Master J na BSS

Master J na BSS

Ofcoz hamis hajui sema wabongo mnapenda kiki na upepo hajui ukilinganisha na washiriki waliopo akina mesha amezing hamisi ni uchafu tu na BSS wameamua kumrudisha tu ili kupunguza makelele ila dogo ana uwezo wa kawaida sana
 
Tatizo Hamisi anataka kushinda kwa huruma ya wananchi,anatiatia huruma km paka wa bar/mgahawani.
Kipaji hamna pale na huo ndio ukweli akitaka aongeze juhud tu maana unaweza kuwa huna kipaji lakin juhudi zikakufanya utusue.Practice makes perfect.
Nakubaliana na wewe jamaa anakipaji sawa ila sio cha kiwango ambacho watu wanamweka alipaswa atoke hata kwenye makundi hiyo 20 bora sijui kaingiaje wametoka akina elisha hans
 
Ha ha! Hamisi karudishwa kwa kelele za watu na huruma ya madam rita,ukiangalia wakati anarudishwa kuna kauli ilitoka kwa madam kwenda kwa master j!! Mgogoro umeanzia kwao majaji ila madam ndio mwenye kauli maana ndie boss!!, Hasira za master j zimemuangukia hamisi na si boss wake atakosa ulaji.. madam kwake ile ni biashara.. ila hamisi kwa wale si kitu asubirie kulamba galasha tu😎😎
 
Nakubaliana na wewe jamaa anakipaji sawa ila sio cha kiwango ambacho watu wanamweka alipaswa atoke hata kwenye makundi hiyo 20 bora sijui kaingiaje wametoka akina elisha hans
Elisha Hans huu mwaka wa pili anashiriki na kutoka katika hatua hiyo hiyo.
 
Point ya mleta mada ipo clear.
Huwezi kumsema mshiriki vile wakati bado yupo kwenye mashindano.

Halafu kwa namna anavyoimba Hamis na kupiga gita ukisema hajui kitu huo unakuwa uchawi.
Bss ya awamu hii inawashiriki wa kawaida sana ambao ni level yake kabisa.

Master J anaonekana wazi huwa anaendeshwa na hisia badala ya professionalism.

Watanzania walivutiwa na Hamis kwakuwa alionesha uwezo ambao hakuna aliyetarajia. Alionekana hajakaa kisanini yaani kilimbukeni, pia muonekano wake ni wa mtu ambae Huwezi kudhania anaweza kupiga gita vile.

Tabia za Master J zinawafanya madogo wengi wenye uwezo kushindwa kujitokeza Bss kwani pale unakwenda kudharirishwa tuu.
 
Nimefuatilia Interview aliyo ifanya Master J Na Refresh Ya Wasafi FM, Kama Master J upo Humu naomba Nikwambie na Niku JUDGE kuwa Wewe huwezi kufanya INTERVIEW na Sio JUDGE Mwenye Elimu Ya Kuwa Judge like huna Maadili Ya Kazi! Sisemi Kwa Ubaya Ila Nakwambia uweze Kujirekebishaa, Hamisi Ni mshiriki ambaye yupo Kwenye 20 Bora ya Mashindano na sasa Shindano Lipo mikononi Mwa wananchi Mkiwasisitiza Wapige Kuraa Kwa Wingi kwa washiriki wanao Wapenda Ikiwa Na maana Kuwa Mmeachia Wananchi Wafanye Judgement!

Ni kweli Kabisa Hamisi Hana Kipaji kama unavyosema nakubaliana na Wewe lakini Unawezaje kwenda kwenye Interview na kuanza Kusema Maneno Ha Hovyo kama Yale kwa Mshiriki ambaye bado Yupo Kwenye Mashindano? Angekuwa Ametoka Kwenye Mashindano Sawa lakini Mshiriki bado yupo kwenye Mashindano then Unatoka Unaenda Kwenye Media Nakuanza kusema Maneno Ya hovyo hovyoo As If Mmegombana na Hamisi? What If Hamisi Akiona Hii Interview Atajisikiaje? Atapa Ujasiri Tena wa Kuimba japo Hajui? Hamisi bado ni Mtoto sana Lakini Unawezaje Kusema Maneno kama Yale kwamba Hajui like ni na nini ikiwa wewe ni Moja Ya Majudge kwenye hayo Mashindano Na Mshiriki bado yupo kwenye mashindano?

Unanifanya Niamini wale Ambao huwa wanasema BSS huwa inakuwa na Mshindi wao Tayari Toka Siku Ya Kwanza? How unaenda Kumjudge Mshiriki kwenye Media? Inamaana Zile Kula Wanazo Piga Wananchii hazima Nguvu,wala Umuhimu wowote Ule... Kwanini mnaendelea kuwatoza Pesa wananchi kwa kusema wapige kura kwa Mshiriki ambae mnajua Hata pitaaaa na hana Kipaji? Huo si ndio Wizi? Kama Mshikiri Kushinda ni Kigezo cha Kura Basii Tuseme Hamisi Ni mshindi!

Then Uache Kumuiga Sallama Kwa Kuwa hayupo kwenye Mashindano basi wewe ndio unataka uwe Yeye... Salama Atabaki kuwa Salama, Isiwe Sababu sasa Ya Wewe kila kituu kukataaa Yaani Kifupi washiriki wote waliopo kwenye Top 20 wewe uliwasemea NO na maneno kibao kisa Washiriki wakuogope wewe na Waseme kuwa Tuna Salama Mwingine! Fanya kazi kwa Uweledi na Kwa Akili!

Huwa nashangaa sana Judges Wa BSS wanavyomsema Vibayaaa mshiriki akikosea Kuimba Anasemwa As If kaiba sijui? kwanini Msijudge kwa hekima kwa Mshiriki Ambae Hajafanya Vizurii hamuoni Mashindano Makubwa kama AGT wanavyo judge? Maneno Yenu ya Kejeli mnapoteza Washiriki Wazuri kwa Kuogopa Maneno Yenu ya Hovyo hovyo na mnamcheka Juu

Badilikeni Kuboresha Mashindano Yenu, Ikiwa pamoja na Kuacha kuwaibia wananchi kupitia kupiga kuraa nashauri Kura Zitumike kwa Washiriki mlio wapeleka Top 3
Huruma za kiboya km hizi ndo zinasabisha tupate washindi mabwege ambao hawawez kujisimamia na wanapoteaga mazima...wapi jumanne Idd?
 
Mkuu unaangaliaga America Next Top Model???

Kuna mdada anaitwa Tyra Banks unamjua??

Huyo kwa kukosoa na kutoa makavu ni kiboko, hata huyu Salama na Master J hawamfikii hata kidogo.

Muda mwingine kukosolewa kunaweka kukujenga zaidi badala ya kukubomoa, Hamis achukue hiyo kama motisha na aongeze juhudi, Si lazima uwe na kipaji ili utusue, juhudi na kujiamini vinaweza kuwa njenzo muhimu sana kwenye safari ya mafanikio.

Hamisi kama utasoma hili bandiko na kuona hiyo interview ya Master J plz isikukatishe tamaa bali ichukulie kama udhaifu wako na pambana ili kuondoa huo udhaifu wako.

Ukiona matatizo mengi basi msimu wa mavuno umekaribia.
Kwenye Tusker project fame kulikua na judge aitwa Ian mkuda balaa,kile chuma noma but kasaidia sana kuwajenga washiriki kwa ukuda wake
 
Huyo Hamis sijui anaimbaga mini zaidi ya kutoa risala. Au kwa vile kafanana na konde boy?
 
Back
Top Bottom