Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

Master J aliniambia sijui kuimba kwenye Bongo Star Search– Harmonize

dah mkubwa mwenzangu kula tano.. kumbe unamkumbuka seleiman mbwembwe.. huyu jamaa alikua ni hatari sana kwa bongo fleva ya sasa hukuna anayemnusa kwa sauti.. pia Hassan rehani bitchuka aka stereo.. hii ni machine kubwa huyu mzee ni fundi na angekua kijana enzi hizi ndio angekua nguli wa muziki huyu mzee anajua ku-balance sauti nakiri hapa bongo kwa muziki wa kale hajawahi kutokea fundi wa muziki na mtaalam wa kubalace sauti kama huyu mzee..
Heshima kwako Mkuu. Nimemkumbuka Tx Moshi.
 
Heshima kwako Mkuu. Nimemkumbuka Tx Moshi.
RESPECT KWAKE HUYU TX MOSHI ALIKUA MTUNZI MAHIRI SANA WA MUZIKI.. KWENYE ALBAMU ZA MSONDO ZAIDI YA NUSU YA NYIMBO YEYE NDIO alikua MTUNZI, TX ndio aliipandisha msondo kileleni enzi hizo shoo zake alikua anajaza na ukichelewa nafasi hupati, MASHABIKI WALIKUA WANAPANGA LINE KUGOMBANIA NAFASI, TX alikua anakimbiza kama diamond, kiba kwa sasa, alikua anajua biashara ya muziki, alikua rafiki wa kila mtu, alipendwa na viongozi wengi wa serikalini, na ma-pedeshee wa mjini kwa kujituma kwake katika kazi, alijitahidi kutengeneza videos za nyimbo nyingi za msondo... BAADA YA TX MOSHI KUFARIKI na MSONDO NGOMA NDIO IKAPOTEA KABISA KWENYE RAMANI YA MZIKI waliobaki hawana ubunifu wowote, toka amefariki wametoa video chache sana au hawajatoa tena hata nyimbo zenyewe hawatoi tena.. KWA SASA MSONDO WANAPIGA COPY TUU NA UKIENDA KWENYE SHOO ZAO NI NYIMBO ZA TX MOSHI NDIO HUPIGWA SANA.. RIP TX MOSHI WILLIUM TANZANIIIIIA..
 
Wanafanya biashara na boss wao kawaambia lazima wafatishe vile ye anaimba. siku domo akianguka hawa wote wanaingia mtaani kuuza vyupi.
hahaha mkuu ile crew ya wasafi naikubali ila naona wanamuelemea sana mondi, sijui itakuwaje akianguka watakimbiana pale hapata tosha yani . . . maana kuna watu mle kutwa wanakesha eti wanafanya mazoezi badala ya kuingia mtaani kuangalia na fursa nyingine wawekeze
 
Mkali wa wimbo ‘Bado’ Harmonize amefunguka na kuelezea harakati zake za muziki mpaka anafika kwenye mafanikio huku akiweka wazi jinsi alivyoambiwa hajui kuimba na Master J katika shindalo la BSS.

Muimbaji huyo ambaye alishiriki shindano la BSS mwaka 2012 na Walter Chilambo kuondoka na taji hilo, amesema baada ya kuambia hajui kuimba katika shindalo hilo alijiangalia na akajikuta ni kweli alikuwa hajui kuimba.

“Hakuna kitu kibaya kwenye maisha kama kutokubaliana na matokeo, the way nilivyokuwa naimba kwenye BSS, hata mimi ningekuwa ni jaji, ningesema wewe huwezi Walter Chilambo anaweza,” alisema Harmonize. “Sikupaniki kwa sababu toka nikiwa nje Master J aliambia tangu ukiwa nje nilikwambia no, kwa Master J alinichana kabisa hajui kuimba,”

Muimbaji huyo alisema kauli hiyo haikumkatisha tamaa kwani aliendelea kupambana na kutafuta njia yakutokea.

xharmonize-bongo.jpg.pagespeed.ic.HGSijcGNBT.jpg


“Mimi nilikuwa naimani moyoni mwangu, kwamba kuna siku Watanzani wataisikia sauti yangu, japo kuwa ukimwelezea mtu mwingine mimi nakipaji hichi, naimba anasema wewe hujui, Master akaniambia wewe hujui, lakini kwa mtazamo wake alikuwa sahihi kwa sababu the way nilivyokuwa naimba hata kama ningekuwa jaji ningejitoa. Lakini mimi moyoni mwangu nilikuwa nasema ninakitu fulani, sikukata tamaa nikaendelea kufanya muziki mzuri na kweli Mungu ameniona sasa hivi nimesikika,”

Pia alisema alikuwa anahudhiria show mbalimbali ili kujifunza jinsi ya kuperfom katika matamasha mbalimbali.
kwani unajua kuimba?muone mashavu kama kambare,mkishajua kubanabana visauti vyenu basi mnajiita waimbaji,na yule mwenzenu linalomsaidia ni lile domo lake kama tarumbeta
 
Kuimba kila mtu anajua kuimba issue iko kwenye kutumbuiza wakubwa.
 
Back
Top Bottom