Maskini kina Masanja na wenziwe, hawa hawakujua sheria! walidhani umaarufu wao utabaki pale pale. Lakini hata kwa watu wanaofurahisha kama walivyokuwa wao mambo mara nyingine hubadirika. Si unakumbuka wale wakina Bishanga enzi zao? walibeba umaarufu sana wale. Lakini leo wako wapi?
Kila mahali unapokuwa katika kazi panakupa umaarufu wa aina fulani na nakwambia unaweza kutoka kwa kudhani umaarufu ule ule uliokuwa nao, utakuwa nao kumbe ndio kabisa kila kitu kikaisha.
Kama walivyodokeza wengi, nina mashaka kama hawa vijana wapya wa Manji ambao kisheria hatutakiwi kuwaita tena ze comedy wataendelea kufanya vitu vyao kwa uhuru ule ule waliokuwa nao. Maana nakumbuka hata Mengi alilalamikiwa na hawa mafisadi kwamba awazuie vijana hawa kufanya waliyokuwa wanafanya na akakataa. Sasa leo wako katika mikono yake si hapo ndio wamekwisha?
Mi nakwambia hakuna atakayeendelea kuangali upuuzi kama hawataendelea ku mantain trend ile ile waliyokuwa nayo walipokuwa EATV. Kama watabadilika kidogo na kudhani watu watafurahia kila kitu, wajue wamejimaliza wenyewe.
Tunataka kama wataendelea na ujasiri huo huo wamuigize huyo Manji kama fisadi namba mojana huyo Tido wao kama kibaraka wa JK na hapo tutawaaminia!