Masters/Phd bila ya kupitia A - level!

Slim5

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2014
Posts
28,203
Reaction score
37,906
Habari za Jumapili wapendwa.

Napenda kuchukua fursa hii kuwajulisha vijana wetu fursa tajwa hapo juu. Mwanafunzi aliemaliza kidato cha 4, na credits zake hazitoshi kumuwezesha kuendelea na A - level, anayo fursa ya kuendelea na masomo mpk lvl ya phd. Anatakiwa kuwa mvumilivu na afanye hivi:


  1. Anaenda kujiunga na moja ya vyuo vya VETA (ada ya VETA kwa mtoto wa boarding ni wastani wa 250,000 Tsh kwa mwaka, na wale day scholars ni 125,000 Tshs kwa mwaka).
  2. Akifanikiwa kupata cheti cha VETA (inawahusu fani kama - Mechanics, Eloctronics, Lab tech, IT etc), anaomba kufanya diploma Arusha tech, Mbeya tech, WDMI etc
  3. Baada ya hapo safari inaendelea mpaka Bachelor, Masters mpaka phd!

Nimewasilisha.
 
Mkuu mbona unarahisisha maisha ya elimu hivi? Kwanza ukijumlisha mwaka mmoja wa VETA, miwili (sijui ni mitatu) ya diploma za hiyo mechanics kwa upande wa muda ni sawa tu na kuresit na kupiga A level. Pili, mtu aliyekosa credit O-level ana nafasi finyu sana ya kufanya vizuri kwenye vyuo vya technical...kule ni pure science na lazima uwe mzuri kwenye at least physics na maths! Kwa mwanafunzi kama huyu aliyekosa credit ni bora akomae na kutafuta credit halafu akachague kozi zisizohitaji msuli mnene!
 

Mkuu mchng wk mzuri. Sijasema waliokosa credits, nimesema waliokosa nfs za A lvl. Na kwa hizo coz wenyewe ni pcm, egm, pcb n.k, hiyo pure maths haianzii juu mkuu, inaanzia chini, chini ndio VETA!
 

Nahisi anafikiri shule ni kazi ndogo. mechanics siyo tamthilia za ngoswe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…