mabuba
Senior Member
- Dec 5, 2006
- 133
- 90
Yanga kwa historia haiwezi fananishwa na timu nyibgine yoyote katika ukanda wa Afrika Mashariki. Ni timu ambayo historia yake inaonesha ni sehemu ya uhuru wananchi yetu. Licha ya kuwa Yanga ina historia ndefu bado katika medani ya soka haijafanya vyema kama umri wake ulivyo.
Hivi karibu Mwenyekiti wetu Yanga (Manji) ameibuka na dhana tata katika medani ya soka, dhana hii ameipa jina “kukodisha timu”. Dhana hii ni mpya katika medani ya soka, kwani katika kuperuzi kwangu sijakutana na dhana hii. Maji kwa kutumia madaraka yake amekuwa akiendesha Timu kwa jinsi atakavyo yeye. Tukumbuka kuwa Manji amekuwa akitumia pesa zake kuendesha Yanga, hili halina ubishi. Lakini pesa hizo hizo anataka wanayanga wamuone kwamba bila yeye hakuna Yanga. Hivyo yeye kwa Yanga sio kiongozi tu, bali ni mfadhili na sio mdhamini.
Kumbe ufadhili wake, nao sio ufadhili bali ni “mkopo kwa Yanga” Manji amekuwa akiikopesha Yanga na sio kuifadhili, hili lazima wanayanga lazima wajue. Mkopo sasa umefikia Bilioni 11, ambao amekuwa yeye mwenyewe akijiidhinishia kukopa na kutumia atakavyo. Siwezi kushangaa siku wanayanga tukiambiwa kuwa hata mechi ya TP Mazembe tuliyoingia bure na Manji akalipa, ni sehemu ya mkopo.
Hili la kukodisha timu nalo linazua maswali mengi, makala inayosambaa katika mitandao ya jamii na magazeti ya kuonesha makubalino ya kampuni Yanga yetu na Young African Sports Club inatia maswali mengi pasi majibu. Kwa ufupi naweza sema hili ni change la macho.
Yanga kupewa ekari zaidi ya 700 huko Kigamboni, ni kiini macho kingine ambacho wanaYanga lazima wajue. Msajiri wa hazina aliwataka watu wote waliobinafisishiwa Viwanda, Mashamba, nk kutoa taarifa juu ya uendelezwaji wa Mashamba. Tukumbuke Manji alichukua eneo hilo kutoka kwa NAFCO. Lakini pia kampeni ya Mh. Lukuvi juu ya maeneo yasiyoendelezwa, isijekuwa haya yote yako mlangoni mwa Mh. Manji. Hivyo sitaki niamini kuwa ameona ahamishe agenda isiwe ya Manji na Serikali bali iwe Yanga na Serikali. Lakini pia kuwa lazima tukubali, nani anajua Yanga sasa inaendeshwaje? Naota ndoto mchana kuwa eneo hilo ni sawa na mtu kutoa pesa mfuko upande wa kulia na kuhamishia kushoto.
Kuna athari kubwa sana ya Manji kuendelea kuifadhili Yanga kwa mfumo huu, na athari hiyo ni ya muda mrefu. Lakini pia kuna athari kubwa ya kwa Manji kuachia timu ya Yanga leo, lakini athari hii ni ya muda mfupi. Ni wakati sasa kwa wana Yanga kufikiri kwa kina juu ya hiki kinachoitwa mfadhili mwenyekiti
Manji kama anataka kuendesha Yanga “adhamini na sio afadhili” lakini pia aweza kutumia mfumo wa hisa na sio wa kukodi timu. Pia lazima kwamba akubali kuondoka katika uongozi ndipo mchakato huo uanze na sio sasa yeye mwenyekiti nay eye ndiye anataka Yanga hapa, hawezi kukwepa mgongano wa masilahi
Mabuba FKM
Mwanamtaa