Kikosi cha mastaa zaidi ya 10 kutoka Kabila la Wangoni kinatarajiwa kuonekana jukwaani siku ya Wakunyumba Traditional Party, wote wakiwa masupa staa wa sanaa mbalimbali.
Kwa mujibu wa muandaaji wa sherehe hiyo, Lucy Francis Komba, mastaa hao wanafanya vizuri katika tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, filamu na tamthiliya, muziki wa dansi na wa Injili, mashahiri, vichekesho na siasa. Na lengo ni kuinyesha watanzania ni jinsi gani wangoni wakiamua kuingia kwenye sanaa wanafanya kweli na vipaji vyao viko kwenye damu.
Lucy alisema kuwa, mastaa hao wameshapelekewa mwaliko maalum kwa lengo la kuwajenga kifikra katika hatua ya kuifikia Agosti 14, 2026 ambayo itakuwa siku ya Ijumaa.
Lucy aliwataja mastaa hao kuwa ni: Luiza Nyoni Mbutu ambaye anatokea kwenye muziki wa dansi akihudumu katika Bendi ya The African Stars 'Twangapepeta' na Joseph Leonard Haule "Profesa Jay' anayetumikia muziki wa Bongo Fleva na Hip Hop.
Wengine ni; Shamila Rashid Ndwangila 'Bi. Star' ambaye ni nyota wa maigizo Bongo. Kwa sasa anavuma kwenye Tamthiliya ya Kombolela akiitwa Mwadawa Kikala na Cosmas Thobias Chidumule yeye kwa sasa anaimba nyimbo za Injili baada ya kustaafu muziki wa dansi na kuokoka.
Aidha, atakuwepo Jokate Urban Mwegelo aliyepata kuwa mlimbwende wa Miss Tanzania, baadaye kuingia kwenye siasa akitumikia nafasi ya Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Pwani na Korogwe, Tanga na kisha Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana ya Chama cha Mapinduzi (CCM).
Wengine ni Andrew Ngonyani au 'Brother K.' ambaye amejipatia umaarufu kwa uchekeshaji kupitia Futuhi ya Televisheni ya Star (Star Tv), Dickson Samson Makwaya 'Bambo' akitokea kwenye jukwaa la uchekesheji nchini.
Sherehe hiyo haitawakosa Mrisho Issa Mpoto ambaye ni mghani mashahiri maarufu nchini, Joseph Osmundi Mbilinyi 'Sugu' staa wa muziki wa Hip Hop na Chrissant Muhenga akisifika kwa kazi ya mtayarishaji na mwongozaji maarufu wa filamu na vipindi mbalimbali vya Tv nchini.
Angel John, Komba, Rose Ndauka, Produce C9 Kanjenje, Producer Mr. T.
Lucy alisisitiza kuwa, wote wamepelekewa barua rasmi za mwaliko kinachosibiriwa ni Ijumaa ya tarehe 14, Agosti, 2026 kuanzia saa 10 jioni na kuendelea.
Wakunyumba Traditional Party imeandaliwa na Taasisi ya Mwendo wa Saa Production (MSP) ikiwa na lengo la kutangaza na kukumbusha tamaduni, desturi na mila za kabila la Wangoni ambalo linapatikana Mkoa wa Ruvuma uliyopo Kusini mwa Tanzania.
Mkurugenzi wa Mwendo wa Saa Production ni Lucy Francis Komba ambaye ni mwigizaji, mwongozaji na mtayarishaji wa filamu nchini. Kwa sasa anaishi nchini Denmark baada ya kuolewa kwa ndoa na Mdenmark.