Maskini aliyeridhika hujimbeleleza kwa misemo inayomkandamiza zaidi

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
Umaskini haufai, na kama ukiwa maskini ukaishi kwa misemo kama hii, ni ishara kuwa umeamua kuukubali, na kwa hakika utateseka.

Hakuna cha kusema “maisha ndiyo haya haya tu” - kuna mazuri zaidi ya hayo. Acha kujifariji kwa misemo kandamizi kama ifuatayo:

1. Maisha si vita.
2. Maisha ndiyo haya haya tu.
3. Pesa hainunui furaha.
4. Utajiri ni dhambi.
5. Kila tajiri ana ushirikina.
6. Pesa si kila kitu.
7. Mapenzi ni upendo, pesa ni ziada tu.
8. Utajiri unatesa sana, bora hata usiwe na pesa.
9. Hata matajiri watakufa.
10. Mbinguni hakuna cha tajiri wala maskini.

Badala ya kutumia misemo hii kama kisingizio, tafuta njia za kuboresha maisha yako na kuachana na mawazo ya kujidhalilisha.
 
Zinaitwa excuse, hutumika sana ili ku justify failure
 
Uwe una hela au huna.hayo.maneno ni ya .ukweli..hakuna uongo apo labda ujizime data tu
 
Maisha ni haya haya mkuu, hakuna maana ya kumtoa uhai mwenzako ili wewe upate pesa, cheo au umaarufu kwa sababu mwisho wa siku utagundua vyote havina msaada yaani ubatili.

Maisha ni haya haya, ukipata tunza, ukikosa tumia ulichotunza
 
🙏
 
Sawa sawa tajiri
 
Wanatutake ili wapate hela. Maskini ya Mungu watatumaliza bure hawa matajiri
 
Kama huamini pesa sio kila kitu , zipate tufanane utajua kwa kweli kuna mambo pesa haina msaada
 
Kama huamini pesa sio kila kitu , zipate tufanane utajua kwa kweli kuna mambo pesa haina msaada
Ukisikia kuna mtu anasema Pesa ni Kila kitu ujue huyo ni Maskini. Hajawahi kushika pesa anatamani ashike pesa na anadhani pesa itamaliza shida zote alizonazo.
 
Ukiwa maskini huwa unawaza kama hivi.

Unadhani huenda ukiwa na pesa badi shida zote zinaisha😅😅😅😅
 
Umesahau freemason. Lakin wakiishiwa wanakuja kuomba msaada wa hela kutoka freemason
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…