Mastaa kumfungia kazi Mpoki kwa udhalilishaji

Mastaa kumfungia kazi Mpoki kwa udhalilishaji

msafwa93

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2011
Posts
4,786
Reaction score
5,963
KIMENUKA! Komediani aliyebahatika kuwa maarufu Bongo, Mujuni Silvery 'Mpoki' yuko njiani kupandishwa kizimbani kufuatia mastaa waliodai aliwadhalilisha usiku wa Tuzo za Kili kucharuka na kwenda kwa mwanasheria wao, Ijumaa Wikienda lina ishu nzima.
Mujuni Silvery 'Mpoki'.
Kwa mujibu wa chanzo makini, mastaa wanaodaiwa kutinga kwa mwanasheria na kuandikisha maelezo ni hawa wafuatao: Mkurugenzi wa Aset Club inayomiliki Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Asha Baraka, mtangazaji wa runinga, Maimartha Jesse, Meneja wa Wema Sepetu, Martin Kadinda na staa wa filamu za Bongo, Vincent Kigosi ‘Ray’.
Aisha Mashauzi.
Wengine ni Mbongo Fleva na mtangazaji, Vanessa Mdee, Miss Tanzania 2006, Wema Sepetu, Aisha Ramadhani ‘Mashauzi’, Maria Sarungi na DJ Bonny Love. WADAI KUDHALILISHWA BILA KUPEWA NAFASI
Chanzo kilisema kwamba siku ya Tuzo za Kili, Mpoki akiwa MC wa shughuli hiyo, aliwadhalilisha kwa kutangaza ndani ya hadhara iliyohudhuria kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar, mambo ambayo wenyewe hawakupata nafasi ya kujitetea (balansi).
Asha Baraka.
“Kule kwa mwanasheria wao, wote walidai kuwa, siku ile Mlimani City, Mpoki alikuwa akitangaza mambo yao, mengine ya siri, mengine si ya kweli, mengine ya udhalilishaji bila wao kupewa nafasi ya kujitetea kama mnavyofanya magazetini. “Wenyewe wanajua Mpoki hakutumwa na Kili kusema maneno yale bali aliamua yeye kama yeye tu. Ndiyo maana wameamua kushughulika na Mpoki na si mwingine,” kilisema chanzo hicho. Maimartha wa Jesse. MADAI YAO YA MSINGI
Chanzo kiliendelea kutiririka kwamba madai ya msingi ya mastaa hao- kisheria ni kudhalilishwa, kuzushiwa na kuchafuliwa mbele za watu, jambo ambalo liliwapa usumbufu mbele za jamaa zao, wakiwemo watoto na ndugu wengine waliokuwa wakifuatilia sherehe za utoaji wa tuzo hizo kubwa kuliko zote Afrika Mashariki. KASHFA ZENYEWE KWA UFUPI
Ili gazeti hili lisijiingize kwenye malalamiko ya mastaa hao linayaandika maneno hayo kwa ufupi sana lakini yenye kueleweka. MAI; aliambiwa amezipiga jeki nido ilhali ana mtoto.
ASHA; aliambiwa kwa usiku huo alipendeza sana (make up) lakini akionekana kesho yake anaweza kupewa shikamoo kwa mabadiliko ya mwonekano. RAY; aliambiwa siku hizi amebadilika rangi, si kama zamani. Pia Mpoki alimwambia amesikia ameachana na Johari na yuko na Chuchu Hans.
Wema.
KADINDA; alimwambia anamuona anakwenda kumpa tuzo shemeji yake (Diamond)...
WEMA; alimuuliza ni kwa nini kila siku kwenye Instagram anatupia picha akiwa anakula mayai tu, anataka watu wamwelewe vipi! VANESSA; alimwambia afanye mazoezi ya kutembela viatu vyenye visigino (na mengine ambayo si vyema kuyaandika hapa).
-
WIKIENDA LAWASAKA--
Baada ya madai hayo, gazeti hili liliwasaka mastaa hao mmojammoja ili kusikia ukweli wa madai hayo.
Ijumaa Wikienda lilianza kwa kumsaka Kadinda juzi ambapo simu yake haikuwa ikipatikana hewani kama alivyozoeleka. Kwa upande wake Ray alikiri kuwepo kwa uwezekano wa kumshitaki kwa kuwa ni kweli alimdhalilisha mbele ya kadamnasi. Naye Mai alipotafutwa aliwaka akidai kuwa alichokifanya Mpoki hakikuwa sahihi kisheria hivyo jambo hilo lipo.
Ray Kigosi.
Kwa upande wake, Isha Mashauzi alisema kuwa labda wenzake wameamua kumshtaki Mpoki lakini hawakuwa wamemjulisha. Mastaa wengine ambao simu zao ziliita bila kupokelewa ni Asha Baraka, Vanessa, Wema na DJ Bonny Love.
-
MSIKIE MPOKI
Mpoki alipopigiwa simu na kuelezwa kuhusu malalamiko ya mastaa hao, katika hali ya kushangaza alisema hakumbuki nini kilitokea siku hiyo. “Kusema ule ukweli mimi sikumbuki chochote kile kilichotokea siku ile, we- nitajie majina ya hao watu niwapigie halafu baadaye ndiyo tutaongea,” alisema Mpoki akiweka sharti hilo wakati yeye ndiye aliyekuwa akiwananga jukwaani.
Martin Kadinda.
ATUMA MESEJI YA HASARA!
Katika hali isiyokuwa ya kawaida, Mpoki baada ya kupigiwa simu saa saba alasiri na kujibu hivyo, usiku wa saa mbili alituma meseji kwa mwandishi iliyosomeka:
“Hapo ndipo uwezo wako wa kufikiri ulipoishia? Sijui lini mtafika kikomo cha kuwa watumwa wa ujinga… Nisichokijua hakiwezi kunisumbua...”
-
AKIKUTWA NA HATIA KISHERIA
Kwa mujibu wa mwanasheria mmoja (jina tunalo) aliyezungumza nasi, endapo Mpoki akipanda mahakamani na kukutwa na hatia, anaweza kufungwa kifungo cha miaka 5 jela au faini kulingana na uzito wa udhalilishaji huo kwa mujibu wa walalamikaji.
 
Labda wana'sheria' watusaidie...kama mtu anafahamika kuwa ni 'comedian', na akawatania watu (inawezekana ikawa matani ya kweli) wakati akifanya kazi zake kama 'comedian' (maana japo ilikuwa ni event ya tuzo za kitaifa, Mpoki alialikwa kuendesha sherehe kama comedian ili watu wasiboreke)...je, anaweza kushitakiwa kwa kutimiza wajibu wake!?
 
Habari yenyewe imeshusha mlegezo full kuchanganyana
wahusika mliowapigia sim hawapatikan na wengine wanadai hawana taarifa kuhusu kumshtaki MPOKI
hapohapo mnadai waliodharirishwa wamecharuka na kwenda mahakaman
kama hakuna hata mmoja aliyethibitisha , ninyi hizi taarifa mmezitoa wapi?
 
Na ashitakiwe tu, alizidi naye kushambulia watu.
 
Waache kumstaki Shigongo anayewaanika kila siku (na matani mengi ya Mpoki yametokea huko) waende kwa Mpoki? akili za matope tu hizi......
 
Hayo walioandika yoote yameanzia wanayaandika kilasiku kwenye magazeti yao na hawashtakiwa itakua yule aliokua anesema kasikia na mengine ni kweli yalitokea? Sasa kama vanessa mdee kuanguka na viatu vyake virefu na kuambiwa afanyie mazoezi ya kutembea navyo nae kaenda kushtaki?
 
On the one hand nilisema kwamba Mpoki alivuka mpaka.

On the other, kumshitaki mtu mwenye "artistic license" ku act the fool, ni kuwa fool. Hususan kwa sababu wengine wanaotaka kumshitaki kasema vitu ambavyo si kashfa kabisa (kwa mfano Vanessa Mdee na viatu vya mchuchumio, kiingereza, etc).

Kama mtu ninayependa uhuru wa kujieleza, na kuchukulia kila kitu kwa context yake, ningependa kuona hili halipelekwi mahakamani.

If anything ma star wanaweza kumlipizia Mpoki kwenye sana zao husika wananchi tuendelee kucheka.

If anything naona Kilimanjaro wana share kubwa ya lawama kwa kutotoa muongozo kuhusu shughuli iendaje.
 
On the other, kumshitaki mtu mwenye "artistic license" ku act the fool, ni kuwa fool. Hususan kwa sababu wengine wanaotaka kumshitaki kasema vitu ambavyo si kashfa kabisa (kwa mfano Vanessa Mdee na viatu vya mchuchumio, kiingereza, etc).

Hiyo "artistic license" bongo inaeleweka kweli?

(That's how low my expectations are with bongo and its people)
 
Khah, kumbe gazeti lenyewe ni Ijumaa Wikienda? No comment!!!!


Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
Hiyo "artistic license" bongo inaeleweka kweli?

(That's how low my expectations are with bongo and its people)

Hahaha, kama haieleweki ni kazi ya JF kueleweshana, wengine wanaweza hata kui google, ikiwa watataka.

Kuna siku Seth McFarlane ali host Oscars, akachemka kichizi kwa kutoa overly inappropriate jokes about women.

Watu wakamchambua na kumchamba, zikaandikwa articles kibao kumsema vibaya, watu wakasema mfumodume, kutoweza kwake kuchekesha bila kuoffend wanawake etc etc.

Lakini sijaona habari ya kutaka kumshitaki. Kwa sababu mtu yeyote anayejua sheria na ethos za Kinyamwezi atajua kwamba hapo mtu akishtakiwa anataja "First Amendment" kesi inatupiliwa mbali.

Comedians wana kazi ngumu, mfano.wa Seth McFarlane unaonyesha kazi hii ya ku.host si ngumu bongo tu ambako bado tunaandika taratibu zetu, bali hata Hollywood they don't necessarily get it right always. Comedians wanahitaji kuwa werevu kweli, ikiwa pamoja na kujisomea sana. On the one hand wanatakiwa ku push tge envelope of being funny kwa kuwa provocative, on the other wanatakiwa kutovuka mipaka ya acceptability.

There is a thin line between funny and offensive, especially if the audience is as diverse as the one in Taanzania and tge rules are still being written.

By the way, Seth ame ji redeem vizuri kwangu kwa kutuletea science series nzuri sana ya "Cosmos: A Space Time Odyssey" pamoja na Neil DeGrasse Tyson. Inanikumbusha ile original ya Carl Sagan. Inafaa sana kuamsha interest ya watoto kwenye sayansi na kufundisha hata sisi wakubwa.

Labda Mpoki anachotakiwa kufanya ili upepo huu upite ni kutoa kazi iliyo nzuri na relevant.

Kwa wanaotaka kusoma zaidi kuhusu epic fail ya Seth McFarlane ona

http://www.today.com/entertainment/...arlane-oscar-lines-include-fat-joke-1C8539124
 
Labda Mpoki anachotakiwa kufanya ili upepo huu upite ni kutoa kazi ikiyo nzuri na relevant

Mi naona wala hahitaji kufanya chochote maana kwa ujumla tuko wasahaulifu sana. Akikaa kimya huo upepo utapita tu.
 
Tanzania na magazeti ya shigongo yatatuharibu sana
 
Back
Top Bottom