UTPC
Journalists' Union
- Apr 17, 2026
- 51
- 38
Unapofika kwenye baadhi ya masoko katika Manispaa ya Morogoro ni kama mahame au yamegeuka kuwa mahame yasiyo na uhai wa kibiashara uliotarajiwa. Badala kusikika kwa kelele za wanunuzi wakibishania bei, vicheko vya wafanyabiashara na harufu ya bidhaa mpya, unakutana na ukimya ‘unaosindikizwa’ na upepo unaopita katikati ya vizimba vilivyoachwa wazi.
Ni taswira inayoibua maswali, hasa ikizingatiwa kuwa masoko haya yalijengwa kwa gharama na matumaini makubwa ya kuboresha maisha ya wafanyabiashara wadogo maarufu kama wamachinga na kuwezesha wananchi kupata biadhaa zao katika mazingira stahiki.
Hali ilivyo Barabara ya Madalaka Manispaa ya Morogoro nyakati za usiku wafanyabiashara wakipanga na kuuza bidhaa zao kando ya Barabara Hali inayohatarisha Usalama wa watumiaji wa Barabara hasa watembea kwa Miguu.
Katika soko la Machinga Complex lililopo eneo la Fire, hali hii ni dhahiri kabisa. Soko hili lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 266, limebakiwa na wafanyabiashara 39 pekee.
Vizimba vilivyojengwa kwa mpangilio mzuri, kimya kimya vinageuka kuwa kama magofu. Kadhalika meza nyingi zipo tupu, na zile chache zenye watu, wafanyabiashara wake wanakaa bila wateja, wakipoteza muda kwa michezo ya drafti na bao wakisubiri siku ipite.
Hali si tofauti sana katika soko la Azimio. Hapa, eneo ambalo lilipaswa kuwa kitovu cha biashara ndogondogo, limegeuka kuwa uwanja wa watoto kucheza mpira wa sodo. Ni ishara ya wazi kuwa pengine kuna tatizo zaidi ya kile kinachoonekana juu juu. Na linaweza kuwa atizo la mfumo, mipango na uhalisia wa maisha ya kila siku ya wafanyabiashara.
Chanzo ni nini?
Uchunguzi unaonesha kuwa chanzo kikuu cha hali hii ni msigano mkubwa uliopo kati ya mipango ya mamlaka za miji na mahitaji halisi ya wafanyabiashara pamoja na wateja wao.
Wakati serikali inasisitiza umuhimu wa kufuata sheria na kufanya biashara katika maeneo rasmi, wafanyabiashara wanahisi kuwa kufuata taratibu hizo ni sawa na kujihukumu kufa njaa.
Omary Habibu, mmoja wa wafanyabiashara waliobaki katika soko la Machinga Complex, anaeleza hali ilivyo akisema wateja wa sasa wanahitaji huduma ya haraka na hawapo tayari kutembea umbali mrefu kuingia sokoni.
“Mteja anaposhuka kwenye daladala, anataka apate huduma hapo hapo. Akiona anapaswa kutembea hadi ndani ya soko, anaamua kununua kwa wale walioko barabarani. Hapo ndipo tunapopoteza wateja,” anasema Omary.
Kauli yake inaungwa mkono na Mwenyekiti wa soko hilo, Bw. Walter Mboya, ambaye anaeleza kuwa changamoto si tu umbali, bali pia aina ya miundombinu iliyojengwa kutokidhi mahitaji ya wafanyabiashara waliopo.
“Soko hili lilijengwa likilenga zaidi wauza mbogamboga, lakini wengi wetu tunauza bidhaa za viwandani kama viatu, nguo na mabegi. Miundombinu yake haiendani na biashara zetu,” anasema Bw. Mboya.
Anasisitiza kuwa kutoshirikishwa kwa wafanyabiashara katika hatua za kupanga na kujenga masoko hayo kumesababisha majengo hayo kukosa uhalisia wa matumizi. Kwa lugha nyepesi, masoko yamejengwa bila kuelewa nani hasa atayatumia na kwa namna gani.
Licha ya kuwepo kwa masoko 11 yenye uwezo wa kuhudumia wafanyabiashara 3,444, bado zaidi ya wamachinga 33,000 wanaendelea kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi. Hii inaonyesha wazi kuwa tatizo si uhaba wa masoko pekee, bali ni ubora na ufanisi wa masoko hayo.
Hali hii inazidi kuchochewa na ukuaji wa kasi wa mji wa Morogoro. Kwa mujibu wa takwimu za Sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022, idadi ya watu imefikia 471,072, ikiwa ni ongezeko kubwa la watu 155,543 tangu mwaka 2012 (miaka 10 iliyopita).
Ni dhahiri ukuaji huu umeongeza mahitaji ya huduma na nafasi za biashara kuongezeka lakini miundombinu haijaendana na kasi hiyo. Kadhalika maeneo ya kiutawala yamepanuka kwani kata zimeongezeka kutoka 19 hadi 29.
Sehemu ya vizimba vya soko la Machiga Complex vikiwa wazi Huku wafanyabiashara wakibaki Barabarani
Athari kwa Manispaa
Kwa upande wa mamlaka, changamoto hii pia ina athari za moja kwa moja kiuchumi. Mkuu wa Idara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji wa Manispaa ya Morogoro, Bw. John Kulunge, anakiri kuwa kuondoka kwa wafanyabiashara katika masoko rasmi kunasababisha upotevu mkubwa wa mapato.
Anasema manispaa hulazimika kutumia fedha nyingi kulipa askari wa akiba (mgambo) ili kuwazuia wafanyabiashara kufanya biashara barabarani—fedha ambazo zingeweza kuelekezwa katika huduma za kijamii kama elimu na afya.
Uchunguzi wetu umebaini kuwa askari mmoja wa jeshi la akiba analipwa Sh. 150,000/- kwa mwezi ambapo manispaa huingia mkataba na askari 10 hadi 20 kulingana na bajeti ya wakati husika.
Kwa upande mwingine Manispaa hupoteza mapato kwa kutokana na kukosa ushuru kwa wafanyabiashara wanaoondoka. Mathalan, uchunguzi umebaini kuwa katika soko la Machinga Complex pekee, wafanyabiashara 227 wameondoka. Kila mmoja alipaswa kulipa shilingi 10,000 kwa mwezi, hali inayosababisha manispaa kupoteza zaidi ya shilingi milioni 2 kwa mwezi.
Ushirikishwaji wa wadau
Pamoja na uwepo wa sheria kama Sheria ya Mipango Miji Na. 8 ya 2007 na Kanuni zake za mwaka 2018, wadau wengi wanadai kuwa utekelezaji wake umekuwa wa kinadharia zaidi kuliko vitendo.
Sheria hiyo katika kifungu cha 4 (1), inazitaka mamlaka za miji kuhakikisha matumizi bora na utaratibu madhubuti wa ardhi, usalama na usawa katika upatikanaji wa rasilimali na ushiriki wa umma katika kutekeleza sera za matumizi ya ardhi. Ujenzi wa masoko ni moja ya matumizi ya ardhi.
Hata hivyo, wananchi wanahisi hawashirikishwi kikamilifu katika maamuzi yanayowahusu. Bi. Doto Juma Fungeni, mjumbe wa Serikali ya Mtaa wa Azimio, anatoa mfano wa pendekezo lao la kuomba daladala ziruhusiwe kuishia karibu na soko ili kuongeza wateja—pendekezo ambalo halijapatiwa majibu hadi sasa.
“Tuliomba halmashauri kwa kushirikiana na LATRA iruhusu daladala ziishie eneo la soko la Azimio ili kuongeza wateja, lakini hadi sasa hatujapata majibu. Wafanyabiashara wamehamia barabara ya Mazimbu kutafuta mzunguko,” anasema Doto.
Suala la ushirikishwaji pia linatajwa na Mwenyekiti wa Wamachinga Mkoa wa Morogoro, Bw. Faustine France ambaye anasisitiza kuwa ushirikishwaji ni kiini cha suluhisho la masuala mengi. Anatoa mfano wa ofisi ya wamachinga iliyojengwa bila wao kushirikishwa, tena katika eneo lisilofikika kirahisi kwa wafanyabiashara wengi.
“Wamachinga wanafanya biashara maeneo ya Kingalu, Msavu na katikati ya mji. Sasa ofisi inajengwa mbali kabisa—hata kupata huduma ni changamoto,” anasema.
Ngoja nikupe mfano mmoja ndugu mwandishi ambao ni ushahidi wa hatushirikishwi, serikali imejenga ofisi ya wamachinga bila ya kutushirikisha, kuna siku nilienda manispaa kudai ofisi, ndiyo nilielezwa njoo uone ofisi yako imejengwa maeneo ya Mkundi baada ya kumaliza daraja la SGR, nikahoji wakati mnajenga ofisi hii mlimshirikisha nani” alisema Bw. France.
Kwa mtazamo mpana, hali hii inaonesha kuwa biashara kando ya barabara si ukaidi wa sheria kama inavyoweza kuonekana, bali ni ishara ya pengo kubwa kati ya sera na uhalisia wa maisha. Wafanyabiashara wanachagua maeneo yenye mzunguko wa wateja, hata kama si rasmi, kwa sababu hapo ndipo kuna uhakika wa kipato.
Wajibu wa mamlaka
Kanuni za Usimamizi wa Mipango Miji za 2018 (Sehemu ya 17–19) zinatoa wajibu na jukumu la kisheria kwa halmashauri kutenga maeneo maalum ya biashara, kuepusha mwingiliano hatari kati ya binadamu na vyombo vya moto, kulinda mpangilio na usafi wa miji.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro, Bw. Khalid Matengo, anasema kuwa mwelekeo wa halmashauri si kutumia nguvu bali kutoa elimu na kuhamasisha urasimishaji wa taratibu.
Anakiri kuwa mchakato huo unahitaji muda na uelewa wa pande zote mbili—serikali na wafanyabiashara. Hata hivyo, wadau wanasisitiza kuwa bila kushirikisha moja kwa moja walengwa, jitihada hizi zinaweza kuendelea kukwama.
Kwa mujibu wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2025–2030, kuna msisitizo wa kuweka mazingira rafiki kwa sekta isiyo rasmi na kuhakikisha urasimishaji unafanyika kwa njia shirikishi na endelevu. Hii ni hatua muhimu inayoweza kuleta mabadiliko ikiwa itatekelezwa kwa vitendo.
Kwa sasa, picha inayoonekana katika masoko ya Morogoro ni ya miundombinu iliyopo lakini isiyotumika ipasavyo. Ni kama hadithi ya nyumba nzuri iliyojengwa lakini haina wakazi. Swali linalobaki ni je, mamlaka na wadau wataweza kukaa pamoja na kujenga mfumo unaozingatia uhalisia wa maisha ya wafanyabiashara?
Kwa sababu mwisho wa yote, soko si jengo pekee—ni maisha, ni mzunguko wa fedha, ni matumaini ya mtu anayehangaika kila siku kutafuta riziki. Bila kuyatambua hayo, hata masoko mazuri zaidi yataendelea kubaki mahame.
ANDIKO LA: Farida Mangube, Morogoro