Tena unatengewa baada tu ya kuzaliwa! Hiyo ni haki yako!Binamu nyama ya hamu haina shida kwa sisi wa pwani unaoa kabisa tena kwa shangwe na kigelegele
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Tena unatengewa baada tu ya kuzaliwa! Hiyo ni haki yako!Binamu nyama ya hamu haina shida kwa sisi wa pwani unaoa kabisa tena kwa shangwe na kigelegele
Tupo msibani! Kijana kafiwa na baba yake. Katikati ya maombolezo anafika binti mmoja hivi mtanashati ingawa tumbo kubwa lakini huachi kuona uzuri wake, anajiunga upande wa wamama asalimiana wanaendelea na maongezi. Pamoja na majozi alokuwa nayo kijana anapata faraja ya haja. Mara akawa kama amechangamka hivi. Tunamuuliza kulikoni kijana?
Anasema da angalao mchumba wangu kaja maana nilikuwa nasikitika kumwacha mwenyewe mbali. Anha kumbe! Mjomba yupo hapa na unajua tena huku uchagani hawakopeshi.
We Lelo unasemaje! Nyie watoto wa siku hizi mafirauni sana! Yaani unathubutu kulala na mtoto wa shangazi yako unakuja hapa unatwambia mchumba wako! Jamaa jasho likaanza kumtoka! Da kumbe kijana keshamvimbisha binti wa wenyewe na sasa ni mtoto wa shangazi!
Ilikuwaje: Familia ya kijana wa kiume ilikuwa ikiishi nje ya Tanzania kwa kitambo kidogo. Ni mara chache sana walikuja Tanzania ingawa wazazi wote ni watanzania. Kwa kujua kuwa huyu mzee atastaafu mapema akaanza kumtanguliza mwanaye wa kiume aje Tanzania na akapata chuo cha kufundisha pale Dodoma.
Akiwa hana hili wala lile akakutana na binti mrembo yuko idara moja na yeye. Mazoea yakajengeka! Upendo ukachanua! Wakajikuta watupu,,,,,,,,,,,hatimaye mmoja akawa amebeba kiumbe cha muunganiko wao. Tuongeapo sasa mimba ina miezi 6 na ushee.
Maskini mzee wa watu hata hakustaafu bali kaugonjwa kakapita akaona wacha aje nyumbani akasalimie. Huku akazidiwa zaidi akalazwa pale KCMC. Mvulana akaomba likizo ya dharura pale chuoni aende kumuuguza mzee. Siku chache baadae baba akaaga dunia. Akamtaarifu mchumba wake kuwa baba mkwe wake mtarajiwa kafariki. Binti naye akaona ni vyema akajumuika msibani. So ikawa pia awatembelee wazazi wake huku kijijini.
Kumbe naye msiba unamhusu kwa njia nyingine bila kujua. Mama wa huyu binti akamwambia kuwa mjomba wake kafa hivyo wakasalimie. Maskini hakujua kuwa huo ndo msiba aloujia! Wakati anaingia hakumwona Kijana hivyo alijua tu kuwa angewasliana na mchumba wake ili amwelekeze msiba uko wapi. Sasa mambo yameharibika!
Mjomba najua na binti hajajua kuwa kule ndo kwa kijana mchumba wake kipenzi. Mimba hii ni kubwa sana inaweza ikaleta madhara! Maskini hawakujua kama ni ndugu! PANDE ZOTE ZIAMBIWE AMA TUACHE MPAKA MSIBA UPITE!
Ni ushauri wako tu. Kama unahisi kuwa unataka kukashfu ni bora uasiweke bandiko iache tu ipite!
UPDATES
Wazazi wa huyu binti wameelezwa habari hizi. Wamehuzunika sana kwa kweli. Binti na kijana wameitwa na kuelezwa ukweli.
Nitawajulisha maendeleo ya hii kitu.
- Kijana amekataa kuamini amedai atatoa maoni yake baadaye.
- Binti ameondoka na ndugu zake hakuweza kusema chochote alibaki kushangaa tu.
- Hakuna hata mtu mmoja keshajua linaloendelea zaidi ya sisi ndugu wa karibu
- Wazee wameshauri hili suala lizungumzwe baada ya kuvunja tanga
- Focus now ni mazishi tu
Ewe eeka mangi mbon nyei nya dede?kwekio kijana nyalesemba nfamaaye?