Maskini huyu mtoto!!!TAMWA mpo?

kwewli tumekwiisha
hii dunia ni ya matajiri na wenye hela..

sina hata la kusema ila Mungu ndo anajua hayo yote..
atakimbia hukumu yake hapa lakini ya Mungu hawezi kimbia kabisa..
na kuna msamaria mwema atajitokeza kumsaidia huyo mama naamini kabisa..
 
Duh! jamani! hi pia inatukumbusha wazazi wenye watoto wadogo tujaribu kujua kila dakika watoto wetu wako wapi na wanafanya nini. Dunia imeharibika jamani. ila malipo ni hapahapa duniani.
 
Kuna baadhi ya nchi zina Child Protection Unit (Kitengo cha Ulinzi wa Mtoto) ambacho kimepewa meno na kinarespond kama polisi kwa maswala yote yanayohusu watoto, na inakuwa na mfumo wa kuhakikisha matibabu, huduma ya dharura na hata kuhakikisha wanahifadhiwa mahali salama na huduma ya kisaikolojia kwa watoto wanaoathirika sio kwa Ubakaji tu, bali kila aina ya udhalilishaji na udhalimu. Tanzania hatuna sababu ya kutoanzisha kitengo kama hiki kama tunahitaji kulinda taifa letu na kujihakikishia taifa bora kwani kwa sasa watu wenye umri chini ya miaka 18 ni zaidi ya 50% ya total population.

Hatua hizi ni muhimu kwa sasa:
1. Mtoto huyu na mzazi wanachohitaji kwa sasa ni huduma ya afya kwa mtoto huyu, bahati serikali hutoa huduma hii kwa mujibu wa circular, bure, namaanisha kwa umri wa mtoto kuwa chini ya miaka mitano na kwa tukio kama hili. Hata hivyo tatizo hujitokeza katika upatikanaji wa dawa ambapo ufisadi na utovu wa nidhamu huvuruga sana upatikanaji wake.

2. Mama huyu kwa sababu za kiusalama na za kisaikolojia wanapaswa kusaidiwa kuweza kuhama mbali zaidi na pale na bila wengi kufahamu atakapohamia.

3. Mama na mtoto wanahitaji sio tu huduma za afya na ya kisheria, bali kuhudhuria kliniki ya msaada wa kisaikolojia. Huduma za Kisheria zinapatikana bure kwa mashirika yaliyotajwa hapo juu kwa kundi hili maalum (hali ya mzazi kiuchumi na mtoto kiumri).

4. Mama huyu na wale wote ambao wapo tayari kuwa mashahidi wanatakiwa wawe wanajitokeza mahakamani ili kuweza kutoa ushahidi pale watakapohitajika bila kukosa ili haki itendeke.

Kwakuwa hapa wengi wetu ni anonimous, natumai mahali hapo ninapajua nitafika na kuona ni msaada gani ninaeza kuutoa wa kitaasisi, kihuduma au wa kifedha!
 
Uwiiii!!
Namuomba Mungu amponye huyo mtoto, amponye na mama yake, ampe neema ya kustahimili maumivu haya.
Ampe faraja yake ipitayo faraja zote. Ainue watu na kabila za watu kwa ajili yake na mwanae.

Mungu wa haki sikia kilio cha mama huyu na watu wanaonewa na kunyanganywa haki zao.
Pigana na adui zetu. Maana kuna watu hatuna mtetezi zaidi yako Mungu. Usinyamaze ee Mungu wa haki yetu.
 
Polisi wa tz wakiona pesa huwa wanachanganyikiwa utafikiri fisi kaona mfupa!si mnakumbuka madawa ya kulevya yaliyokamatwa tunduma polisi wakapeleka majivu kituoni!bora tujichukulie hatua wenyewe!polisi wa tz=pesa=rushwa=Wahalifu
 

Katika hili huruhusiwi kuwa na woga. Kama wewe utaogopa huyo mtoto wa miaka mitatu atafanyaje?? Na mama yake afanyaje??

Kama kuna njia yoyote ya kumpata huyo mama kwa simu tafadhali tujulishane! Tutamsaidia kwa hali na mali ili ukweli ujulikane. Please send the number if you ever get it to this email address albert@albertmsandolegal.com.

Justice will be done, on earth or in heaven!

In fear sin prospers, in bravety it is reduced to ashes...............AGM, 2011.
 
Namwonea huruma mtoto huyu kwa kitendo cha kinyama alichofanyiwa. Hivi huyu jamaa alijisikia vipi?? Alikuwa na lake jambo labda kumwambukiza VVU!!!!!!!!!! Duh, Mungu atamwadhibu tuuu fataki huyu!!! na mtoto atamponya. Amen
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…