Masikitiko - Timu ya Taifa yawa timu ya Mkoa wa Dar es salaam

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Sitaki kuamini kwamba wachezaji wazuri nchi hii wamo kwenye timu zile 3 tu za mkoa wa DSM , hii itakuwa ni kashfa kubwa sana na ni kutowatendea haki wachezaji wengine waliojazana kila pembe ya nchi .

Sijaridhishwa na uteuzi wa timu yetu ya Taifa , ni wa kibaguzi na umejaa ubabaishaji mtupu.

Nakulilia Maximo .
 
tatizo tff wameendekeza usimba/yanga , pia uwekezaji wetu ksyika soka la vijans ni wa ovyo. Tanzania hakuna menejiment nzuri katika soka la bongo
Tusitarajie matokeo kwa ubabsishaji wa viongozi, upangaji matokeo, ufisadi wa viongozi wa soka, pamoja na kuleta siasa za uccm kwenye soka.
 
Hukumbuki mwaka fulani iliundwa timu ya taifa B nadhani ilikuwa inaitwa KAKAKUONA ikafika nusu fainali kama sio fainali challenge.....mwenye kumbukumbu anirekebishe tafadhali
 
Tumia akili basi kidogo, wachezaji wazuri wote Tanzania wanachukuliwa na timu hizi tatu, yaani ukiwika tu kidogo kwenye team ya kolomije fc unajikuta upo yanga, simba na Azam. Pili hizi timu zina wachezaji ambao wanauzoefu angalau na international matches, ningeliona bandiko lako la maana kama ungesema badala ya kumweka hajibu wa simba angemweka Alberto baskite wa Call me J fc, ila kama na wewe haujawajua wachezaji wazuri nje ya simba, yanga na azam. Basi hawajafikiu uzuri unaouongelea
 
Hukumbuki mwaka fulani iliundwa timu ya taifa B nadhani ilikuwa inaitwa KAKAKUONA ikafika nusu fainali kama sio fainali challenge.....mwenye kumbukumbu anirekebishe tafadhali
Nadhani ilikuwa ile miaka kati ya 1994 na 1995
Timu ilikuwa na wachezaji wazuri akina Gasper Lupindo na sekilojo chambua kama sikoei
 
Nadhani ilikuwa ile miaka kati ya 1994 na 1995
Timu ilikuwa na wachezaji wazuri akina Gasper Lipindo na sekilojo chambua kama sikoei
Na games zao zilipigwa Sheikh Amri Abeid I thought
 
Kwani kama timu inashinda kuna shida gani hata kama wachezaji wote wanatoka kolo mije? Mbona watanzania mnalalama ovyo ovyo? Yaani mmekuwa kama wale viumbe ambao mpaka leo haifahamiki wanataka nini! Au nyie mmekuwa kama wale wa Libya?
 
Tumia akili kufikiri, hizo timu tatu ndo timu bora hapa nchini! Wachezaji wazuri wote hugombewa na hizi timu tatu. Pia ndo timu pekee zenye mipango endelezi za kisoka. By the way, hizo ndo timu zenye mchanganyiko mzuri wa Wachezaji kutoka kila pembe ya nchi. Ukienda majimaji utakuta asimilia 90 ya Wachezaji ni watu wa kusini.

Kocha anaangalia viwango tu, ishu za geographical distribution pelekea watu wa sensa
 
Sitaki kuamini kwamba wachezaji wazuri nchi hii wamo kwenye timu zile 3 tu za mkoa wa DSM , hii itakuwa ni kashfa kubwa sana na ni kutowatendea haki wachezaji wengine waliojazana kila pembe ya nchi .

Sijaridhishwa na uteuzi wa timu yetu ya Taifa , ni wa kibaguzi na umejaa ubabaishaji mtupu.

Nakulilia Maximo .

Mbona hata Timu ya Taifa ya Uingereza Wachezaji wake 85% wanatokea katika Jiji Kuu la London na bado Timu yao inafanya tu vizuri? Muhimu tuwe na Timu nzuri au tuwe na Wachezaji wa kutoka Mikoa yote ya Tanzania kama utakavyo? Halafu naomba nikuulize hivi kwani kuna Sheria au Kanuni yoyote ile inayomtaka Kocha wa Taifa Stars ateue Wachezaji kutoka Klabu zote zilizopo katika Ligi mbalimbali hapa Tanzania?
 
nimefurahi nape alipoingia tu, watu wakamshangilia wanataka kumpa mkono. anapendwa na watu. yule mwingine hakujulikana kama yupo uwanjani hadi nape alipoenda kukaa naye...najua atakuwa amejisikia vibaya sana.
 
Hizo ndiyo timu bora, sasa zile ambazo ni matawi yake zitapata wapi wachezaji bora zaidi ya kuzichangia timu kubwa.
 
Sitaki kuamini kwamba wachezaji wazuri nchi hii wamo kwenye timu zile 3 tu za mkoa wa DSM , hii itakuwa ni kashfa kubwa sana na ni kutowatendea haki wachezaji wengine waliojazana kila pembe ya nchi .

Sijaridhishwa na uteuzi wa timu yetu ya Taifa , ni wa kibaguzi na umejaa ubabaishaji mtupu.

Nakulilia Maximo .
Bila shaka wewe msukuma.. maana mshazoea kubebwa kwenye vyeo na mtukufu sasa mnataka kutupanda kichwani hadi kwenye soka... Tulia ngosha
 
Mbona hata Timu ya Taifa ya Uingereza Wachezaji wake 85% wanatokea katika Jiji Kuu la London na bado Timu yao inafanya tu vizuri? Muhimu tuwe na Timu nzuri au tuwe na Wachezaji wa kutoka Mikoa yote ya Tanzania kama utakavyo? Halafu naomba nikuulize hivi kwani kuna Sheria au Kanuni yoyote ile inayomtaka Kocha wa Taifa Stars ateue Wachezaji kutoka Klabu zote zilizopo katika Ligi mbalimbali hapa Tanzania?
Swali lako sitajibu , ila andiko lako limenipa mzuka wa kufikiria kugombea uongozi TFF
 
Bila shaka wewe msukuma.. maana mshazoea kubebwa kwenye vyeo na mtukufu sasa mnataka kutupanda kichwani hadi kwenye soka... Tulia ngosha
Niombe radhi mkuu .
 
Back
Top Bottom