Mastori: Unaifahamu laana ya maarifa(Curse of Knowledge)?

Mastori: Unaifahamu laana ya maarifa(Curse of Knowledge)?

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Joined
Jan 31, 2021
Posts
11,884
Reaction score
21,175
Umewahi kutana na mtu ana maarifa mengi lakini anapata tabu au ni kama 'mvivu' kujieleza. Pamoja na sababu nyingine hii inaweza kuwa imesababishwa na laana ya maarifa.

Curse of knowledge ni kitendo cha mtu mwenye maarifa kudhani kuwa kila mtu anayo hayo maarifa. Yaani mtu anaamini anayoyafahamu karibu watu wengi wanayafahamu. Hivyo anapokuwa anazungumza kuna vitu anaviacha akiamini watu wanavijua tayari. Kumbe sivyo. Hilo linamfanya aonekane mzungumzaji asiyeeleweka au haelewi mambo.

Epuka hii laana. Unapozungumzia jambo jitahidi kufafanua yote yanayohusika. Ila sasa siyo ndiyo uwe na maneno meeengi.
 
Back
Top Bottom