Maskini anaanzia umri gani?

Sa 7 mchana

JF-Expert Member
Joined
Dec 30, 2018
Posts
5,214
Reaction score
10,276
Naomba kuuliza umaskini unaanzia umri gani? Yani mtu ukifikisha umri gani na akawa bado hajiwezi katika mahitaji yake muhimu anaqualify kuitwa maskini.

Ikiwa na maana gani mtoto wa miaka 9 anaeishi kwao hatuwezi kumuita maskini ila kwakua Mpwayungu Village mwenye miaka 46 anaeshi kwa shemeji yake pale Isunga chupi tunamuita maskini ( natania πŸ˜‚πŸ€£) .

Swali ni je maskini anaanzia umri gani? Kama ni 18 kama Mtu mzima tujue....

Bado nachukua darasa la uandishi
 
Umasikini huanzia miaka 5 tu baada ya kuandikishwa shule, wenzako wanapewa pesa wewe unaishia kuomba, uniform 1, viatu pea moja, mfuko sport wa madaftari badala ya Begi unajuwa tayari vita imeshaanza.

Maana umaskini huanzia kwa wazazi wako.

Case closed
 
Umaskini ni hali, yeyote anaweza kua na hiyo hali.

Hata mtoto mdogo ambaye wazazi wake hawawezi kumpatia mahitaji muhimu kwa wakati ni maskini.

Ndo ninavyoona mimi.
 
Umaskini Unaanzia Baada ya wewe kuwa na majukumu na kushindwa kuyatimiza. Kama kushindwa kusaidia Mtoto wako, Mke wako, Wazazi wako na wakiwa wanakutegemea , basi ww ni maskini.
 
Ukitobowa maisha ndio umaskini unapokoma.

Ndio sababu matajili wengi hawataki masihara kwenye pesa, wanaogopa usiwarudishe kwenye laana ya umaskini.
 
Unaweza kuzaliwa ukiwa maskini...maana umaskini unajumuisha vitu vingi mali,afya,akili,hali
 
Hadi mifugo inayoishi kwa mtu asiye jiweza nayo ni masikini.

Hadi mashamba utasikia mashamba ya yule masikini
 
Umri wa adriz na Mpwayungu Village
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…