Siku niliyoacha kuangalia BSS ni siku ile nilipoona ubaguzi wa rangi wa waziwazi. Jopo zima la majaji.
Sikumbuki ilikuwa ni mwaka gani, ila nachokumbuka ni mzungu kushiriki tena alikuwa anapendwa mno hata tano bora akafika. Kilichomponza ni rangi yake, majaji hawakumpenda pia.
Yaani jamaa akawa akiimba anamaliza, cha kukosoa wanashindwa zaidi ya kumwambia maneno mabaya. Ikiwemo "Unajua wewe ni mjanja sana, umechagua nyimbo zinazopendwa tu na mashabiki" "Mashabiki wanachanganywa tu na hiyo rangi yako, wakitokwa na hali hiyo hawatakushangilia kabisa"
Yaani huwa tunalalamika ubaguzi kwa wenzetu akibaguliwa mwenzetu. Ila tunasahamu sisi ni wabaguzi kuliko.
Ukweli mchungu lile shindano Mzungu alishashinda kwa kura na hata uimbaji, kulifanyika figisu. Ndiyo nikaacha kuangalia hadi leo hii.
Hakuna cha kutafuta vipaji wala nini, wanapanga ashinde nani hata kama hana vigezo.