Masoud Kipanya na Fina Mango wa Clouds FM

Status
Not open for further replies.
Who give a damn on what they are doing, let's discuss issues not people or events wakubwa! Nadhani tuwaache tu wafanye au kuchagua wanachopenda.....kuna watu wengi sana wanaacha kazi na kuajiriwa!! Naomba kuwasilisha

Acha roho mbaya wewe,

wao mchango wao ulikuwa mkubwa sana hapa Tanzania ndio sababu unaona kila mtu anawaulizia,ndio wengi sana wanaacha kazi,lakini ni kwa nini hawa tu ndio tuwajadili?Jiulize,tafakari na upate jibu

Paulo anaboa sana afadhali ya Hando,kile kipindi kimeharibika sana.
 
Mimi hapo nadhani pia kuna upande wa maslahi kama ninavyoijua hiyo redio ya watu mara nyingi vipindi hujiendesha kulingana na udhamini wa kampuni kubwa mbalimbali suala la mshahara au posho linakuja baadae sasa hapo KP atakuwa amelizungumzia hilo lakini naona amesahau upande wa wadhamini hawa jamaa nadhani kutokana na utundu na umaarufu wao waliweza kujipatia wadhamini wa kuendesha vipindi vyao pamoja na ofisi kama ofisi kupata fungu lake. Sasa hiyo nadhani kwa kiasi fulani lazima itakuwa imewapa kujiamini fulani katia kazi lakini mwisho wa siku unakuwa unaifanyia kazi taasisi fulani na huo naweza kusema ndio ulikuwa udhaifu mkubwa wa clouds. Sasa jamaa naona jamaa wameamua kucontrol kila aspect na kimsingi kugoma kama kugoma ina taratibu zake katika kazi sio ujamkie tu asubuhi na uanze kugoma. Mimi simlaumu KP ila hiyo ni changamoto kwake najua hata yeye inaweza kumkuta je ni uamuzi gani ambao atautoa. Big up KP life goes on huwezi kufanikiwa usipojifunza kutokana na makosa.
 
Acha roho mbaya wewe,

Paulo anaboa sana afadhali ya Hando,kile kipindi kimeharibika sana.

Mi naona hamko fair kwa Paulo, as so far he is doing good.....tukuchukue wewe uende ukatangaze pale tuone itakuwaje. Na ugumu wa PB sio kutangaza kama vipindi vingine, kwamba u need to have a story to read or tell, pale unatakiwa kupiga story. Gerald was kama alivyo Paulo wakati anaanza, but look at him right now yuko wapi. He is very good in what he does. Najua kuwapoteza Fina na Masoud ni pigo, lakini pia waliopo wanafanya vizuri tu na wataendelea kufanya freshi. Kwa hizi siku chache Paulo ameimprove sana na ataendelea kukua.

Najua JF iko hapa kujenga, wala sio kudondosha na kukatisha tamaa watu....

Hakuna mtu yeyote ambaye wiki ya kwanza katika chochote atafanya sawa na aliyekifanya kwa miaka nane. Kwa hiyo it is too early kuanza kumlinganisha Paulo na Masoud
 
What Masudi expressed ndio ukweli wa hali halisi kwenye sekta binafsi, natamani angebaki.. lakini nina i mani jamaa atashine zaidi huko mbele kutokana na kipaji na tabia yake hasa ukilinganisha upembuzi wake na kiwango chake cha elimu, he is talented
 
KP keep up the good work.....

Usikute watu walikuwa wanakutafutia sababu tu ili wakunyuke barua. By the way mlikuwa mwiba kwa watu wote wanaoenenda kinyume na matarajio ya watanzania, sasa usikute (na nasema tu USIKUTE, which is very likely) mabosi wako walikuwa washapewa KAUSHAURI kwamba inabidi wawape barua ya kukutakia success kwenye hiyo future endovours yako......
 
Pole KP, ni mambo ya kawaida hapa duniani,lakini naamini maisha yanaendelea
 
KP, baada ya muda mfupi tu utagundua hili limekuja kwa wakati muafaka wa wewe kujimuvuzisha mbele! You have the potential, wenye kuona wanaona. Na hata kama ni maslahi, you have all the right to ask for better if you bring more people kufungulia Clouds FM asubuhi na mapema na tena kuwapata hao wadhamini wanaogombea chance! Km kipindi hovyo watakuja? Move on Brother and keep the fire burning!
 
Mtafuteni na Fina mwana wa Mango na yeye pia aweke mambo yake hadhalani.
 
sasa anaenda kuwa employer wa private sector, tena mzawa kama bosi wake wa zamani.
yuko upande wa pili wa shilingi.
We done masudi, we said.
atakayeongeza au kupunguza jambo ana lake.
All the best,
tulikujua tangu Business times, kipanya kikaja juu, clouds na sasa baada ya clouds, ni masudi yule yule ila anakua mkubwa na elimu unaipata kila uchapo,
tuko wote tu, labda ubadilike uwe fisadi.
 
Masudi amenifurahisha sana na majibu yake, yanaonesha ukomavu na utulivu wa akili. Hii ni aina ya watu wa kipekee sana, ambao kwa hakika wanatamanisha kuajiri, ningekuwa na biashara ya redio au televisheni hakika ningemtafuta huyu Masudi nimpe hiyo kazi, kwa lugha ya siku hizi Masudi ni "kichwa". Wala "hajawatupia madongo" waliomtimua, wala waliochukua nafasi yake, na badala yake anazidi kuwapa wasikilizaji matumaini na kuwatunzia heshima waliomfukuza!

Jambo la pili Masudi amenikumbusha kitu ambacho wenzangu wengine waliopitia seminari za kikatoliki wanalifahamu, "kushauriwa"! Kule kulikuwa hakuna kosa dogo! Ukisikia unaitwa kwenda kushauriwa elewa ndio nyumbani hivyo, shule imeisha! Mkuu anakuambia tu "tunakushauri ukajaribu maisha mengine na tunakuombea kila la heri, Mungu akubariki!" Kama utani vile!

Suala la usalama kazini kweli ni kero kubwa, lakini nadhani pia inafaa kuangalia aina za mikataba tunayosaini ambayo ndiyo inayowaruhusu waajiri kutufukuza kazi kwa staili hiyo aliyotuambia Kipanya. Tunahitaji washauri wa kisheria katika haya masuala ya kazi, hasa kwa mtu aliyekuwa anafanya kazi yenye ushawishi kama Kipanya, kuishia kufukuzwa kirahisi hivyo haileti picha nzuri.
 
Kithuku umenikumbusha mbali saaana kaka! Niliitwaga na 'fadha' enzi hizo...mhh..nashukuru sikufukuzwa lakini..Cha moto nilikipata!! yaani umekuwa kama vile you were in my shoes! GUESS WHAT? NILIKUWA SIJAINGIA "MORNING PRAYER" SIKU HIYO... ALL IN ALL I LOOK BACK WITH HUMILITY AND GRATITUDE. IAM SURE IAM HERE BECAUSE OF SUCH PEOPLE LIKE "FADHA'......

On the topic, KP amejibu kwa ukomavu wa hali ya juu sana. Na mtu mwenye kichwa as you put it, this tells all. Lakini unajua nini? kwenye nchi zetu za kimaskini ni rarely kuheshimu mikataba ya kazi..yaani unaajririwa na kufukuzwa at the pleasure of the employer. Na wengi wanakuwa hawana sauti kwa sababu hawana plan B...We acha tuu mkuu..usione watu waoga kutake risk za kuchukua kazi (especially toka serikalini) kwenda private sector..ni kwa sababu ya kuogopa job insecurity.....Hapa KP Unaweza kukuta hajapewa hata warning wala nini..In any case life moves on and I am sure, God allowing, jamaa atazidi kufanikiwa tuu. Wala hana haja ya kuwa na kinyongo..its life..
 
Mi naona hamko fair kwa Paulo, as so far he is doing good.....tukuchukue wewe uende ukatangaze pale tuone itakuwaje. Na ugumu wa PB sio kutangaza kama vipindi vingine, kwamba u need to have a story to read or tell, pale unatakiwa kupiga story. Gerald was kama alivyo Paulo wakati anaanza, but look at him right now yuko wapi. He is very good in what he does. Najua kuwapoteza Fina na Masoud ni pigo, lakini pia waliopo wanafanya vizuri tu na wataendelea kufanya freshi. Kwa hizi siku chache Paulo ameimprove sana na ataendelea kukua.

Najua JF iko hapa kujenga, wala sio kudondosha na kukatisha tamaa watu....
Hakuna mtu yeyote ambaye wiki ya kwanza katika chochote atafanya sawa na aliyekifanya kwa miaka nane. Kwa hiyo it is too early kuanza kumlinganisha Paulo na Masoud

TM,
hatumkatishi tamaa mtu yeyote hapa,hii ni picha halisi mabayo Paulo anatakiwa aijue kuwa PB ina umuhimu gani kwa wasikilizaji na anategemewa afanye nini.Paulo amekuwa mtangazaji miaka mingi tokea RFA,RedioOne/ITV na sasa Clouds (na nadhani kasomea journalism pia) tofauti na KP na Fina ambao wana TALENT.Tunazungumzia ubunifu/creativity and boldness, sio prefessionalism.Paulo kwa wanaomfatilia sio mtu mwenye boldness&creativity ambavyo vinahitajika sana PB.Anyway KP na Fina songeni mbele,ndio dunia hiyo an vikwazo ni njia pia ya kuelekea mafanikio zaidi.
 
sasa anaenda kuwa employer wa private sector, tena mzawa kama bosi wake wa zamani.
yuko upande wa pili wa shilingi.
We done masudi, we said.
atakayeongeza au kupunguza jambo ana lake.
All the best,
tulikujua tangu Business times, kipanya kikaja juu, clouds na sasa baada ya clouds, ni masudi yule yule ila anakua mkubwa na elimu unaipata kila uchapo,
tuko wote tu, labda ubadilike uwe fisadi.

Unajua kuna kitu kimoja huwa nakipenda sana katika maisha. Masoud alikuwa akimuita boss wake Mkurugenzi/Boss. Sasa wakikutana katika mikutano mbali mbali ya kimajukumu, Boss wake naye ataanza kumuita "Mkurugenzi". Yaani hii inaonyesha utamu wa kushift toka kwenye utumwa hadi kwenye ubepari.

Safi sana, endeleza libeneke, na ninavyoamini nyanga zako, si ajabu hao hao mabosi wa clouds wakaja kununua pamba zako = Wateja wako.
 
nimesoma bongocelebrity Kipanya kasema amefukuzwa kazi kwaajili ya kuongelea utendaji mbovu wa wenzao ambao waliwaharibia kipindi cha mahojiano kati yao na balozi.
 
Nimepata bahati ya kusoma blog ya Michuzi muda mfupi uliopita na nimeona taarifa pamoja na maoni mbalimbali ya wadau. Pengine bila ya kutoa ufafanuzi, watu wataendelea kuongea mambo ambayo hayapo kabisa. Ukweli ni huu ufuatao; Nitajizungumzia zaidi mimi kwa vile ishu yetu na Fina ni moja ila maamuzi yanatofautiana kidogo na yanatofautiana si kwa sababu ya upendeleo, la hasha, nataka kuamini ni kwa sababu ya aina ya mikataba tuliyokuwa nayo.Wa kwangu ulikwisha February 28 mwaka huu ingawa nilishaanza kuutumikia mkataba mpya wa miaka miwili, wa Fina unakwisha nadhani mwishoni mwa mwaka huu(sina uhakika)

Mimi sikuacha kazi Clouds Fm kama inavyosemekana, mimi nimepewa barua ambayo inazungumzia ku-revoke (kutengua,kuahirisha) mkataba wangu na Clouds.Nitazungumzia sababu za kupewa barua hiyo, ila kabla sijaingia ndani zaidi, mwisho wa barua ile niliyopewa imesema, nainukuu, ‘we wish you all the best in your future endeavors' mwisho wa kuinuukuu barua niliyopewa na HR Manager wa Clouds Media Group. kwa lugha rahisi ikimaanaisha tunakutakia kila la heri katika mahangaiko yako ya mbeleni.

Kwa mantiki hiyo labda wasomaji waniambie sijaielewa maana ya barua ile, lakini kwa kifupi nilichoelewa ni kwamba, kutokana na makosa niliyoyafanya, Clouds imeonelea kuwa sina sifa za kuendelea kuwa sehemu ya timu ya Clouds Fm. Sasa basi, hebu tuangalie makosa niliyoyafanya mimi pamoja na Fina.

Tarehe 29th May 2008, kwa pamoja, mimi na Fina tuliamua tusiingie kwenye kipindi kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya wenzetu. Kama kuna waliosikia, siku moja kabla yaani tarehe 28th May tulifanya mahojiano na Balozi wa Marekani nchini Tanzania.Bahati mbaya (kwa sababu ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wa Technical Department) mahojiano yale hayakusikika vizuri, yalisikika vibaya mno!!! Na hata vifaa pia havikuwa timilifu, mfano mmoja mdogo tu ni kwamba tulikuwa tunatumia mic moja.Yaani watangazaji watatu na balozi, kwangu ilinipa wakati mgumu sana hasa ikizingatiwa taarifa za interview zilipatikana karibu wiki nzima.Nilitegemea wenzetu wangejiandaa kwa kila kitu. Kwa kifupi watu wa technical walikuwa na uwezo wa kusema kwamba interview isingewezekana kutokana na ufinyu wa signal na vifaa, TUNGEAHIRISHA.Makosa kama haya yamekuwa yakijirudiarudia mara kwa mara na ndio maana nasi tukaamua kuweka msisitizo kwa njia ile ya kugoma.

Najua kuna watakaojiuliza, hapa Gerald anaingia wapi, kwa sababu alisikika wakati wa mahojiano na balozi, akayapata madhira lakini hakugoma. Hilo sitolitolea maelezo nikiamini yeye mwenyewe ndiye mwenye nafasi nzuri ya kufafanua atakapotakiwa kufanya hivyo ingawa halazimiki. Ila ieleweke kwamba, kwenye mpango wa kugoma, ALIHUSISHWA NA AKAUKUBALI.

Kilichofuatia ni kutakiwa tujielezee kwa nini hatukwenda kwenye kipindi, tukajielezea, na hatimaye mimi nikapewa barua niliyoielezea hapo juu na tetesi za uhakika nilizo nazo ni kwamba mtu wa technical kapewa barua ya warning.

Kwa hiyo basi, kuondolewa kwangu hakuhusiani kabisa na suala la masilahi yaani mishahara. Kosa ni hilo hapo juu na tulilifanya kwa nia njema ya kujaribu kujenga zaidi kwa vile tunaamini Clouds inazidi kukua siku hadi siku.

Ni juu ya atakayesoma waraka huu kupima uzito wa kosa na uzito wa adhabu.Kwangu naona sawa kwa sababu si kila kinachotokea lazima kiwe na sababu za msingi. Bado mwenye mali ana mamlaka ya kuamua nani awe kwenye timu na nani asiwemo.Na ninaamini kila anayekosea lazima aadhibiwe,nami nimeadhibiwa na nimeheshimu. Maisha yanaendelea.

Namshukuru mungu na nawahakikishia wachache waliokuwa wakitusikiliza kwamba kamwe hatukuwahi kulewa sifa kwa sababu kama ni kulewa sifa tungeshagoma siku nyingi zilizopita kama suala lingekuwa ni mshahara. Kwa wenye kumbukumbu, Power Breakfast ilianza kama ‘wake up show', enzi hizo kipindi kilikuwa kinaanza saa 11 alfajiri, maana yake ni kwamba mimi na Fina tulikuwa tunaamka saa 10 alfajiri, kwa mshahara wa kawaida kabisa na bado tuliweza kulibeba jahazi.

BC: Unawaambia nini wapenzi wasikilizaji wenu na wasikilizaji wa CloudsFm kwa ujumla?

KP: Nawaambia wasikilizaji wa Clouds na wasomaji wa Bongo Celebrity kwamba tuwe wepesi wa kukubali matokeo kama vile tunavyoweza kukikubali kifo kinapotutenganisha na wapendwa na tunaowachukia.Pia tuweze kukubali kwamba kila kitu kinajengwa taratibu. Hata waliobaki powerbreakfast wana vipaji na uwezo wa kukipeleka juu zaidi, kikubwa kinachohitajika ni subira yenu mnaowasikiliza, msijaribu kuwalinganisha wala kutafutia makosa. Mwisho wa siku mtazoea na mtafurahia.

Kwa upande wangu, napumzika kidogo, naelekeza nguvu zaidi kwenye katuni na kabiashara kangu kadogo. Pengine wakati umefika wa kuwekeza zaidi kwenye haka kabiashara.

Mwisho kabisa nawaomba radhi wale ntakaokuwa nimewakwaza kwa kuyaanika haya, ila kwangu ni kwa faida zaidi kwani ninapochora katuni nategemea wasomaji zaidi ambao ni watu, na ninapokuwa mmachinga wa nguo nategemea watu pia.Hivyo basi bila UFAFANUZI ni rahisi kwa watu hao ambao ni wasomaji wa katuni na wanunuzi wa nguo zangu kunishusha thamani kwa kudhani tumeacha Clouds kutokana na kudhani tumeshakuwa wakubwa hivyo basi tumeanza kuringa. LA HASHA!!!SIKUACHA CLOUDS, NIMETIMULIWA (nahofia kuuzungumzia mkataba wa Fina kwa kuwa una mambo yake haswa upande wa kisheria) NA SIJAPATA KAZI,ILA NINATAFUTA KAZI ILI WANANGU WAENDELEE KWENDA CHOONI. WALA SIJACHUKULIWA NA TBC, KWANZA UTUKUFU WALIONAO ZE COMEDY HATA ROBO SIJAUFIKIA.

Laiti nisingekuta mjadala kwenye blog ya Michuzi wenye kulaumu, kuponda kutoa pole na kutia moyo, kamwe nisingeyasema haya.Naomba kuwasilisha.
 
Nimepata bahati ya kusoma blog ya Michuzi muda mfupi uliopita na nimeona taarifa pamoja na maoni mbalimbali ya wadau. Pengine bila ya kutoa ufafanuzi, watu wataendelea kuongea mambo ambayo hayapo kabisa. Ukweli ni huu ufuatao; Nitajizungumzia zaidi mimi kwa vile ishu yetu na Fina ni moja ila maamuzi yanatofautiana kidogo na yanatofautiana si kwa sababu ya upendeleo, la hasha, nataka kuamini ni kwa sababu ya aina ya mikataba tuliyokuwa nayo.Wa kwangu ulikwisha February 28 mwaka huu ingawa nilishaanza kuutumikia mkataba mpya wa miaka miwili, wa Fina unakwisha nadhani mwishoni mwa mwaka huu(sina uhakika)

Mimi sikuacha kazi Clouds Fm kama inavyosemekana, mimi nimepewa barua ambayo inazungumzia ku-revoke (kutengua,kuahirisha) mkataba wangu na Clouds.Nitazungumzia sababu za kupewa barua hiyo, ila kabla sijaingia ndani zaidi, mwisho wa barua ile niliyopewa imesema, nainukuu, ‘we wish you all the best in your future endeavors’ mwisho wa kuinuukuu barua niliyopewa na HR Manager wa Clouds Media Group. kwa lugha rahisi ikimaanaisha tunakutakia kila la heri katika mahangaiko yako ya mbeleni.

Kwa mantiki hiyo labda wasomaji waniambie sijaielewa maana ya barua ile, lakini kwa kifupi nilichoelewa ni kwamba, kutokana na makosa niliyoyafanya, Clouds imeonelea kuwa sina sifa za kuendelea kuwa sehemu ya timu ya Clouds Fm. Sasa basi, hebu tuangalie makosa niliyoyafanya mimi pamoja na Fina.

Tarehe 29th May 2008, kwa pamoja, mimi na Fina tuliamua tusiingie kwenye kipindi kuonyesha kutoridhishwa na utendaji wa baadhi ya wenzetu. Kama kuna waliosikia, siku moja kabla yaani tarehe 28th May tulifanya mahojiano na Balozi wa Marekani nchini Tanzania.Bahati mbaya (kwa sababu ambazo zilikuwa ndani ya uwezo wa Technical Department) mahojiano yale hayakusikika vizuri, yalisikika vibaya mno!!! Na hata vifaa pia havikuwa timilifu, mfano mmoja mdogo tu ni kwamba tulikuwa tunatumia mic moja.Yaani watangazaji watatu na balozi, kwangu ilinipa wakati mgumu sana hasa ikizingatiwa taarifa za interview zilipatikana karibu wiki nzima.Nilitegemea wenzetu wangejiandaa kwa kila kitu. Kwa kifupi watu wa technical walikuwa na uwezo wa kusema kwamba interview isingewezekana kutokana na ufinyu wa signal na vifaa, TUNGEAHIRISHA.Makosa kama haya yamekuwa yakijirudiarudia mara kwa mara na ndio maana nasi tukaamua kuweka msisitizo kwa njia ile ya kugoma.

Najua kuna watakaojiuliza, hapa Gerald anaingia wapi, kwa sababu alisikika wakati wa mahojiano na balozi, akayapata madhira lakini hakugoma. Hilo sitolitolea maelezo nikiamini yeye mwenyewe ndiye mwenye nafasi nzuri ya kufafanua atakapotakiwa kufanya hivyo ingawa halazimiki. Ila ieleweke kwamba, kwenye mpango wa kugoma, ALIHUSISHWA NA AKAUKUBALI.

Kilichofuatia ni kutakiwa tujielezee kwa nini hatukwenda kwenye kipindi, tukajielezea, na hatimaye mimi nikapewa barua niliyoielezea hapo juu na tetesi za uhakika nilizo nazo ni kwamba mtu wa technical kapewa barua ya warning.

Kwa hiyo basi, kuondolewa kwangu hakuhusiani kabisa na suala la masilahi yaani mishahara. Kosa ni hilo hapo juu na tulilifanya kwa nia njema ya kujaribu kujenga zaidi kwa vile tunaamini Clouds inazidi kukua siku hadi siku.

Ni juu ya atakayesoma waraka huu kupima uzito wa kosa na uzito wa adhabu.Kwangu naona sawa kwa sababu si kila kinachotokea lazima kiwe na sababu za msingi. Bado mwenye mali ana mamlaka ya kuamua nani awe kwenye timu na nani asiwemo.Na ninaamini kila anayekosea lazima aadhibiwe,nami nimeadhibiwa na nimeheshimu. Maisha yanaendelea.

Namshukuru mungu na nawahakikishia wachache waliokuwa wakitusikiliza kwamba kamwe hatukuwahi kulewa sifa kwa sababu kama ni kulewa sifa tungeshagoma siku nyingi zilizopita kama suala lingekuwa ni mshahara. Kwa wenye kumbukumbu, Power Breakfast ilianza kama ‘wake up show’, enzi hizo kipindi kilikuwa kinaanza saa 11 alfajiri, maana yake ni kwamba mimi na Fina tulikuwa tunaamka saa 10 alfajiri, kwa mshahara wa kawaida kabisa na bado tuliweza kulibeba jahazi.

BC: Unawaambia nini wapenzi wasikilizaji wenu na wasikilizaji wa CloudsFm kwa ujumla?

KP: Nawaambia wasikilizaji wa Clouds na wasomaji wa Bongo Celebrity kwamba tuwe wepesi wa kukubali matokeo kama vile tunavyoweza kukikubali kifo kinapotutenganisha na wapendwa na tunaowachukia.Pia tuweze kukubali kwamba kila kitu kinajengwa taratibu. Hata waliobaki powerbreakfast wana vipaji na uwezo wa kukipeleka juu zaidi, kikubwa kinachohitajika ni subira yenu mnaowasikiliza, msijaribu kuwalinganisha wala kutafutia makosa. Mwisho wa siku mtazoea na mtafurahia.

Kwa upande wangu, napumzika kidogo, naelekeza nguvu zaidi kwenye katuni na kabiashara kangu kadogo. Pengine wakati umefika wa kuwekeza zaidi kwenye haka kabiashara.

Mwisho kabisa nawaomba radhi wale ntakaokuwa nimewakwaza kwa kuyaanika haya, ila kwangu ni kwa faida zaidi kwani ninapochora katuni nategemea wasomaji zaidi ambao ni watu, na ninapokuwa mmachinga wa nguo nategemea watu pia.Hivyo basi bila UFAFANUZI ni rahisi kwa watu hao ambao ni wasomaji wa katuni na wanunuzi wa nguo zangu kunishusha thamani kwa kudhani tumeacha Clouds kutokana na kudhani tumeshakuwa wakubwa hivyo basi tumeanza kuringa. LA HASHA!!!SIKUACHA CLOUDS, NIMETIMULIWA (nahofia kuuzungumzia mkataba wa Fina kwa kuwa una mambo yake haswa upande wa kisheria) NA SIJAPATA KAZI,ILA NINATAFUTA KAZI ILI WANANGU WAENDELEE KWENDA CHOONI. WALA SIJACHUKULIWA NA TBC, KWANZA UTUKUFU WALIONAO ZE COMEDY HATA ROBO SIJAUFIKIA.

Laiti nisingekuta mjadala kwenye blog ya Michuzi wenye kulaumu, kuponda kutoa pole na kutia moyo, kamwe nisingeyasema haya.Naomba kuwasilisha.
 
mie nampongeza kwa ku muv one step forward n hata the way alivyojibu maswali yaani yashow kabsaa huyu mtu ka mature katika nyanja yake......wala hashow chuki na mtu well done masoud riziki popote ndugu yangu chA msingi kama ulivyosema watoto waende chooni!!!
 
Ofcourse sasa kipindi kinaboa mno. Mie nilikuwa msikilizaji mzuri sana. Sasa hivi nabadilisha kila idhaa muda huo. Gerald kwa uzoefu wake, apaswa atumie muda mwingi kwenye kipindi, kwani yeye huja wakati wa kubarizi na kudadisi magazeti tu. tumechoka na miziki wanayopiga kila wakati (hakuna la kuongelea???). Ingawa hata alipobaki Fina peke yake, masoud sijui alienda wapi.... naye akawa anaboa!! Nadhani kile ni kipindi cha kuendeshwa na watu wawili au watatu. Kile kilikuwa kipindi cha kuacha watu midomo wazi. Anyway tuwape wiki au hata mwezi. Waache uoga na waonyeshe ukomavu na uelewa wa mambo kama wale partners.
 
yupo Gerald Hando Na Paul James...wanaboa Haooooooo!!!!! Afadhali Kidogo Gerald Ana Kauzoefu Ka Kukaa Na Wale Wawili Lakini Paulo Kama Wanavyomuita! Mhhh! Safari Pevu!

I Dont Think Wanaboa, Its Just A New Thing... Kama Mnakumbuka Wakati Wanaanza Fina Alikua Worse But We Got Used To It And I Hope Pj Will Improve. Either Way I Am Happy Masoud Accepted That His Future Lies Elsewhere, Mtafuteni Fina Jamani
 
Jamani! hili swali nilitaka kuliuliza mda si mrefu,kwani mara ya mwisho kuwasikia wawili hawa ni pale walipokuwa Ubalozi wa Marekani wakifanya mahojiano na Balozi wa Amerika,I thought labda wameamua kuzamia kwa kujificha Ubalozini..kwani toka siku ile hawakusikika tena,Sasa hizi habari zenu za kuwa wameacha kazi kwa ajili ya maneno ya watu siwezi kuwaamini Wana Jf kwani wale vijana ndo future yao na Pia Clouds hawawezi kukubali kuwapoteza..Ila hili la uhusiano may be....manake walikuwa karibu mno...pengine mambo ya TBC labda yamewafika....manake TBC waenifurahisha kwa kummaliza Kidomodomo Tajiri mmoja wa kichaga ambaye anadhani kila kitu Bora aweza kukifanya yeye by hook or Crook ili mradi aonekane mwema kwa watu...
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom