Maskini huyu mtoto!!!TAMWA mpo?

Maskini huyu mtoto!!!TAMWA mpo?

kwewli tumekwiisha
hii dunia ni ya matajiri na wenye hela..

sina hata la kusema ila Mungu ndo anajua hayo yote..
atakimbia hukumu yake hapa lakini ya Mungu hawezi kimbia kabisa..
na kuna msamaria mwema atajitokeza kumsaidia huyo mama naamini kabisa..
 
Duh! jamani! hi pia inatukumbusha wazazi wenye watoto wadogo tujaribu kujua kila dakika watoto wetu wako wapi na wanafanya nini. Dunia imeharibika jamani. ila malipo ni hapahapa duniani.
 
Kuna baadhi ya nchi zina Child Protection Unit (Kitengo cha Ulinzi wa Mtoto) ambacho kimepewa meno na kinarespond kama polisi kwa maswala yote yanayohusu watoto, na inakuwa na mfumo wa kuhakikisha matibabu, huduma ya dharura na hata kuhakikisha wanahifadhiwa mahali salama na huduma ya kisaikolojia kwa watoto wanaoathirika sio kwa Ubakaji tu, bali kila aina ya udhalilishaji na udhalimu. Tanzania hatuna sababu ya kutoanzisha kitengo kama hiki kama tunahitaji kulinda taifa letu na kujihakikishia taifa bora kwani kwa sasa watu wenye umri chini ya miaka 18 ni zaidi ya 50% ya total population.

Hatua hizi ni muhimu kwa sasa:
1. Mtoto huyu na mzazi wanachohitaji kwa sasa ni huduma ya afya kwa mtoto huyu, bahati serikali hutoa huduma hii kwa mujibu wa circular, bure, namaanisha kwa umri wa mtoto kuwa chini ya miaka mitano na kwa tukio kama hili. Hata hivyo tatizo hujitokeza katika upatikanaji wa dawa ambapo ufisadi na utovu wa nidhamu huvuruga sana upatikanaji wake.

2. Mama huyu kwa sababu za kiusalama na za kisaikolojia wanapaswa kusaidiwa kuweza kuhama mbali zaidi na pale na bila wengi kufahamu atakapohamia.

3. Mama na mtoto wanahitaji sio tu huduma za afya na ya kisheria, bali kuhudhuria kliniki ya msaada wa kisaikolojia. Huduma za Kisheria zinapatikana bure kwa mashirika yaliyotajwa hapo juu kwa kundi hili maalum (hali ya mzazi kiuchumi na mtoto kiumri).

4. Mama huyu na wale wote ambao wapo tayari kuwa mashahidi wanatakiwa wawe wanajitokeza mahakamani ili kuweza kutoa ushahidi pale watakapohitajika bila kukosa ili haki itendeke.

Kwakuwa hapa wengi wetu ni anonimous, natumai mahali hapo ninapajua nitafika na kuona ni msaada gani ninaeza kuutoa wa kitaasisi, kihuduma au wa kifedha!
 
Uwiiii!!
Namuomba Mungu amponye huyo mtoto, amponye na mama yake, ampe neema ya kustahimili maumivu haya.
Ampe faraja yake ipitayo faraja zote. Ainue watu na kabila za watu kwa ajili yake na mwanae.

Mungu wa haki sikia kilio cha mama huyu na watu wanaonewa na kunyanganywa haki zao.
Pigana na adui zetu. Maana kuna watu hatuna mtetezi zaidi yako Mungu. Usinyamaze ee Mungu wa haki yetu.
 
Polisi wa tz wakiona pesa huwa wanachanganyikiwa utafikiri fisi kaona mfupa!si mnakumbuka madawa ya kulevya yaliyokamatwa tunduma polisi wakapeleka majivu kituoni!bora tujichukulie hatua wenyewe!polisi wa tz=pesa=rushwa=Wahalifu
 
Wandugu, hii habari nimeicopy sehemu, ila nimeamua kuiweka hapa kutokana na jinsi ilivyoendeshwa sivyondivyo, Je hawa watu wanjyonge kweli watapata hakiz zao kisa pesa za wenye navyo? Police wamekuwepo kunyanyasa wanjonge tu!!

INASIKITISHA MNO.!

HABARI:




MIMI NI MKAZI WA KIMARA STOP OVER GARAGE- KUNA MTOTO WA MIAKA 3 ALIBAKWA HAPA MAENEO YA KIMARA GARAGE MBELE KIDOGO YA KIMARA STOP OVER,,,KWA KWELI MKASA WENYEWE UNASIKITISHA UWEZI AMINI KAMA WATU NA AKILI ZAO WANAWEZA KUFANYA KITENDO CHA KUSIKITISHA HIVI HASA JESHI LA POLISI,,,,STORY YENYEWE ILIANZA HIVI,,,MTOTO MDOGO KWA JINA TUNAMHUIFADHI ALIRUDI KWA MAMA YAKE MCHANA KWEUPE AKILALAMIKA MAUMIVU SEHEMU ZA SIRI.

MAMA YAKE BAADA YA KUMPEKUA AKAMKUTA AKIVUJA DAMU KIBAO ILIYOCHANGANYIKA NA MBEGU ZA KIUME,,HUKU SEHEMU ZAKE ZA SIRI ZIKIWA ZIMECHANIKA KABISAAAAA,MTOTO BAADA YA KUULIZWA NANI KAKUFANYA HIVI AKASEMA FULANI (JINA TUNAMUHIFADHI)KWA KWELI MAMA ALIPIGA UKUNGA MAJIRANI WAKAJAA PALE,,BAADA YA KUAMBIWA KILICHOTOKEA WATU WAKAKIMBILIA KWA MBAKAJI NA MAWE NA MATAIRI WAMCHOME MOTO,,JAMAA TAYARI ALIKUWA KASHATOROKA SAA NYINGI.

IKABIDI WATU WAMSAIDIE MAMA KUMBEBA MTOTO NA KUMKIMBIZA KITUO CHA POLISI CHA MBEZI KWA YUSUF(MBEZI LUIS) WAKAPATA PALE PF3 YA MATIBABU NA RB YA KUMKAMATA MBAKAJI NA KESI IKAFUNGULIWA PALE,KWA KWELI ILIBIDI UFANYIKE MCHANGO KIDOGO KUMSAIDIA YULE MAMA MAANA ALIKUWA HANA MUME WALA UWEZO KAZI YAKE YEYE NI KUWACHOTEA MAJI MAJIRANI NA KUPATA VIJISENT ANAVYOJIKIMU YEYE NA MWANAWE.

MTOTO AKAPELEKWA MWANANYAMALA AKALAZWA...JIONI SASA NDO IKAWA KIMBENDE MAANA YULE MVUTA BANGI AU MBAKAJI ALIRUDI NA KUANZA KUWATUKANA WATU KWAMBA HAWAWEZI KUMFANYA LOLOTE,, ALIKUWA ANATUMIA JEURI YA KAKA YAKE ANA PESA NA HATA MKIMUWEKA NDANI ATATOKA TU (KAKA YAKE ANAFANYA KAZI TBL).NA POLISI AKIENDA ATATOKA TU ATA KWA UCHAWI.

WATU WAKAPIGA SIMU POLISI DEFENDER YA POLISI IKAJA IKAMBEBA SAA 5 USIKU AKALALA KITUO CHA POLISI MBEZI KWA YUSUF,,ALILALA LITUONI SIKU MBILI BILA HATA KUPELEKWA MAHAKAMANI,,,KATIKATI YA HIZO SIKU 2 SIJUI NDO MPELELEZI WA KESI AU POLISI HATA HATUJUI (HAWAKUWA WAMEVAA UNIFORM)KUTOKA KITUO CHA POLISI MBEZI WALIENDA HOSPITAL YA MWANANYAMALA NA KUMLAZIMISHA DAKITARI ANAYESIMAMIA VIPIMO VYA UBAKAJI AWAPE FAILI WARUDI NALO KITUONI DAKTARI AKAKATAA KATA KATA KUWAPA,,(KISHERIA HAMNA DHAMANA KWA MBAKAJI NI MAGERZA TU).

CHA AJABU SIKU YA 3 KESI IKACHAKACHULIWA NA POLISI ANAYEIPELELEZA! YULE MBAKAJI AKAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA KESI YA UKABAJI BADALA YA UBAKAJI PATAMU HAPO..CHA AJABU HATA MJUMBE WA NYUMBA KUMI KUMI NDO ALITOA KIBALI CHA DHAMANA,,HIVI KWELI HII TANZNIA TUTAFIKA KWELI KWA UNYAMA HUU,NASIKIA MAMA WA WATU KAJIFUNGIA NDANI NA MWANAWE KAZI YAKE NI KULIA TU,,,WATU WALIPOJARIBU KURUDI KITUONI PALE MBEZI ASKARI WAKASEMA ETI WALIKOSEA BADALA YA KUANDIKA MBAKAJI WAKAANDIKA MKABAJI.

WALIPORUDI KUJA KUMKAMATA YULE MBAKAJI TAYARI ALIKUWA AMETOWEKA KUSIKOJULIKANA,,KAKA WA MBAKAJI ALITOKA AKAENDA KWA MAMA WA MTOTO NA KUANZA KUMTISHAKAMA AKIFUATILIA ZAIDI HII KESI ATAMHUAMISHA MJINI,,,INASIKITISHA JAMANI HEBU MTUSAIDIE HATA KUISUKUMA HII MSG TAMWA HATA KWENYE VYOMBO VYA HABARI ILI HAWA POLISI WALIOCHUKUWA PESA WASHITAKIWE....NAOMBA MSINITAJE JINA MIMI NILIERIPOTI VITISHO VIMEKUWA VIKUBWA

ASANTENI SANA
MLALAMIKAJ

Source- Florah blog spot

Katika hili huruhusiwi kuwa na woga. Kama wewe utaogopa huyo mtoto wa miaka mitatu atafanyaje?? Na mama yake afanyaje??

Kama kuna njia yoyote ya kumpata huyo mama kwa simu tafadhali tujulishane! Tutamsaidia kwa hali na mali ili ukweli ujulikane. Please send the number if you ever get it to this email address albert@albertmsandolegal.com.

Justice will be done, on earth or in heaven!

In fear sin prospers, in bravety it is reduced to ashes...............AGM, 2011.
 
Namwonea huruma mtoto huyu kwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa. Hivi huyu jamaa alijisikia vipi?? Alikuwa na lake jambo labda kumwambukiza VVU!!!!!!!!!! Duh, Mungu atamwadhibu tuuu fataki huyu!!! na mtoto atamponya. Amen
 
Back
Top Bottom