Kati ya hiyo massey na ford. Zote ni imara sana, ila chukua massey. Kwa Tanzania na kwa sisi wakulima wadogo tukitaka kununua trekta lazima tuangalie uimara ikifuatiwa na upatikanaji wa spare afu ndo yatakuja mambo mengine. Spare za trekta ni ghali bila kujali ni ya kampuni ipi(natumaini umejipanga kwa hilo), ila za massey ni rahisi kuzipata kuliko za hiyo ford. Ila kama unataka uonekane unamiliki trekta la gharama basi chukua ford. Massey likiharibika katikati ya msimu wa kulima linaweza kupona ndani ya siku 2 tu maana unapanda bodaboda au basi fasta unaingia dukani unarudi na spare. Ila ford ikiharibika katikati ya msimu wa kulima, upatikanaji wa spare unaweza kupanda ndege kufuata[emoji16] au kuingia alibaba, amazon na ebay kuitafuta(hapa namaanisha spare za ford ni ngumu kupatikana kidogo ndani ya Tz japo zinapatikana). Na kumbuka msimu wa kulima haukusubiri kamwe. Mwisho, trekta ni matunzo kama unavyoitunza gari yako au pikipiki kwa kumwaga oil kwa wakati, kubadili filters, coolant na mengineyo. Ukilitunza litakutunza.