Awali ya yote pole sana kwa matatizo. Ningependa kufahamu sababu zilizopelekea masiko yako kutoboka. Je umewahi kuwaona wataalam wakathibitisha kuwa ngoma zimetoboka? [ Eardrum perforation].Pili unapotumia mashine unazosema, je hali inakuwaje katika usikivu.
Kuna sababu kadhaa zinazoweza kusababisha ngoma kupasuka ikiwa ni pamoja na Ear infection au Physical damage inayoweza kupasua ngoma, hii ni pamoja na kuingiza vitu ndani ya sikio, au ajali n.k.
Lakini pia inaweza kuwa kulikuwa na sababu za kimaumbile [in born] ambazo hazikuwa bayana kwa nyakati fulani na kadri siku zinavyosonga ndipo dalili zinavyojiopnyesha.
Kwa vile unatumia mashine na kupata usikivu, na kwa vile bado unasikia kwa msaada huo, si rahisi kujua kiwango cha uharibifu wa ngoma. Kwa mantiki hiyo ni kwa vipimo vya kitaalam ndivyo vinaweza thibitisha hatima ya sikio lako. Ningekushauri ukaonane na Daktari bingwa wa maradhi ya masikio, pua na koo [ENT SPECIALIST], Huyu atatoa msaada wa hatima ya masikio yako.
Usikate tamaa bado kuna nafasi ya marekebisho, lakini kumbuka kumuona ENT Specialist kwa msaada zaidi.