Massanza: Simba ni tawi la Yanga

Labani og

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2020
Posts
19,637
Reaction score
29,473
SIMBA NI YANGA B

Baada ya kikosi cha Simba Sc, kuruhusu kichapo cha mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya mtani wake Yanga Sc, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza ameibuka na kusema kuwa ni rasmi kuwa watanzania na wanasoka watakua wameitambua Yanga B kwenye soka la ‘bongo’ ni timu gani.

Massanza amesema kuwa kumekuwa na kauli nyingi zinazosema kuwa Singida FG ni Yanga B kila wanapopoteza mchezo dhidi ya Yanga hivyo ameeleza kuwa Simba nayo imepoteza mchezao kwa goli nyingi ambazo wao kama Singida hawajahi kufungwa na Yanga hivyo basi Simba ndiyo Yanga B.

“Sasa nadhani Yanga B mmeiona, sisi huwa tunasingiziwa tu, maana tukipoteza mchezo dhidi ya Yanga tunaitwa Yanga B, je hawa waliopoteza kwa idadi ya goli 5-1 tuwaite vipi?,” amesema Massanza.

Hamsa [emoji113] 5 G
 
Jana ndio nimeongea nao wengi, juzi sikuwatafuta. Wengi wanakiri hawakulala, kila wakikumbuka ni goli tano usingizi unapotea!
Yanga walimwaga maji ya BAHARI kila Kona ya uwanja na kumwaga kwenye dimba ilikuwa kazi ya kocha, haribu uchawi wote wa walinda uwanja.
 
Fanyeni kazi, inamaana mpaka leo bado mnaongelea hilo?
Kwanza mpira dhambi
 
Mkuu, michuano ile ilipangwa mapema. Laiti kama wangesubiri mpaka tulipocheza fainali CAFCC tungeenda sisi na tusingeishia pale.
Inawezekana pia walimchukua kolo....kama pazia la kumpitishia Al ahly [emoji23]
 
SIMBA NI YANGA B

Baada ya kikosi cha Simba Sc, kuruhusu kichapo cha mabao 5-1 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya mtani wake Yanga Sc, Afisa Habari wa Singida Fountain Gate, Hussein Massanza ameibuka...
Au hao Simba na wenyewe watuambie kama walipokea bahasha kutoka GSM, au la.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…