Ndugu, hivi niulize, kuna mtu ana haki miliki ya kipaji cha mtu mwenyewe...?? Ndio kwenye jina wanaweza wakawa wana haki miliki. Ninavyojua na kwa jinsi wanasheria wengine (walio wataalamu wa sheria za haki miliki) manake wengine huwa wanakurupuka hali hawajui haki miliki, mtu huwezi kuwa na haki miliki kwenye talent ya mtu bila idhini yake tena ya kimaandishi..!! Yaani in other words, Asha baraka hana haki miliki na style maarufu ya Ally Choki, ndio maana hata alipokuwa anahama, hakuweza kumpiga stop kuitumia. Ukiongelea kipaji, the first beneficiary wa haki miliki (pale panapokuwa hapana makubaliano yaliyo halali na siyo ya kusurutishwa; kwa lugha ya kisheria pasipo na undue influence) huwa ni mtu mwenyewe. Sasa sielewi huyu jamaa wa COSOTA anakurupuka vipi, hali yeye mwenyewe akishirikiana na BASATA waliwahi kumtetea Mengi, Mhavile na Rita Paulsen pale walipowaibia haki miliki vijana wanyonge hali hawa madogo walikuwa na maandishi ya kuwa wamiliki halali wa copyright ya Bongo Star Search (kesi bado iko mahakamani). Wafuatiliaji wa maswala ya sheria mtakuwa mmeisikia. Hayo tuyaache, tu-concentrate kwenye Ze Comedy.
Kwa hiyo, hawa madogo wasinyanyaswe hata kidogo, na ninaomba wataalamu wa sheria za haki miliki wasimame na kuongea facts. Tuachane na hawa wanasheria waliopewa cha juu na kuanza kuwakandamiza vijana wa watu. Pia tukumbuke kuwa hawa vijana hivi sasa wanafadhiliwa na Manji, na kwa wafuatiliaji wa maswala ya kijamii, mtakumbuka ugomvi kati ya Mengi na Manji ulivyoleta gumzo hapa TZ kiasi cha kuburuzana. Kwa hiyo hii ni ishara tosha ya namna ambavyo Bwana Mengi na familia yake pamoja na washirika wake walivyoamua kuwaharibia vijana hawa bila kujua wakidhani wanamharibia Manji ambaye nahisi keshashiba utajiri. Ushauri wangu kwa Mengi na washirika wake ni kuwa, wasilete ugomvi wao na Manji katika maeneo yatakayoumiza wanyonge. Kama wanataka kupambana wakapambane kule BOT au Kempinski ambako ni kwa mapede wenzao. Au if possible wakapambane huku wakiwaumiza matajiri wengine kama kina Mkono, Bakhresa au Rostam kabisa.
Huu ni ukoloni mamboleo ndani ya nchi yetu wenyewe. EATV ningewashauri wakatae mambo mengine lakini sio matumizi ya talents za vijana wa watu ambao waliamua kujituma badala ya kujiingiza katika u-kibaka na matumizi ya madawa ya kulevya. Tumeona vipindi kibao vya TV vinarushwa leo kwenye SABC kesho kwenye channel nyingine kwa mwendo ule ule.