Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Ni heri ukose vyote lakini usikose akili , maskini anapumbazwa na vitu vidogo vidogo tu maana akili yake haiwezi kutazama hata umbali wa hekari 5 mbele.
Maskini anasifia wema wa mbunge kwakuwa aliwahi kusaidiwa sh. 20000 ya viatu vya shule vya mtoto wake ili akanze kidato cha 1 kwenye shule ambayo elimu hugeuka kuwa kama bahati na sio reality.
Shule ambazo mpaka mwalimu mkuu hajui matokeo ya NECTA yatakuwaje. Anasubiri tu matokeo aone kama atapata demotion au ataendelea kuwa mkuu wa shule.. Maana akifeliisha sana chaki inamngoja, ikibahatika watoto wameangaliziana vizuri akatoa vi one vitano atasifiwa kwenye mabalaza yao mpaka avimbe kichwa.
Leo hii nyama kg 1 ni kati ya sh. 11k mpaka sh15k.
Ukiplus na viungo na mchele maana yake lazima sh. Elfu 20 iende. Huyu maskini muuza bamia , nyanya na maskini kibarua wa Muhindi malipo sh. 200000 kwa mwezi (7000 kwa siku) huku nauli na chakula juu yake hawezi hata kuisogelea nyama.
Kuna maskini wawiili juzi walijifanya kujiongeza wakachanga sh. 5000 kila mmoja ili wapate elfu 10 wanunue kichwa cha ng'ombe Vingunguti. Walijisifu sana kuwa wana akili wamepata nyama nyingi na kudharau wanaonunua nyama kg. 12000.
Maskini wamepewa pesa kati ya sh. 2000 mpaka sh. 5000 ili wamchague mgombea wa chama pendwa. Ubaya zaidi hiyo rushwa ilianza kwenye uchaguzi wa ndani. Wanashindwa kujua kuwa huyu mwenyekiti kwanini anakubali kutoa rushwa huku uenyekiti wenyewe posho ni sh. 50000 tu. Je, pesa zao za maendeleo zitabaki salama mikononi mwa mtu aliyeingia kwa rushwa?
Tunakoelekea maskini atashindwa kumudu hata dagaa kauzu.