Raphael Alloyce
Senior Member
- Nov 15, 2020
- 128
- 372
"TUNAONA TAABU SANA KUUNGANA KUMKABILI MWENYE NGUVU. WENYE NGUVU WANAUNGANA KUMKABILI MNYONGE," Mwl. Nyerere
Kama ningekuwepo wakati wa Mwalimu Nyerere, ningemuuliza swali hili: Ni rahisi kwa kiasi gani kwa Mwafrika kumwamini Mwafrika mwenzake katika dola, ili waweze kuungana?
Kwa sababu hayupo, inabidi tuendelee na hili....!
Moja ya adhabu kubwa sana tuliyopewa Waafrika ni kutoaminiana sisi kwa sisi na badala yake kuwaamini wale waliotutawala na kuwategemea hadi kifikra. Tunaenda mbali zaidi, tunaamini kwamba wao wapo kwa ajili yetu.
Mhafrika ndiye kiumbe pekee ambaye amepewa tuzo ya kuwa msaliti bora kwa Waafrika wenzake.
Mwafrika ndiye kiumbe ambaye haiamini uwezo wa akili yake mwenyewe. Isipokuwa akiwa na dola, anaamini yeye ndiye MUNGU.
Mwafrika ndiye kiumbe ambaye anapewa elimu inayowasifia wenye nguvu kuliko yeye (mnyonge).
Mwafrika huyuhuyu ni yule ambaye anashindwa kujisimamia mwenyewe kuanzia kwenye familia, kijiji/mtaa, n.k., na kuilaumu serikali yao kwa kila jambo ambalo hata wao wenyewe wangeweza kuungana na kulitatua.
Huyo ndiye Mwafrika. Sasa ukiwa hivyo, utaungana na nani wakati wote wamekaa kimagendo magendo?
Hata kwenye familia hakuna kuungana kati ya mke na mume; wote wamekaa kimagendo magendo. Utasikia, "Rafiki wa Mwanamke ni Mwanamke," mara "bora niwe single mama/single baba," n.k. Imekuwa utaratibu vijana na wazee hawaaminiani.
Huu ni ulimbukeni kama ulimbukeni mwingine ulioikumba Bara la Afrika. Karne ya leo hii hao wenye nguvu wanaleta midori kwa ajili ya kukidhi akili za ngono za Mwafrika. Je, Waafrika na vizazi vyao vitaendelea kuwa salama?
Kutana na hili bara ambapo wanasiasa wanaamini wao ndio wenye haki miliki ya Bara la Africa. Wengine wote wamebaki kutapatapa.
Itawezekana vipi kwa Mhafrika kumsaidia Mwafrika mwenzake katika kujilinda na kujitetea dhidi ya wenye nguvu ikiwa hata Mwafrika mmoja-mmoja mawazo na mtazamo wake ni mparaganyiko?