Mastaa saba Yanga hatarini kusugua benchi.

Mastaa saba Yanga hatarini kusugua benchi.

Hearten

Member
Joined
May 17, 2016
Posts
46
Reaction score
54
pic+yanga.jpg

Dar es Salaam. Wachezaji saba wa Yanga wamejiweka kwenye nafasi ngumu ya kupata namba katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, ugenini dhidi ya Township Rollers ya Botswana, wiki ijayo.

Kiwango kisichoridhisha na ufanisi mdogo wa wachezaji hao kwenye mechi za hivi karibuni zile za kirafiki, vinaweza kuwakaanga na kujikuta wakisotea benchi. Na si mechi hiyo tu, bali hata zile za mashindano mengine wanaweza kujikuta wakikosa namba.

Wachezaji hao ni beki Ally Ally; viungo Feisal Salum, Abdulaziz Makame, Deus Kaseke na Raphael Daud pamoja na washambuliaji Maybin Kalengo na David Molinga.

Makosa ya washambuliaji Molinga na Kalengo kushindwa kutumia nafasi ambazo Yanga ilitengeneza na pia hata wao wenyewe kutopika mabao kwa wengine, vinawaweka kwenye wakati mgumu kuwapora nafasi Juma Balinya na Sadney Urikhobi.

Katika mechi zote za kirafiki ambazo zimeonekana kuwa za ushindani, Kalengo na Molinga wameshindwa kupachika mabao.

Pia hali inaweza kuwa tete kwa viungo Kaseke, Makame, Feisal na Daud kutokana na kushindwa kutimiza vyema majukumu yao kwenye safu hiyo ambayo ni kiunganishi cha timu kinachotengeza nafasi za mabao.

Kukosa ubunifu na kutengeneza muunganiko wa kitimu utawapa kazi ya ziada kulishawishi benchi la ufundi kuwapatia nafasi mbele ya Mapinduzi Balama, Patrick Sibomana, Pappy Tshishimbi na Mohamed Issah ‘Banka’.

Mwanaspoti
 
Molinga ka hecheza mechi tatu tu na hakuanza.
Bado Nina Imani na Molinga, huyo Mnamibia na Balinya wamefanya Nini cha maana
 
Huyu makame tuliambiwa ni mtu hatari sana

Huyu kalengo tuliambiwa ni balaaaaa

Falcao molinga tuliambiwa tutamsahau makamboo
 
bado mapema sana kuwalaumu wachezaji, subirini ligi iishe ndio muwalaumu, hakuna timu isiyofungwa hata barcelona juzi kafungwa
 
Yaani hata ligi tu haijaanza! Ni mapema sana kuwahukumu. Ligi itakapo changanya itakua rahisi kuwatathmini. Ila kwa sasa siungi mkono hoja.
 
Hawa Mwanaspoti ni vilaza Sana. Hivi kwa mtu unayejua mpira unapata wapi uthubutu wa hata kumlinganisha huyu Banka na huyu Balama na Feisal. Mpira anaocheza Banka kila mtu anaweza kuucheza, pasi za kulia na kushoto! Banka hapiga pasi hata moja ya hatari, Banka hana driving capacity, Banka hawezi kupora mipira, huyu Balama ndiyo kabisa anakimbia kimbia tu.
Mechi ya Jana Feisal alivoingia zilianza kupigwa pasi zenye macho, forcing ikawa kubwa, objective football ikaonekana.
Kama Kuna watu watamfanya Zahera Afukuzwe basi ni Balama, Mohamed Banka na All Sonso, aendelee kuwangangania!
 
Wakulaumiwa Zahera..kikosi Cha Kwanza wameondoka..Makambo,Ajibu ,Kindoki na Gadiel..alitakiwa wachezaji wanne tu wapya ndio wazibe hayo mapengo..alafu wengine wapiganie namba..Nimemuelewa kocha wa mikia mchezaji mpya mwenye uhakika wa kuanza ni Shiboub tu..
 
Wakulaumiwa Zahera..kikosi Cha Kwanza wameondoka..Makambo,Ajibu ,Kindoki na Gadiel..alitakiwa wachezaji wanne tu wapya ndio wazibe hayo mapengo..alafu wengine wapiganie namba..Nimemuelewa kocha wa mikia mchezaji mpya mwenye uhakika wa kuanza ni Shiboub tu..
Wewe kuna wachezaji wengi tu pale simba wa kuanza
Kahata huyu ni mara mia ya washambuluaji wenu hao
Deo kanda anaujua mpira hadi tumeanza kumsahau okwi.
Siyo mtuletee habari za akina molinga kukimbia utadhani anefungiwa fuko la mchanga miguuni
 
Wewe kuna wachezaji wengi tu pale simba wa kuanza
Kahata huyu ni mara mia ya washambuluaji wenu hao
Deo kanda anaujua mpira hadi tumeanza kumsahau okwi.
Siyo mtuletee habari za akina molinga kukimbia utadhani anefungiwa fuko la mchanga miguuni
Mkuu huyu amesema mwenye uhakika shiboub akiwa na maana ndani ya Simba wengine wote wanazipigania wenyewe kwa wenyewe
Kahata-Ajib-Chama
Mkude-Fraga-Mzamiru-Ndemla
Manula-kakolanya
Kanda-wilker-Dilunga-
Tairone-nyoni-wawa-kenned
Tshabalala-Gadiel
Shamte-kapombe

Me ndio nimemuelewa kwa pigo hizo mzee
 
Back
Top Bottom