Maskini mwenzenu heslb yasababisha kuua baba yangu na mama yangu

Maskini mwenzenu heslb yasababisha kuua baba yangu na mama yangu

Kwanza kabisa nawaombeni msamaha wana jamii wote wapenda amani kwa kitendo changu cha kuwaua kinadharia wazazi wangu hali wangali wazima. nililazimika kufanya hivyo ili niweze kupata mkopo asilimia mia kwani hali za wazazi wangu ni dhoofili bin taabani hivyo nilichangamka na nikasajili vifo vya wazazi wangu na kupata death certificate toka RITA ili hali wenyewe wangali hai mpaka sasa na hivi ninavyoongea niko mwaka wa pili chuo kikuu kimojawapo hapa nchini napata mkopo asilimia mia na masomo na maisha yangu pamoja na wazazi wangu yanaenda vizuri kwani nikipata boom langu huwa nakata fungu nalituma kwa wazazi wangu ingawa kwa upande wa pili nikifikiria huwa na simanzi na huzuni. wana jf naombeni ushauri kwa kile nilichokifanya nawakilisha.

kula bata wewe!! acha mawazo uongo ni uongo tu hapo ni sawa na mimi ambae hua nadanganya naumwa kumbe sitaki kwenda shule!! punguza stress kisha piga pesa bhana
 
hiyo haina tatizo kabisa,kwasababu ulifanya kwa nia njema maana wazazi hawakuwa na uwezo wa kulipa hiyo hela.cha msingi mara umalizapo masomo yako usisite kuwaeleza kisa hicho nadhani watakuelewa.
 
wewe piga kimya soma maliza lipa fadhila kwa wazazi wako,sometimes IF YOU CANT CONVIENCE CONFUSE ,MAMBO MENGINE MUNGU ANASAMEHE TU JE WAZAZI WANAPOPOKEA HIZO HELA WANAJUA UNAFAANYA KAZI??????????USIKAE UMWAMBIE MTU.
 
Tofauti yako na wale wana Apollo wapumbavu wa kule Kibosho ambao walimuua mama yao na kumkata sehemu za siri na kisha kuchemsha ili wapate Tanzanite ni ndogo. Wewe ukiambiwa tumboni mwa mama yako kuna gold ya milioni 300 utamwuua uichukue na utajitetea kwamba sisi ni maskini sana na ilikuwa ni jitihada za kujikomboa na umaskini. Kwa ufupi unatakiwa utubu hiyo dhambi ya kuua kwa maneno na maandishi na dont expect baraka out of what you're trying to do.
 
Kama wazazi wako hawako jf usitarajie hapa utapata chochote juu ya kukosa kwako amani na kuwasingizia kifo wazee wako: Ushauri wangu ni kwamba nenda kwa wazee wako na uwaombe msamaha kwa hilo, ukiweza kufanya hivyo utaona mwenyewe nafsi yako itakuwa huru sana mbele ya Mungu na hata wazazi wenyewe. Uwe makini na maamuzi unayochkua always sometimes maamuzi ya dk 5 yanaweza kukufanya ukakosa raha maisha yako yote.
 
Ulitumia akili sana. hata hivyo wako hai. kuna mijitu ina uwezo mkubwa lakini inapata asilimia mia ya mkopo mfano mke wa RIZ 1
 
kula bata wewe!! acha mawazo uongo ni uongo tu hapo ni sawa na mimi ambae hua nadanganya naumwa kumbe sitaki kwenda shule!! punguza stress kisha piga pesa bhana

Ha ha ha haaaaaaaaaa umenifurahisha hebu ngoja kwanza nikacheki bank labda boom limeshaingia nawe nikugawie kidogo.
 
Wazazi waliibiwa uhai wao, heslb waliibiwa kiinimacho, taifa liliibiwa na uenda wanafunzi wengine ambao ni mayatima kweli kweli walikosa mkopo kwani uenda kulikuwa na bajeti maalum. Vilevile uwezi kujua kuwa Mungu anampango gani juu yako ni nafasi hii kutubu na kuomba msamaha heslb na kwa wazazi wako kwani kuna kupata mkopo lakini na kudisco kupo jamani ya dunia yanapita lakini kumbuka Mungu yupo ni faida gani kupata ya dunia lakini ukakosa ufalme wa mbinguni na kuishia in the fire of hell? Soma kutoka 20:1-17 kisha ukabatizwe marko 16:16.......... "aaminiye na kubatizwa ataokoka hasiyeamini ataukumiwa"
 
Kuna uzembe unafanyika RITA hadi wanakupa vyeti vya vifo kwa watu walio hai. Kwa imani yangu lazima kwanza uwaombe msamaha wazazi wako na waridhie... kisha Mungu. Mungu atakusamehe kwa sababu ni mwingi wa huruma na ni mwenye kusamehe.
 
mi naamin ulikua unamaana kufanya hivyo kwaiyo kitu kitakachofata ni kumaliza chuo na kuwaeleza wazazi hope watakuelewa tu kama kweli walikwambia hawawezi afford chuo expensise huwa wanasema 'succes need sucrifice and things you ever do'

good advice... Smtm ther is no choise.
 
Kwanza kabisa nawaombeni msamaha wana jamii wote wapenda amani kwa kitendo changu cha kuwaua kinadharia wazazi wangu hali wangali wazima. nililazimika kufanya hivyo ili niweze kupata mkopo asilimia mia kwani hali za wazazi wangu ni dhoofili bin taabani hivyo nilichangamka na nikasajili vifo vya wazazi wangu na kupata death certificate toka RITA ili hali wenyewe wangali hai mpaka sasa na hivi ninavyoongea niko mwaka wa pili chuo kikuu kimojawapo hapa nchini napata mkopo asilimia mia na masomo na maisha yangu pamoja na wazazi wangu yanaenda vizuri kwani nikipata boom langu huwa nakata fungu nalituma kwa wazazi wangu ingawa kwa upande wa pili nikifikiria huwa na simanzi na huzuni. wana jf naombeni ushauri kwa kile nilichokifanya nawakilisha.

Tufikirie kwa mapana hili jambo. Umaskini wa hawa wazazi na famili akwa ujumla ndicho chanzo. Na mleta mada ili aweze kusaidia wazazi wake ni lazima hali kama hizi zitokee. Imagine kwa sasa allowance zake ndizo anatumia kwa mahitaji yake na wazazi. Mleta mada una akili sana na Mungu anajua hujakusudia maamuzi uliyofanya. Nchi yako ambayo inatoa mikopo bila uadilifu na kujaza hongo na watoto wa vigongo kupewa mkopo hali maskini wanaachwa ndiyo yanayosababisha haya. Ukosefu wa uadilifu wa watumishiwa wa Loan Board ambao wanakwapua hela za mikopo kwa kuwapa wanafunzi hewa ndiyo yanaleteleza haya. Na udhaifu wa utendaji wa taasisi nzima ya mikopo ndiyo msingi wa yote hayo. So now, mleta mada be happy, soma kabisa na wala huna hatia.
 
asiyetumia akili atakuponda, najua hukupenda iwe hivyo lakini yote hayo ni sababu ya umasikini na wapo wengi wanaolazimika kufanya kama wewe
 
Umekopeshwa 100%.Hivyo utakatwa zaidi kuliko waliopewa mkopo kidogo.Mimi nadhani umesolve sehemu tu ya matatizo uliyo nayo.
 
Mm nadhan ni kwenye harakati 2 za kutafuta mafanikio,wazaz wambie na uwaombe radhi kama niwaelewa hamna noma bt Mungu akusamehe bure coz ulijua ulitendalo.
 
Ishu ni pale hao wazazi wako Mungu atakapoamua kuwarejesha benchi, sijui huko Rita watapewa vyeti vya second selection au mtajitetea walitangulia mbele za haki wakafufuka
 
bora lawama kuliko fedhea la msingi ni kuwaambia tu wazazi walifahamu na imani nao wasingelipinga hilo ni la kawaida unapoitaji kitu kwa maisha yako kwani wangapi wanakula kodi zeu bwana
 
Back
Top Bottom