Masoud djuma ..na kiatu kisichomtosha..

Masoud djuma ..na kiatu kisichomtosha..

Tangu Mtibwa wawe apeche alolo sioni timu nyingine ya kushabikia hapa Tanzania.

Timu zinafukuza makocha kama zimetumwa!!! Eti mchezaji anakua mfungaji bora msimu huu na timu yake inachukua ubingwa, msimu unaofuata analetwa kocha mpya halafu anasema huyo mchezaji (aliyekua mfungaji bora msimu uliopita) hana stamina hivyo hamtaki anamuuza.

Hii ligi yenyewe na TFF yote utumbo (Bora enzi za Leodgar Tenga), ukipata gazeti la leo ukaangalia msimamo wa ligi utakuta kuna timu zimecheza mechi 6 nyingine 7 nyingine 3 nyingine 4. Ligi za wenzetu utakuta nyingi zimecheza 7 halafu zilizobaki timu nne zimecheza 6 na weekend ndiyo wanakamilisha.

Rais alitaka kuhamia Posta akapange jengo wakati TFF ina jengo lake. Na yule jamaa akaulizwa kwanini Taifa Stars tunabanwa michezoni, bila aibu akajibu tatizo ni jezi.

Kufuatilia mpira Tanzania ni kujichosha.
Haahaha et apeche alolo [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji119]
 
DJUMA, BORA UKWELI MCHUNGU, KULIKO UONGO MTAMU.

-Rafiki yangu Masoud Djuma amepeana mkono wa kwaheri na mabosi wa Simba. Muda wowote kutoka sasa ataenda Uwanja wa Ndege kuianza safari ya kurudi kwao Rwanda. Simba haina inachomdai na Djuma mwenyewe hana anachoidai Simba.

-Djuma anaondoka, huku nyuma akiwaacha vinywa wazi baadhi ya manazi wa Simba wanaompenda. Ameiacha sumu hii na ameipakaza sehemu kubwa. Manazi hao wanaamini kaondolewa kwa kuonewa.

-Sio kificho tena. Maneno ya Try Again jana asubuhi yamehitimisha safari ya Djuma kama kocha msaidizi wa Simba. Kama Try Again Rais wa Simba alisema wanatumia nguvu kubwa ya usuluhishi baina ya Djuma na Mbelgiji, lakini mambo yamekuwa magumu, hapa tunapaswa kutumia akili ndogo ya 2 + 2 = 4 kuelewa Djuma hana chake Msimbazi. Try Again alikuwa muwazi.

-Lakini ninachokiamini kuwa kuna siku Djuma atarudi nchi hii kufundisha soka. Kama si msimu huu, msimu ujao. Au msimu mwingine, ila atarudi. Zimwi likujualo, halikuli likakwisha. Djuma hajaondoka kama walivyoondoka makocha wengi wa Simba walioondoka hivi karibuni. Ameondoka kama dume la Nyani linalotembea kwa madaha katikati ya kundi kubwa la nyani wa kike.

-Djuma kama wanadamu wengine ana mapungufu yake. Lakini anajua kufundisha. Anajua kuifanya timu ikacheza anavyotaka. Ana identity yake ya mpira. Ni Guardiola fulani hivi wa 'bei rahisi'. Ana sex football. Anajua kumfunga mpinzani na kumtawala. Hapa ndipo Djuma alipowashika wanaompenda. Hajawashikia kwingine, ni hapa tu.

-Hawa mashabiki wa Simba waliowehuka nae sio wajinga. Kuna kitu wanakiona katika kichwa chake. Simba imewatimua Omog, Mayanja, Lechantre, sababu ni yeye, lakini hii haijafanya manazi hao waache kumuona kama Djuma mwanadamu wa ajabu, ndiyo kwanza wamemuweka vizuri katika mioyo yao na ilichokifanya Simba wanahisi kaonewa. Huu ndiyo 'uchawi' wa Djuma.

-Mashabiki hawa waliamini hata sare yao na Ndanda Fc pale Mtwara na kipigo chao cha Mbao kule Mwanza ilitokana na Djuma kutokuwepo katika benchi lao. Kuna imani fulani wameiweka kwake. Tutakapoona amerejea nchini iwe kufundisha Simba au timu nyingine tusishangae.

-Katika kipindi hiki ambacho Simba inaenda katika uchaguzi, si ajabu wagombea wakatumia jina lake kuombea kura kwa wanachama. Ni mwanachama gani asiyetaka kusikia ngoma za masikio yake likipenya neno urejeo wa Djuma kwa mara nyingine? Ni wengi, wasiomtaka ni wachache wanaohesabika kwa vidole vya miguuni, mkononi. Wengi watataka.

-Wakati mwingine inakanganya na kuleta maswali magumu unapoona Djuma huyu anayekubalika hivi, ameifanyia nini Simba? Inashangaza kidogo.bHiki kiburi chake kilipaswa kuwepo kwa Selemani Matola aliyefanyia makubwa Simba, lakini msimu wake mmoja tena kama kocha msaidizi amekuwa star. Anasifiwa kuliko inavyosifiwa Simba yenyewe.

-Narudia tena iko siku Djuma atarudi nchi hii. Naamini hivi. Siamini vingine. Ni ngumu tembo kupenya tundu la sindano, lakini ni rahisi Djuma kurudi nchini. Iwe Simba. Iwe Yanga. Kokote kule, lakini atarudi tu! Si ajabu viongozi hawa waliopeana nae mkono wa kwaheri ndiyo watakaomtumia tiketi ya ndege kumtaka arudi nchini. Hupaswi kuwaamini sana viongozi wetu wa soka. Nao wana mihemko yao.

-Tumewahi kushuhudia kwa Partick Phiri. Miaka ya hivi karibuni huyu anakuwa kocha aliyetimuliwa mara nyingi na Simba na hapo hapo kuwa kocha aliyeifundisha mara nyingi katika vipindi tofauti. Phiri anatimuliwa mchana, jioni anarejeshwa. Nasikia mwenyewe ameizoea hali hii, haimpi shida.

-Sitashituka Djuma akiwa Phiri mwingine. Kunataka moyo wa Hawafu mwenye nguvu kuachana moja kwa moja na Djuma. Djuma si Omog, Djuma si Mayanja, Djuma si Lechantre, Djuma ni Djuma tu. Yuko mmoja kama alivyo.

-Mwisho kabisa namtakia kila la kheri rafiki yangu Djuma. Safari njema my friend na fika salama, ila wacha nikunong'oneze kitu hakikisha simu yako inakuwa na chaji muda wote. Burundi na Tanzania sio mbali. Bon Voyage my friend Djuma.
Unaonekana ni mwandishi mzoefu wa soka la bongo, hizi feki id zinaficha mengi
 
Miaka yote huwa naamini adui yako hatoki mbali... yaani yupo karibu yako..
ndo kinachomkuta masoud djuma.. kocha msaidizi wa simba sc.. ni kipenzi cha mashabiki. anapendwa na wengi ,lakini viongozi hawana imani nae tena, alikuja kocha mfaransa akashindwana nae.. na pia huyu mbelgiji wamegombana.. moja kwa moja utagundua tatizo ni masoud djuma mwenyewe.. kwanini??
mara nyingi huko ulaya kocha msaidizi anahusika na pg za mazoezi.. ila kikosi anapanga kocha mkuu.. hii inazuia kutoingiliana majukumu... inasaidia kila mmoja kuona anawajibika.... sasa palé simba masoud anaona kama hasikilizwi, so njia anayotumia ni kuwashawishi wachezaji Kuwa upande wake.. masoud anautaka ukocha mkuu.. lakini inabidi akubali Kuwa yeye bado sana yaani Viatu bado havimtoshi.. akiwa kocha mkuu kwa muda.. alipoteza final sportpesa kisha akaja kapoteza final kagame na azam na ilionekana wazi kabisa djuma ni mzito wa kufanya sub zenye macho, kiufupi masoud aendelee kupata uzoefu...

"mchizi kichizi "
Hizo final alipoteza kwa wachezaji wapi? Kikosi kipi, kumbuka wachezaji wengi walipewa likizo
 
Hizo final alipoteza kwa wachezaji wapi? Kikosi kipi, kumbuka wachezaji wengi walipewa likizo
Kocha mkomavu anaenda hata na team b.. mbona gor mahia wachezaji wao wengi walikuwa national team na bado waliwafunga..??
 
Lakin timu ilifika fainali Mkuu,
Kagame Simba ilikua ikijaribu kikosi kipya, ndio maana hukuwaona kina Bocco, Kichuya, Mkude, Manula etc,
Sasa unapojaribu kikosi kwenye mechi kubwa kama zile lolote linaweza kutokea,
Labda tujiulize wazo la kuchezesha kikosi kipya ambacho hawajawahi kucheza pamoja lilikua lake au la Uongozi?
Wachezaji nyota wote hawakuwepo, ndio maana tulilalamika kukosa wachezaji wetu kwenye mashindano makubwa kama yale.
 
Mie siuoni ubingwa mwaka huu kwa huyu kocha. Kiufundi hayupo vizuri sana ukizingatia ubora wa wachezaji aliokuwa nao.
Umeandika kwa emotion na uelewa mkubwa wa soka la simba, nampenda masoud namtakia kila la kheri, Bado sijaona kama kuna kipya mbelgiji atakileta msimbazi na bado naamini kwa masoud.

Thanks Djuma
 
Kama mpaka sasa ujui uzandiki wake sina sababu ya kukwambia maana wewe tayari upo upande wake

Simba ni taasisi kubwa lazima imfanye mtu aitegemee na wala sio yeye ndio ategemewe na Club ukiangalia hiyo mgogoro inayoibuka kila mara baina yake na makocha wakuu huoni kama ni conflict zinazoipa panic club
Hilo jibu ni la jumla sana, migogoro maana yake nini. Kupishana mawazo ni jambo la kawaida tatizo nyie wajamaa huwa hampendi mawazo mbadala mnataka 'ndio mzee' kama wabunge wa CCM.
 
Tulifungwa na Gor Mahia 2-0, alifunga Tuyisenge na Meddie Kagere wote hao ni wachezaji wa Rwanda, unasemaje wachezaji wao walikuwa national team.
Kocha mkomavu anaenda hata na team b.. mbona gor mahia wachezaji wao wengi walikuwa national team na bado waliwafunga..??
 
Simba ndio timu inayoongoza kwa kufukuza makocha wenye performance nzuri uwanjani kwa sababu za nje ya uwanja.
Sababu za nje ya uwanja?? na kocha Ana rekodi nzuri uwanjani..mambo ya nje ya uwanja yanamuhusu nini??
 
Tulifungwa na Gor Mahia 2-0, alifunga Tuyisenge na Meddie Kagere wote hao ni wachezaji wa Rwanda, unasemaje wachezaji wao walikuwa national team.
kumbuka rwanda alikuwa na mechi wiki chache baadaye... halafu Kenya walikuwa India.. palé gor wachezaji wengi wa kikenya walikuwa team ya taifa.. kuwaga na kumbukumbu..
 
Fuatilia kumbukumbu vizuri. Kenya walikuwa bado wapo kwenye ligi wakiwa na vikosi vyao vya kwanza.
Acha uongo Kenya ligi yao walishamaliza.. wakawa Wanasubiri simba wamalize ligi ndo sportpesa ianze....usitufanye sisi wajinga.. mpaka kocha alilalamika ratiba ya kufungulia yao ni ngumu..
 
Hilo jibu ni la jumla sana, migogoro maana yake nini. Kupishana mawazo ni jambo la kawaida tatizo nyie wajamaa huwa hampendi mawazo mbadala mnataka 'ndio mzee' kama wabunge wa CCM.
Mbona ulaya hatuskii migogoro ukiachana na mabeef ya kocha na mchezaji..
 
Wachezaji nyota wote hawakuwepo, ndio maana tulilalamika kukosa wachezaji wetu kwenye mashindano makubwa kama yale.
Nyie si ndo mmewapa likizo.. Sasa mnamlalamikia nani??mchezaji mkubwa ndo huyo okwi??
 
Huwezi kusikia migogoro kwa sababu wamezoeza akili zao kupishana mitazamo. Mgogoro unakuja pale ambapo mtu hataki mawazo kinzani.
Mbona ulaya hatuskii migogoro ukiachana na mabeef ya kocha na mchezaji..
 
Back
Top Bottom