Mastaa wenye mvuto zaidi kwenye Jamii

warumi

R I P
Joined
May 6, 2013
Posts
16,218
Reaction score
18,440
Ukiachilia mbali wingi wa wasanii wanaofanya vizuri kwenye tasnia mbali mbali apa bongo, sio wote wanaobahatika kukubalika na kupokelewa vizuri na Jamii/mashabiki. Hawa ndio wasanii wenye mvuto zaidi na wanaoongoza kwa kupendwa na mashabiki.

1.DIamond platinum
Anaweza akawa sio muimbaji mzuri kama Alikiba au barnaba, ila haina ubishi huyu ndiye msanii wa kiume kwa upande wa bongo fleva anayeongoza kwa kupendwa zaidi na mashabiki, jina lake linazidi kukua siku hadi siku na kazi zake zinafanya vizur karibia east Africa nzima.

2. Wema sepetu
Sio muigizaji mzuri kumshinda Johari, wala hana filamu nyingi sokoni kuliko Irene uwoya, ndio maana hata waandaji wa tunzo za filamu hawajawahi kum nominate hata kwenye category ya msanii chipukizi bora, hiyo haijafanya jina lake lishuke kwenye Tasnia hiyo, Bado haina ubishi wema ana nyota Kali na anapendwa kuliko msanii yeyote. mwenyewe anajiita ENDLESS FAME.

3. LADY JAYDEE
Kiuno chake kina mfupa, hana mauno makali kumzidi Snura mushi, sauti yake nzuri na kipaji cha pekee alichobarikiwa kimemfanya apendwe zaidi na mashabiki kibao. Unadhani ana pesa sana kuliko ruge? Hakustahili kabisa kushindana naye , ila jeuri ya mashabiki aliyonao ilimfanya ajione malkia , nadhan unakumbuka Team anaconda ilifanya nini pale Nyumbani Lounge. Jide ana nyota Kali sana.

4. JB
Kipaji chake hakikumfikia marehemu kanumba(r.I.p),sio director mzuri kama Jackson kibirigi, ubunifu alionao kwenye filamu zake umemfanya apendwe zaidi na mashabiki kuliko msanii yeyote wa kiume kwa upande wa filamu apa bongo.

5.Lulu Michael
Hajawahi kuigiza vizuri kama Diana kimaro(Danija,Kigodoro) ila ana nyota nzuri sana, licha ya umri mdogo alionao , anapendwa na ana mashabiki wengi zaidi.

6.Monalisa
Hana umbo kama masogange, kipaji cha kipekee alichonacho na umakini alionao kwenye uigizaji umemfanya ajiongezee mashabiki wengi zaidi.

7. Ray kigosi
Sio muigizaji mzuri kumshinda Gabo, kampuni makini aliyonayo na aina ya waigizaji anaowatumia imemfanya kazi zake zinunuliwe zaidi kuliko kampuni yeyote apa bongo. Steps ilishawahi kusema kuhusu kazi za waigizaji zinazonunuliwa kama njugu, ray alishika namba mbili akitanguliwa na kanumba.

8.Johari
Hana swagger kama wema sepetu, kazi zake na umakini alionao kwenye uigizaji , vimemfanya apendwe zaidi na mashabiki , ndo maana hadi Leo kazi zake zipo juu.
 
Ila bhana Rich anamzidi JB sema JB anaonekana sana kwenye screen
 

Ila ungetakiwa useme kwa mtazamo wako maana najua haujafanya utafit wowote kupata hizo data. Afu mie hao no. 7 & 8 km ndo ningekua nimeandika hii list ningewatolea mbaliii hukooooo
 
Ila ungetakiwa useme kwa mtazamo wako maana najua haujafanya utafit wowote kupata hizo data. Afu mie hao no. 7 & 8 km ndo ningekua nimeandika hii list ningewatolea mbaliii hukooooo

Hujakosea kusema kwa mujibu Wangu, Nina experience kidogo na haya mambo, mambo mengine hayahitaji kumulika na torch uone.
Hata Mimi nilisita kuwataja, ila kutokana na sababu nilizozitaja, bado RJ company inafanya vizur , na ni moja ya kampuni first class kibongo bongo, angalau wanajitahid kwa ubora kwa kias chake , na ndio maana hata STEPS iliwahi kuwapa Awards kama kampuni bora ya mwaka , na ni wazi kazi zao zinakubalika , mchango wao ni mkubwa bado nchini, ndio maana watu wengi ukimbilia kuomba kazi kwa Ray. Wanakubali na wana mvuto kwenye Jamii, nadhan namba Saba na nane zinawafaa..
 
Kwa sasa hivi Bongo msanii mwenye mvuto zaidi ni Gabo, hao wengine skendo zinawabeba.!
 
Huyo wa kwanza na wapili sema Wasanii wanaoongoza kwa scandal Diamond sio msanii mkali kupita wote Tz na wala hafahamiki sanaaaa na kujitangaza nje na kuwa na collable nyingi na wasanii wa nje kumshinda AY. Ukija kwa Sepetu ndo kabisaa ila hiyo joint venture yao na Shigongo na share zao Instagram naona zina wanufaisha sana.
 
Ukiwatoa Lady Jaydee, Diamond, Ray na Monalisa, hao wengine nimewajua kupitia Magazeti..
Ila sijawahi kuona wala kusikia kazi zao..
 
Ukiwatoa Lady Jaydee, Diamond, Ray na Monalisa, hao wengine nimewajua kupitia Magazeti..
Ila sijawahi kuona wala kusikia kazi zao..

Imetokea tu wamependwa
 
Ila ungetakiwa useme kwa mtazamo wako maana najua haujafanya utafit wowote kupata hizo data. Afu mie hao no. 7 & 8 km ndo ningekua nimeandika hii list ningewatolea mbaliii hukooooo

Tukopamoja mkuu! Ray na Johari sio wazuri. Wanalazimisha tu.

Sent from my GT-I9192 using Tapatalk
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…