Ngasa kurejea Nyumbani Kesho
April 24, 2009
Mshambuliaji mahili wa Timu ya Yanga na Taifa Stars, Mrisho Ngasa, anatarajiwa kurejea Tanzania kesho jioni akitokea Uingereza ambako alifanyiwa majaribio na Timu ya West Ham united.
Habari za uhakika nilizozipata toka kwa afisa husika wa kuratibu zoezi zima la wachezaji wapya ndani ya West ham, zinabainisha hivyo, na kuwa leo joni ataagwa rasmi na jopo la makocha waliokuwa wakimuangalia pamoja na wachezaji wengine. baada ya kufanya mahojiano na afisa huyo, kwa njia ya simu muda mfupi uliopita.( 11:20 am.24.04.09.Ijumaa)
Jioni ya leo Ngasa ataelezwa hatima yake, ataambiwa " Umejitahidi sana, pia umeonyesha kiwango kizuri cha Nidhamu ya hali ya juu, tunaimani ukiendelea na ari hii, kuna kila dalili kuwa huko mbeleni utafanikiwa katika suala zima la kupata Timu bora, ataendelea kuambiwa, umeonyesha kuwa katika Tanzania kuna vipaji vingi ambavyo kwa kushirikiana na wakala wako, iko siku tukawa na mchezaji kutoka Tanzania, hivyo tunakutakia kila la kheri na safari njema".
Kwa watanzania hili ni jambo jema, ni imani yetu huko mbeleni tutatumia uwakilishi mzuri wa Ngasa.
Kutoka,
Tanzania Sports - TanzaniaSports.com