Naomba wabunge wapitishe mswada utakaotoa muongozo wa namna ya kuikosoa serikali, kila kitu kiwekwe wazi nani anaruhusiwa kuikosoa serikali, atumie njia gani na wakati gani. Kama haitakiwi kuwakosoa basi waseme humo humo.
Wasitufanyee wajinga mtu ukiamka tu unajsikia unapindisha sheria unamkamata mtu, hii inajenga chuki baina ya wananchi na serikali yao, mnajifanya mnazuia uchochezi kumbe ndio mnatuchochea zaidi kutokana na uonevu mnaofanya kwa kupindisha sheria.
Ni bora tujue moja kwamba hatuna haki ya kuhoji chochote serikali inachofanya kuliko mtudanganye kwamba tuko huru kusema chochote halafu mnatukamata.