawafahamu wajumbe wote wa UKAWA? Unawajua UKAWA walioko CCM na serikalini?

Kati ya hao uliowaona una uthibitisho gani kuwa wamewahi kuwa wajumbe wa UKAWA? Au ulimsikiliza Uluoch ukiwa unakimbilia kuandika? Ungekuwa umemsikiliza kwa makini usingekuja kuandika hiki kaka...

Leo cham chako, serikali yenu na cronies wenu mmelazimika kujadili suala la katiba mpya kwa sababu ya nani?

So longer as CCM inazidi kukosa ushawishi kwa kugombana na watu hao hao eti inaotaka kuwaongoza, upinzani nchi hii unazidi kupata nguvu na kuwa imara kuliko jana na juzi. Unalifahamu hilo kwa uzuri.

Kama mnafikiri mnaweza kuandika katiba inayotokana na misingi ya sera ya chama chenu badala ya maoni ya wananchi, si muendelee kisha mwende kwenye kura ya maoni itakayosimamiwa na mfumo huru halafu muone itakuwaje!

Why waste your time talking about dying stuff kama kweli unaamini hivyo na kwamba kifo chao litakuwa furaha yako...si ungefurahia kimoyo moyo ili zitimie ndoto zako badala ya kutumia nguvu kuzuia hicho kifo.
 
Nakumbuka nikiwa katika moja ya Mkoa katikati ya Mwaka jana, wakati wa maandalizi ya Mabaraza ya Katiba ya Kata nilikutana na wajumbe wanajadiliana kuhusu muundo wa Serikali 3 kwa mujibu wa Rasimu. Wakawa wanasema tumeambiwa serikali 2 tatu ni gharama. Nikawauliza Serikali mbili zipi hizo? Wakadai hawajui
 
ni vyema ukaandika kitu kama kiongozi wa ngazi za juu wa chama tawala, weka kitu kilichokamilika ni idadi ya wana UKAWA wangapi wamerudi leo Bungeni ili tupate kujua, sasa na wewe tutakutofautisha vipi na le mutuz? unaandika kijuu na kiushabiki zaidi? na ni vyema ukashabikia Utaifa na kuendelea kutafuta utatuzi wa makundi mengine katika upatikanaji wa katiba mpya, na ninajua unatambua kuwa bila upinzani ccm watabaki na mawazo mgando, kwa hiyo upinzani ni muhimu katika demokrasia, sasa kama wewe unafurahia kufa kwa upinzani hupendi demokrasia.
 
Mnawekeza bilion of $kuua upinzani nchini badala ya kuwekeza hizo hela kwenye matatizo yanayoizunguka jamii mnayodai kila uchweo inawapenda

Mtu mzima unapokuja na kebehi za kilukuvi unategeme wenye busara tutakuonaje?

Ccm msiwe wabishi kwa vile mnajua kubisha,jaribu kuwaelewa ukawa ili mueleweshwe

Mshukuru sana kinana kakufanya uonekane tena japo wengi wanajua ww ni mbuzi wa kafara mda wowote unachinjwa na watu wanaendelea kutajirika tu kwa nyota yako
 
- Shibuda haendi Escape 1 Beach Club kaka, wacha kurusha majina ya watu bila ukweli!!

Le Mutuz System

Ukweli gani? sikuhizi mmeshajifunza kuishi kwa ukweli ninyi? Hebu mtaje basi kama kweli mmebadilika.
 
Hivi CCM kinacho wawasha kwa kifo cha upinzani ni nini?
Mbona kama vile hawapendi?
Kama UKAWA ni kifo cha upinzani wacha iwe kuliko kuongea ongea watapeperusha njiwa.
Adui ukimjua si adui tena, so watulie wasubiri kifo.
 
Nape katika vijana watakao kuja kujuta baadaye kwa kutumika kama wakala wa usaliti na uhuni wa kila namna kwa wanananchi wa tanganyika na zanzibae ni wewe, halafu inakuhusu nini sasa si ufurahi kama chadema itasambaratika ili mshinde kilaini mwakani 2015, nakuomba usikimbie kivuli chako subiri kila jambo litakuwa wazi mwakani, hamna hata aibu kumtukana jaji warioba na jopo lake la tume ya rais ya mabadiliko ya katiba, shame on you nape na viongzozi wenzako wa ccm, lazima tupate tanganyika yetu pende msipende.
 
Hahaha! Kwani Oluoch ni chama gani cha siasa? Kuna uhusiano gani Kati ya Olouch kuingia bungeni na upinzani kufa? By the way upinzani ukifa wewe utafanya kazi gani? Kwa nini usifurahi badala ya kusikitika? It's too low for you kaka

Hatuutaki upinzani Bungeni... Tunayoitaka ni Katiba bora.. Mm siamini kama upinzani ndio unaoleta katiba bora hata kidogo
 

Ccj yako ivi bado unaisapoti?
 

Kina Nape,
Wanadhania ushindi wa 2/3 upande wa "bara" kura ya maoni, hivyo kufanya bao 1-0 ndio ushindi wa msimao wao. Wanadhania kura ya maoni itaangalia wingi wa kura (grand total) kama uchaguzi wa rais wa Muungano. Hawajui kwamba ushindi kamili utahitaji pia washinde 1-0 upande wa zanzibar yani 2/3 pia kuungwa mkono upande ule. Hilo halitatokea, upande wa zanzibar mtapigwa 1-0 serikali tatu hivyo matokeo kuwa 1-1. Na hawajui madhara ya matokeo haya ni nini kwa CCM na muungano kwa ujumla. Mbaya zaidi, hawajui matokeo yatakuwa haya haya hata kama:

1. Polisi watafanikiwa kuzuia mikutano yote ya UKAWA mpaka siku ya kura ya maoni.

2. Hata kama chadema itakufa kesho na kupotea kabisa katika siasa za Tanzania.

Hoja ya Tanganyika ilianzia humo humo CCM, tena ikiletwa na makamu mwenyekiti wa CCM Taifa (Aboud Jumbe) 1983. Hapakuwa na chadema wala ukawa. Na nchi ilikuwa chini ya chama kimoja (CCM).

Hoja ya Tanganyika ikaendelea na tume mbalimbali zilizoteuliwa na marais. Hapakuwa na chadema wala ukawa.

G55 - kundi la wabunge, wote walikuwa ni CCM. Na hapakuwa na ukawa wala vyama vingine vya siasa nchini. Rais wa Jamhuri ambae pia ni Mwenyekiti wa CCM wakati ule (Mwinyi), makamu mwenyekiti na waziri mkuu na makamu wa kwanza wa rais (Malecela), katibu mkuu ccm taifa (Kolimba), wote waliridhia serikali tatu. Malecela kama kiongozi wa serikali bungeni, bunge 100 pct CCM, akafanikisha hoja ya Tanganyika ipite. Waziri wa Sheria na Katiba wakati ule (Samuel sitta), akaanza mchakato wa kura ya maoni kabla ya Nyerere kuingilia.

Mwalimu angekuwa hai leo, asingeizuia Tanganyika kwani aliamini katika ccm imara, ccm yenye ushawishi mkubwa, ccm inayolinda katiba ya nchi. Leo znz wamevunja katiba ya nchi, leo ccm sio imara tena na wala haina ushawishi mkubwa tena, kwani upinzani umeshamiri. Chini ya mazingira haya, katiba ya nchi haiwezi tena kuwa ni sera ya chama cha siasa.

Mwalimu aliwahi sema kwamba "yapo ya maana na yapo ya kijinga aliyofanya katika uongozi wake". Hakika, hili la serikali mbili lilikuwa ni la kijinga (kwa kuazima maneno yake). Na akaenda mbali na kusema kwamba anashangaa viongozi waliomfuata, badala ya kuachana na ya kijinga na kuendeleza ya maana, wao wanaacha ya maana na kuendeleza ya kijinga.
Nape Nnauye, acheni kuendeleza yale ya kijinga kama serikali mbili nyakati hizi. Endelezeni ya maana - boresheni azimio la arusha liendane na mahitaji ya leo, sio kuboresha serikali mbili. Hilo ni la kijinga kabisa.

Kwa maelezo haya, nadhani ni dhahiri kwa nape kwamba kwa kushambulia UKAWA, Chadema, "he's barking at the wrong tree".

Tanzania Kwanza, Tanganyika Kabla.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…