Maslahi: samatta kulipwa 40 kwa mwezi, wenzake wakivuta wastani 200 kwa wiki

Singida ndio home

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
3,188
Reaction score
3,370
mpira sio burudani tu, ni ajira yenye maslahi kiuchumi.


Kijana wetu kafanikiwa kutinga huko ulaya na kweli anatoa burudani safi ila tatizo ni hapa kwenye maslahi.

Wengi wakisikia analipwa milioni 40 kwa mwezi wanaona ni nyingi sana ila ni mshahara mdgogo ama wa kawaida mnoo katika soka la kulipwa barani ulaya,

Pengine akisogea ligi za uingereza ambako wengi wamekejeli kwamba atakosa namba aua timu zinazomtaka hazishiriki uefa ama europa, yawezekana ikawa ni neema tosha wndapo akihamia hizo timu ambazo zinaweza kumlipa vizuri zaidi akawa kwenye levo zinazokaribia na wachezaji wa kawaida kama kina wanyama wanavuta milioni 200 hivi kwa wiki

Kijana umri unaenda, kwa sasa ana miaka 27 kabakiza miaka micjache ya kuwa katika standard nzuri kwenye soko .

Je ni muda muafaka wa kijana kwenda ligi za england ili apambanie maslahi???
 
Ili kufanikiwa lazima upitie maumivu.Genk ndiyo timu iliyokubali kumtangaza naye pia ameirangaza uefa hivyo sasa njia iko wazi yeye kwenda uingereza maana kazitungua timu kama LIVERPOOL bila huruma kwanini abakie.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona unateseka sana na maisha ya mwenzako? Huyo Samatta unamfahamu zaidi ya kumsoma kwenye magazeti? Au wewe umri wako umesimama ila wa Samatta ndiyo unasonga mbele?
 
Kwani England anaenda kwa kutaka yeye au kwa kiwango chake cha mpira?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzuri wa wabongo tunapenda sana kufatilia ya wenzetu. Kwani mkuu mbona yeye mwenyewe anayehangaika kwa mazoezi na shida za uwanjani karidhika mimi na wewe ni kina nani tuanze kukosa raha na mshahara wa mtu mwingine hadi tumjadili mkuu?

Lakini pia, kwanini usilinganishe tofauti yake na kina Ngassa wanaolipwa milioni moja kwa mwezi?
 
Ili kufanikiwa lazima upitie maumivu.Genk ndiyo timu iliyokubali kumtangaza naye pia ameirangaza uefa hivyo sasa njia iko wazi yeye kwenda uingereza maana kazitungua timu kama LIVERPOOL bila huruma kwanini abakie.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli kabisa, Liverpool ama timu nzuri ikimtupia jicho basi kujana anaweza kuanza kuvuta angalau milioni 150 kwa wiki
 
Kwa ligi aliyopo 40 ni nyingi. Akisogea Germany anaweza sogea labda hadi 75-80+
Ndio hivyo mkuu, Insallah akisogea pa;e uingereza kwa team zenye mkwanja anaweza kuanza kupokea milioni 200 hivi kama kina wanyama
 
Kodi 80% ya huo mshara. Haaa
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kodi 80% ya huo mshara. Haaa

Sent using Jamii Forums mobile app
Smata yupo belgium, Serikali inachukua asilimia 53 ya pato lile la milioni 40 kwa mwezi, hivyo anabakiwa na milioni 18 hivi kwa mwezi

Hivi vitu viliwahi kuwaumiza sana ronaldo na messi, ronaldo aliomba mkataba wa kulipwa mshahara wake baada ya kodi, kijana alikuwa ana mshahara wa milioni 800 kwa wiki, akipokea hasumbuliwi na tra za huko spain, kiufupi mshahara waliokuwa wakimpa ni takribani bilioni moja na nusu na wakienda kulipa kodi zake ndio wanamuingizia benki hio milioni 800

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…