Kanungila Karim
JF-Expert Member
- Apr 29, 2016
- 20,743
- 25,564
HIVI karibuni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imecharuka. Imekuwa ikiwachukulia hatua baadhi ya mastaa mbalimbali ambao wamekuwa wakienda kinyume na maadili ya Kitanzania kwa kutupia picha zisizo na maadili kwenye kurasa zao katika mitandao ya kijamii na hatimaye wengine kufungiwa kabisa. Mwaka huu baadhi ya wasanii hao ambao wengi wana majina makubwa na wanapendwa kwenye jamii walipewa adhabu mbalimbali ikiwa ni sehemu ya kuwafundisha na kuwarekebisha juu ya namna ya kutumia mitandao ya kijamii vizuri. Wapo wengine walioonja mahabusu na hata kupelekwa mahakamani.
WEMA SEPETU
Staa huyu alikumbana na misukosuko baada ya kuposti picha na video akiwa kwenye mahaba mazito na mwanaume aliyedai kuwa ni mchumba’ke, Patrick Christopher ‘PCK’. Baadaye zilivuja picha zao nyingine zikiwaonesha wakifanya mambo ambayo siyo ya kimaadili. Mwisho wake staa huyo aliitwa na Bodi ya Filamu na kufungiwa kujihusisha na mambo ya filamu kwa kipindi kisichojulikana hadi atakaporuhusiwa huku kesi yake hiyo ikiendelea kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar.
FAUSTINA CHARLES ‘NANDY’
Mwanamuziki huyu wa Bongo Fleva aliwashtua wengi baada ya video yake kuvuja akiwa na mwanamuziki mwenzake, William Lyimo ‘Billnas’ wakifanya mambo ya chumbani, jambo ambalo liliwafanya kupoteza dira zao, lakini pia TCRA iliwaita na kuwapa onyo huku wakitakiwa kuomba radhi hadharani kutokana na kitendo hicho.
NASCAT ABUBAKARY ‘AMBER RUTTY’

Huyu alijipachika kazi ya uanamitindo na msanii wa muziki ingawa watu wengi walikuwa hawamjui. Alianza kufahamika baada ya video yake ya ngono na mwanaume wake aliyekuwa akiishi naye kuvuja kila kona na hatimaye kutiwa mbaroni na mpaka sasa yeye na mwenza wake kutolewa nyuma ya nondo za mahabusu kwenye Gereza la Segerea baada ya kupata dhamana ya shilingi milioni 15 kila mmoja.
GIFT STANFORD ‘GIGY MONEY’
Awali msanii huyu wa Bongo Fleva alikuwa video queen. Baadaye alijiingiza kwenye muziki wa Bongo Fleva. Kufuatia tabia yake ya kusambaza picha na video chafu aliitwa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) kwa ajili ya wimbo wake wa Nampa Papa kuwa moja ya nyimbo zisizokuwa na maadili ambapo wimbo huo ulifungiwa jumla hadi leo kutokana na video yake kukosa maadili.
SUZAN MICHAEL ‘PRETTY KIND’
Baada ya kurejea nchini akitokea India, mrembo huyu aliamua kujiingiza kwenye muziki wa Bongo Fleva ambapo wimbo wake wa kwanza alimshirikisha Gigy Money unaoitwa Vidudu Washa, lakini wimbo huo ulipigwa marufuku kisha alifungiwa kufanya muziki kwa muda wa miezi sita.
FAIDHA OMARY ‘SISTER FEY’
Msanii huyu awali alikuwa ni mwigizaji wa filamu za Kibongo. Baadaye aliona uigizaji haumpi kipato hivyo aliamua kuanza kujirekodi video mbalimbali za kuelimisha wanawake jinsi ya kukaa na waume zao kisha kutupia mitandaoni. Baadaye aliibuka na mpenzi aitwaye John Njau ‘All Star’, wakawa wanajirekodi video mbalimbali ambazo hazikuwa na maadili mpaka waliposhtakiwa na mamlaka husika ambapo waliwekwa lupango na walipotoka walipewa masharti ya kutoweka tena picha zisizo na maadili kwenye mitandao ya kijamii.
FAIZA ALLY
Huyu alijulikana zaidi baada ya kuzaa na Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’. Alijulikana pia kwa mavazi yake ambayo yalikuwa hayafanani na ya mtu mzima hasa pale alipovaa ‘pempasi’ kwenye bethidei yake.
Baada ya kujiingiza kwenye uigizaji, Faiza alionja mahabusu kufuatia kuitwa Kituo cha Kati cha Polisi jijini Dar baada ya kutupia picha zisizokuwa na maadili kwenye mtandao muda mfupi akiwa ametoka kujifungua. Mpaka leo simu yake aliyoitumia kujipiga picha hizo ipo Polisi.
IRENE UWOYA
Mwanamama huyu maarufu kwenye tasnia ya filamu, aliitwa na Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ‘TCRA’ na kupewa onyo kali la mwisho ikiwa ni baada ya kuposti picha ya nusu utupu kwenye ukurasa wake wa Instagram kinyume na maudhui ya mtandao. Sambamba na onyo hilo, alitakiwa kuomba msamaha kupitia ukurasa wake huo na kweli akatii maagizo hayo.
HAMISA MOBETO
Mwanamitindo huyu maarufu aliitwa pamoja na Uwoya na TCRA kwa kosa la kuweka picha za nusu utupu mitandaoni. Katika uamuzi yake, TCRA ilimtaka Hamisa kuweka tangazo kwenye ukurasa wake wa Instagram la kuwaomba msamaha Watanzania na kuwataka kutosambaza picha zake za nusu utupu. Hamisa alitii agizo hilo na kuahidi kwamba hatarudia tena.