Master J na BSS

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Nimefuatilia Interview aliyo ifanya Master J Na Refresh Ya Wasafi FM, Kama Master J upo Humu naomba Nikwambie na Niku JUDGE kuwa Wewe huwezi kufanya INTERVIEW na Sio JUDGE Mwenye Elimu Ya Kuwa Judge like huna Maadili Ya Kazi! Sisemi Kwa Ubaya Ila Nakwambia uweze Kujirekebishaa, Hamisi Ni mshiriki ambaye yupo Kwenye 20 Bora ya Mashindano na sasa Shindano Lipo mikononi Mwa wananchi Mkiwasisitiza Wapige Kuraa Kwa Wingi kwa washiriki wanao Wapenda Ikiwa Na maana Kuwa Mmeachia Wananchi Wafanye Judgement!

Ni kweli Kabisa Hamisi Hana Kipaji kama unavyosema nakubaliana na Wewe lakini Unawezaje kwenda kwenye Interview na kuanza Kusema Maneno Ha Hovyo kama Yale kwa Mshiriki ambaye bado Yupo Kwenye Mashindano? Angekuwa Ametoka Kwenye Mashindano Sawa lakini Mshiriki bado yupo kwenye Mashindano then Unatoka Unaenda Kwenye Media Nakuanza kusema Maneno Ya hovyo hovyoo As If Mmegombana na Hamisi? What If Hamisi Akiona Hii Interview Atajisikiaje? Atapa Ujasiri Tena wa Kuimba japo Hajui? Hamisi bado ni Mtoto sana Lakini Unawezaje Kusema Maneno kama Yale kwamba Hajui like ni na nini ikiwa wewe ni Moja Ya Majudge kwenye hayo Mashindano Na Mshiriki bado yupo kwenye mashindano?

Unanifanya Niamini wale Ambao huwa wanasema BSS huwa inakuwa na Mshindi wao Tayari Toka Siku Ya Kwanza? How unaenda Kumjudge Mshiriki kwenye Media? Inamaana Zile Kula Wanazo Piga Wananchii hazima Nguvu,wala Umuhimu wowote Ule... Kwanini mnaendelea kuwatoza Pesa wananchi kwa kusema wapige kura kwa Mshiriki ambae mnajua Hata pitaaaa na hana Kipaji? Huo si ndio Wizi? Kama Mshikiri Kushinda ni Kigezo cha Kura Basii Tuseme Hamisi Ni mshindi!

Then Uache Kumuiga Sallama Kwa Kuwa hayupo kwenye Mashindano basi wewe ndio unataka uwe Yeye... Salama Atabaki kuwa Salama, Isiwe Sababu sasa Ya Wewe kila kituu kukataaa Yaani Kifupi washiriki wote waliopo kwenye Top 20 wewe uliwasemea NO na maneno kibao kisa Washiriki wakuogope wewe na Waseme kuwa Tuna Salama Mwingine! Fanya kazi kwa Uweledi na Kwa Akili!

Huwa nashangaa sana Judges Wa BSS wanavyomsema Vibayaaa mshiriki akikosea Kuimba Anasemwa As If kaiba sijui? kwanini Msijudge kwa hekima kwa Mshiriki Ambae Hajafanya Vizurii hamuoni Mashindano Makubwa kama AGT wanavyo judge? Maneno Yenu ya Kejeli mnapoteza Washiriki Wazuri kwa Kuogopa Maneno Yenu ya Hovyo hovyo na mnamcheka Juu

Badilikeni Kuboresha Mashindano Yenu, Ikiwa pamoja na Kuacha kuwaibia wananchi kupitia kupiga kuraa nashauri Kura Zitumike kwa Washiriki mlio wapeleka Top 3
 
Kwenye BSS ni Master Jay na Salama ndio wenye ufahamu na sikio kuhusu music.

Ila pamoja na hayo ukisilikiza judgement zao kwa washiriki hazina weledi wa kimuziki Madamu Rita yeye ndio mtupu kabisa.

Kwa ufupi BSS inafelishwa na majaji wake.
 
Kwenye BSS ni Master Jay na Salama ndio wenye ufahamu na sikio kuhusu music.

Ila pamoja na hayo ukisilikiza judgement zao kwa washiriki hazina weledi wa kimuziki Madamu Rita yeye ndio mtupu kabisa.

Kwa ufupi BSS inafelishwa na majaji wake.

Ni kweli kabisa Wana Judge kama Sio watuu wanaofahamu mziki
 
Na me nimeiona hiyo interview kiukwel master Jay yupo sahihi kwa asilimia 100 sema tu watanzania hawapendi ukweli hamisi hajua kuimba na shindano sio kwaajili ya kuonea huruma watu Bali kupata watu wenye vipaji kazidiwa Sana na waimbaji wenzake Sana.

Nakubaliana na Wewe 100% lakini Je kulikuwa na Ulazima Kumsema Mshiriki ambae bado Hajatoka Yupo kwenye Mashindano?
 
hakuna kitu kinaboa kama huu upuuzi wa ma- judge kujigeuza Mungu watu, ilihali mashindano yao pasipo uwepo wa hao washiriki wanao wakejeli na kuwadhauri hayawezi kufanyika!

#ni wapuuzi sana na ushamba ndio unawasumbua, wajifunze kupitia kwa wenzao huko mambele...
 
Mkuu unaangaliaga America Next Top Model???

Kuna mdada anaitwa Tyra Banks unamjua??

Huyo kwa kukosoa na kutoa makavu ni kiboko, hata huyu Salama na Master J hawamfikii hata kidogo.

Muda mwingine kukosolewa kunaweka kukujenga zaidi badala ya kukubomoa, Hamis achukue hiyo kama motisha na aongeze juhudi, Si lazima uwe na kipaji ili utusue, juhudi na kujiamini vinaweza kuwa njenzo muhimu sana kwenye safari ya mafanikio.

Hamisi kama utasoma hili bandiko na kuona hiyo interview ya Master J plz isikukatishe tamaa bali ichukulie kama udhaifu wako na pambana ili kuondoa huo udhaifu wako.

Ukiona matatizo mengi basi msimu wa mavuno umekaribia.
 
Tatizo Hamisi anataka kushinda kwa huruma ya wananchi,anatiatia huruma km paka wa bar/mgahawani.
Kipaji hamna pale na huo ndio ukweli akitaka aongeze juhud tu maana unaweza kuwa huna kipaji lakin juhudi zikakufanya utusue.Practice makes perfect.
 
Ni kweli kabisa Wana Judge kama Sio watuu wanaofahamu mziki
Master J ni mkongwe sana kwenye tasnia ya mziki, unashangaa kwanini amekengeuka au ndo kisurisuri kimemfika. Lakini hata salama hayupo salama sana mana kuna kipindi walimfichaga kwa sababu ya vijimaneno vyake vya kuhudhi.
 
Master J ni Mtu wa hovyo kabisa katika hiyo BSS. As a judge, hakupaswa kusema zile takataka zake. Ana madharau ya kishamba, unawavunja moyo washiriki wa BSS, na zaidi ya yote anajivunjia heshma hata yeye mwenyewe!
 
Hebu angalia american Got talent na american Idol utakuja futa uzi wako mwenyewe. Judjes kule wanampa mtu makavu live hawakwepeshi ni bora umwambie mtu ukweli direct kuliko kumpaka mafuta kwa mgongo wa chupa. Cc Simon Cowel
 
Itakuwa alikuwa bwax maana mzee wa tungi sana huyu
 
Issue hapa sio hamisi kuwa na kupaji au la. Issue hapa ni kwa nini judge awe bias tena kwa mshiriki ambaye bado yuko mashindanoni.

Tafsiri yake ni kwamba hamisi hata aki perform vipi hawezi kumpa kura yake.
 
kwani kasema maneno gani?
Halafu kauli mbovu hazinaga mwenyewe hata huko AGT simon yanamtokaga sana maneno mbona, Mel b aliwahi kumnanga Mtoto mdogo wa miaka 9 mbele ya Hadhara, The four meghan aliwahi kumnanga kendyle paige na washiriki wengine live live...
kwahiyo haya maneno maneno hata majuu yapo mkuu hakuna penye uafadhali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…