GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Pombe na sigara ni kati ya bidhaa zinazoingizia nchi hela nyingi kwa njia ya kodi. Ingawa ni bidhaa iileteayo Serikali ukwasi mkubwa, ina madharabhasi kwa baadhi ya watu hasa masikini.
Ilishawahi kutokea, na hata sasa hali inaweza ikawa hivyo kwa baadhi ya maeneo, ambapo:
1. Mwanaume anaenda kufurahia bia baa wakati watoto wake wana utapiamlo
2. Wengine hushindwa kufanyq kazi kwa sababu ya ulevi
3. Maeneo mengine unaweza ukamkuta mtu kalala njiani kwa sababu ya ulevi. Kwamba, pengine alikuwa na hela ya kulewea tu lakini ya usafiri wa kumfikisha kwake hakuwa nayo
4. Masikini anapokuwa mlevi ni familia yake ndiyo inayoteseka
5. Wengine wakishakuwa waraibu wa pombe huwa radhi kutokula ili hela ya chakula aitumie kwa pombe
Labda inaweza ikawa msaada endapo utaratibu utawekwa kuwa watu wa kipato fulani pekee ndiyo watakaoruhusiwa kunywa pombe? Itasaidia? Huo utaratibu unaweza kuwahamisha masikini kufanya kazi kwa bidii ili hatimaye na wao wapewe leseni ya kunywa pombe?