Masoud Kipanya adaiwa kukamatwa kwa kuchora katuni ya kichochezi. Yeye aibuka, adai aliyetoa taarifa 'AMESAIDIA'

Mkuu wa kaya anayekushauri kwenye hii kamatakamata anakupotosha! Za kuambiwa changanya na zako ....
Ina maana umesahau kuwa yeye hashauriwi na ukishauri ndio umeharibu kabisa? Samehe lakini usiisahau!
 
#BREAKING_NEWS

Mchoraji wa katuni Masoud Kipanya amekamatwa na Jeshi la Polisi muda mfupi uliopita kwa tuhuma za uchochezi baada ya kuchora katuni inayoichonganisha serikali na wananchi.

Habari24UPDATES
 
Hio katuni iko wapi!? Kuna wengine hawajaiona, weka kwa faida ya wengine, ili mjadala uwe hot.!
 
Bado hakuna reliable source!
Ilikuwa ni Chadema in blood (sasa imefutwa), huko nako ukienda huoni kitu.
Nikikumbuka na rekodi ya Mwanahabari Huru kwa post za uongo uongo basi nachoka...
 
Afu nimewahi sikia hyu jamaa ana mihela sana afu anamiliki ndinga kali
 
Suala la usalama si kwa wapinzani peke yao. Hata kwangu mimi na wewe.

Pia yakupasa uelewe kuwa huyo huyo polisi anafanya kazi kwa kusimamiwa na sheria. Hajapewa bunduki yenye risasi za moto aitumie kama atakavyo. Amepewa aitumie inapobidi. Ndio maana mwisho wa askari kupiga risasi ni kiunoni ambako hawezi kuua. Kazi yake ni kukata waharifu na kuwapeleka mahakamani.

Ndio maana nikasema, askari WA kweli ana mafunzo maalumu ya kukabiriana na uharifu. Uaskari hauendeshwi kwa hisia za askari. Atatumia siraha ya moto pale atakapokutana na muharifu mwenye siraha ya moto anayekataa kutii amri ya askari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…