pole mkuu. Nashangaa kina mzizi mkavu hawajaibuka kutoa maelezo ya kukusaidia
HABARI ndugu zangu mimi ninamatatizo ya kusikia ngoma zimepasuka nimehangaika sana kutafuta tiba lakini wapi.ninamshukuru mungu wakati nimeanza kuugua nilikuwa kidogo ninapesa hivyo nilizunguka sana katika hospitali zote kubwa na ndogo,sikuwa na shida na pesa ila shida yangu ilikuwakupona masikio lakini hamna kitu mpaka nikaamua kununua mashine ya masikio. sasa je ninaweza nikaja nikasikia tena ?au ndo SIKIO LA KUFA HALISIKII DAWA? nipeni data wazee.
Awali ya yote pole sana kwa matatizo. Ningependa kufahamu sababu zilizopelekea masiko yako kutoboka. Je umewahi kuwaona wataalam wakathibitisha kuwa ngoma zimetoboka? [ Eardrum perforation].Pili unapotumia mashine unazosema, je hali inakuwaje katika usikivu.
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha ngoma kupasuka ikiwa ni pamoja na Ear infection au Physical damage inayoweza kupasua ngoma, hii ni pamoja na kuingiza vitu ndani ya sikio, au ajali n.k.
Lakini pia inaweza kuwa kulikuwa na sababu za kimaumbile [in born] ambazo hazikuwa bayana kwa nyakati fulani na kadri siku zinavyosonga ndipo dalili zinavyojiopnyesha.
Kwa vile unatumia mashine na kupata usikivu, na kwa vile bado unasikia kwa msaada huo, si rahisi kujua kiwango cha uharibifu wa ngoma. Kwa mantiki hiyo ni kwa vipimo vya kitaalam ndivyo vinaweza thibitisha hatima ya sikio lako. Ningekushauri ukaonane na Daktari bingwa wa maradhi ya masikio, pua na koo [ENT SPECIALIST], Huyu atatoa msaada wa hatima ya masikio yako.
Usikate tamaa bado kuna nafasi ya marekebisho, lakini kumbuka kumuona ENT Specialist kwa msaada zaidi.
Pole sana Mungu Yupo utapata ufumbuzi. tunakuombea.
pole mkuu ni chalange za maisha... ingawa mimi c mtaalam wa mambo hayo ila naamini iko siku utakuja sikia... pengine kuna ukungu tu au (mwangi) ndani ya sikio lako
nashukuru bro.kwani mzizi mkavu anakujaga na huku?maana huwa namuona sana kwenye jukwaa la sayansi na teknojia. Naomba utengeze link ili aje humu nae amwage mautaalam.
Jamani pole sana, unahitaji vifaa maalumu vya kusikilizia,
je kule ulikopata tatizo hili hukuwa na medical insurance ? Ok kama hakuna
Ungeweza ku claim permanent disability na kulipwa kiasi fulani cha hela ambacho kingekuwezesha kumiliki mashine, unajaza workmen's compensation injury form na kama injury uliipatia kazini, kwa sheria mpya ya kazi unastahili kulipwa unless kama ulikuwa umejiajiri, bado hujachelewa.
pole mkuu ni chalange za maisha... ingawa mimi c mtaalam wa mambo hayo ila naamini iko siku utakuja sikia... pengine kuna ukungu tu au (mwangi) ndani ya sikio lako
Mkuu kwanza pole. Ila sasa umesema source yaweza kuwa kelele,lakini ulipochoma quinine ndo yakazidi. Kama source imekuwa accelerated na quinine,utapona japo baada ya muda mrefu. Otherwise sina utalaam wa kukupa zaidi ya kukushauri ukae sehemu tulivu mda mrefu. Kama ni quinine utapona na nadhani kama ni tatizo la kupasuka kabisa hapo pagumu! Ila eardrum ikipasuka huwezi sikia 20%. Hapa ni tatizo linaloweza kutibika ,meanwhile ntamtafuta mtu anaemjua mtaalam yuko bunju dsm ni bingwa wa ajabu!ngoja nimsake alaf ntakupa jawabu. Ukiona kimya naomba uniPM ili nikumbuke mkuu. Wish u fast recovery!